Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
JF kiboko tetesi za kuamia habari corporation nilizisikia hapa hapa JF yapata wiki 3 au 4 zilizopita, nasubili comment ya Matola kwanza
 
Last edited by a moderator:
Jamii Forum ni kiboko sana.
Kuna wadau walisema wiki tatu zilizopita kuwa huyu Kibanda anakwenda kuajiriwa Habari Cooperation, hivyo zile makala zake za kumsifia Kinana na kuwaponda Chadema zilikuwa ni chokochoko za kuanzisha bifu na mwajiri wake(Mbowe) ili aondoke kwa visa, lakini watu walimwangilia tu na sasa kaamua kuvaa magamba wazi.

Hata haya anayoambiwa leo , ndiyo yatakayokuja kutokea , watu wameusoma mchezo siku nyingi sana .
 
Absalom Kibanda, ameenda kukumbatiwa na mafisadi kudaadek...ni haya haya yaliyompata Salva Rweyemamu...

Ama kweli penye uzia penyeza rupia.

Naomba ndugu Ansbert Ngurumo achukue nafasi yake fasta...namuaminia Ansbert...Go to hell Absalom
 
Huku anaenda kuwa chini ya msomali Bashe ngoja tuone
Nchi yetu hii tamu kweli kweli! Nataka nione zile makala motomoto za kuichachafya serikali na CCM zikitoka kwenye magazeti ya New Habari!

Ndugu Mwita Maranya yametia yaliyonenwa na manabii
 
Last edited by a moderator:
Si alikuwa na kesi kama mhariri mkuu ama ndiyo imeisha sasa? any way, agenda 2015, matayarisho ya kinyang'anyiro, bahati mbaya magazeti hayasomwi vijijini afadhali ingekuwa radio. Kazi njema mkuu, tunategemea kuona ile kitu inaitwa 'objectivity' katika yote ufanyayo katika tasnia.
 
Nani asietafuta kazi yenye maslahi, hata Rose kamili mzazi mwenza wa Dkt Slaa alitumikia udiwani kupitia CCM MPAKA 2010 pale alipomwagwa na Dkt Nagu!mwacheni akatengeneza maisha ya watoto wake , kwani faida ya gazeti si inatiwa kwenye mifuko ya Mbowe!
 
Good riddance, alikuwa hana msimamo imara!! Ansbert Ngurumo will do a better job.
 
kila kitu kimefungwa na majira ni wakati wake wa kwenda kupata challenges mpya ya kazi yake
 
Aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda, leo ameaga rasmi na kuachia nafasi yake mhariri mtendaji, kwa maelezo kuwa anaenda kujiunga na kampuni ya New Habari Corporation 2006, inayochapisha zaidi ya magazeti manne hapa nchini.

Akiongea na wafanyakazi wa gazeti la Tanzania Daima leo asubuhi, kibanda alisema sababu kubwa ya kuondoka hapo ni kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika majukumu yake ya uandishi.

Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa,

hapo kwenye red, ni kweli kwa sababu yeye ameshindwa kutimiza hayo, bora awaase wenzake waendeleze, na yeye aproceed na kunakomfaa, tunamtakia heri aendako. na yote ni observations zetu tu, bado hatujasikia from both parties
 
Kuondoka kwa Kibanda ni faraja kwa sisi tuliokuwa tunaona kuwa ameanza ku-lipoteza mvuto Tanzaniadaima.

Tusihemke kila mpango wa mabadiliko mwenyezi Mungu anauratibu, ameanza kutenganisha chuya na mchele.

Heri anaondoka kuliko angeendelea kubaki.
 
Sasa Prince Bagenda anaenda wapi? Au keshatemeshwa kibarua na kurudi Tazama?
 
Safi sana kibanda kwa kukataa kuwa zoba haiezekani ulazimishwe kuandika mazuri ya CDM tuu hata kama wamekosea sasa nenda ukawaonyeshee kipaji chako Jembeeee
 
Kile kilichfikiriwa na wengi kuhusu Mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania daima Absalom Kibanda kuwa yupo mbioni kuondoka katika gazeti hilo, kimetimia.

Kibanda amehama rasmi na kuaga leo na anahamia kule ambako wengi mlitabiri kabla hajaenda. Pengine stori alizoandika zilikuwa za kuhujumu wapambanaji wengi, lakini mapambano yataendelea na sisi tunamtakia Kazi njema kwa Husein Bashe.

Kilichosemwa siku zote kuwa jamaa yupo kwenye pay roll ya EL, ninajaribu kukubali. Kazi kweli kweli................

Pesa inanunua kila kitu, wenye pesa wananunua hata wahariri na waandishi, ukombozi wa nchi yetu unahitaji vita kubwa zaidi ya tunavyodhani..........

BOSS wa TEF, sasa yupo kwa BASHE!
 
Hawawezi mkuu labda iwe ni mkakati wa kambi yao.Pengine mkakati wa kumshughulikia Mbunge wa mtama na kiongozi ajaye wa upinzani (baada ya uchaguzi mkuu 2015)Sasa huko alikoenda kuna changamoto gani?

Ben ishu ya habari corporation ni very controversial hasa msimamo wao kuhusu mbunge wa mtama, natabiri kutakuwa na tofauti kubwa kimtizamo kati ya kibanda na bagenda pale habari corporation, Bagenda haeleweki eleweki kuna muda amekuwa mtata na kuonekana kama anambeba mbunge wa mtama, pengine sasa kibanda kaletwa mahususi kumkangaa na kumdhibiti bagenda.lets wait and see
 
Mkuu Yericko,

huu ndiyo unafiki wa hawa watu.Lakini katika safari ya mabadiliko ni lazima tupate moyo hasa tunapoona kasi ya usaliti inaongezeka.Kama mimi kadiri ninaposalitiwa ndivyo kasi yangu na ari ya kupambana inapokua juu.Let us move on comrade!

Umenena mkuu,

Enzi zetu kulikuwa na ngoma inaitwa mdundiko, siku hizi siusikii sana. Mdundiko ukianza kila mtu anaingia anafuata ngoma kwenda unakoelekea. Mbele kunakuwa na mshika bendera. Mdundiko ukifika unakokusudiwa kwenda, mshika bendera anaitua bendera yake na kuikita ardhini. Baada ya hapo mpigo wa ngoma hubadilika, siyo mdundiko tena bali huitwa 'vanga'. Inabidi ujue namna ya kucheza mdundiko wa vanga, sio rahisi kama ule wa kutembea. Wengi waliokuja na msururu kufuata mdundiko ikifika hapo huachia ngazi.

Ndipo tunapowaona watu kama hawa kina Kibanda, na tusishangae, wengi tu tuko pamoja kwenye hatua ya mdundiko. Siku zinavyozidi kwenda mbele mmoja mmoja wanaachia na wataachia ngazi. La maana ni kuwafahamu na kutoshangazwa na hilo. Wajuzi wa kulicheza 'vanga' tutaendelea hata baada ya mpigo wa mdundiko kubadilika.

Mpaka kieleweke!
 
Aje tena hapa akane kutumika kuichafua CDM.By the way tunamtakia kila la kheri.
Kamata jahazi Ansbert Ngurumo
 
Kweli kazi ya uandishi wa habari Tanzania haina tofauti na uuza baa. Jamani Kibanda kama aliyokuwa akiandika yalikuwa yanatoka moyoni, huko ataandika nini au ni wale wale akina Salva Rweyemamu. Kweli namna hii hatuwezi kuendeleza nchi yetu. Yaani kila mtu anapigwa bei kienyeji hivi hivi.
Atakuwa kama Tambwe akiwa NCCR then KAFU leo bado anasema tu Ubaya wa wapinzani so Kibanda kaanza
 
Kwani alikuwa na hisa tanzania Daima, wacha akatafute maisha popote

Kibanda ni mchumia tumbo siku nyingi hivo sishangai kama anaweza kuacha jukumu zito alilokuwa amejitwika kwa manufaa ya wengi na kwenda kuliko na maslahi zaidi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom