Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
"Tukiwakamata Mafisadi, Uchumi wa nchi yetu utayumba".....Mizengo Kayanza Peter Pinda, Bungeni 2011

Napenda tu kutambua kwamba kwenda Habari Cop. kwa huyu jamaa ni pigo kwa mageuzi nchini. Alikuwa mwana mageuzi mzuri na tamaa ya maslahi zimemwondoa. Alikuwa askari hodari ila hakuwa Imara. Ameshindwa kusimamia anachoamini na uzalendo wake kwa tamaa ya fedha. Ni pigo kwa mageuzi na ninasikitika! Ameshindwa kuwa imara lakini uhodari wake ulikuwa na faida kubwa sana kwetu! Tutamkumbuka kwa uhodari wake na tutasikitika kwa kutokuwa kwake imara!
 
Mwisho wa siku utasikia ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya (DC)
 
Sina shaka atajutia. Wametafuta namna ya kumnyamazisha wameshindwa wameamua kutumia kanuni ya sticks and carrots. Wakishampa kibarua baada ya muda watamtimua abaki kuhangaika. Ni uamuzi mbaya amefanya ingawa ni haki yake na shauri yake. Time will judge us kindly and timely. Kweli adui yako muombee njaa na tamaa mbele mauti nyuma. Ni bahati mbaya kuwa taaluma ya habari imevamiwa na mdudu ufisadi na umasaburi.
 
Naanza kupata hofu kuwa uandishi wa habari unaanza kugeuka uchangudoa. Bahati mbaya sana tatizo liko katika taaluma nyingi kama si zote. Juzi juzi Tundu Lissu aliwashukia majaji vihiyo na wasio na maadili wala sifa. Nini kimefanyika? Kama tunao viongozi wa hovyo waliotokana na rushwa, kuchafuana na uchakachuaji unategemea nini. Siku zote nasema madili yamechukua nafasi ya maadili. Kibanda amejivua nguo. Wamempa karoti amezidandia. Watampa kazi baadaye wamtimue baada ya kuona kuwa integrity yake imo msambweni. Alikuwa shujaa ataishia kuwa coward. From a hero to a villain! Shame on you Kibanda! Nenda ukale ugali na Rweyemamu Mihingo na Salva, Balile, Bagenda, Shoo na mbwehe wengine waliouza utu na taaluma zao kwa vipande thelathini vya fedha fedheha.
 
Kila la heri Kibanda katika kazi yako mpya ya kuusafisha mkaa
hadi utakate na kuwa mweupe. Usijali ilimradi siku zinakwenda...
 
Kibanda ni mchumia tumbo siku nyingi hivo sishangai kama anaweza kuacha jukumu zito alilokuwa amejitwika kwa manufaa ya wengi na kwenda kuliko na maslahi zaidi!

Mkuu Mulama hao huwa nawaita wasaka tonge!
 
Last edited by a moderator:
Si maslahi na wala si bifu na muajiri wake huu ni uamuzi wake, tukijifunza kuheshimu uamuzi wa wengine tutakuwa katika njia sahihi tuitakayo, hata kama hatukubaliani nao.halikuwa bifu na waajiri wake wa awali kama inavyavysemwa hapa, ule ulikuwa mtazamo wake katika kuonyesha kile anachoamini ni jukumu la wale watakaoona ukumbusho ule unawafaa watumie na wasioutaka waache
Huu mtazamo wake ulianza kubadilika pale wazo la kuhama lilipomjia?
 
Hawawezi mkuu labda iwe ni mkakati wa kambi yao.Pengine mkakati wa kumshughulikia Mbunge wa mtama na kiongozi ajaye wa upinzani (baada ya uchaguzi mkuu 2015)Sasa huko alikoenda kuna changamoto gani?
Mzee akiingia magogoni, jamaa atakuwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano kama Siliva Rweyemamu
 
Jambo moja lililokuwa linanishangaza ni kwamba inakuwaje Ansbert Ngurumo kuwa naibu wa Kibanda?ni kama vile Ferguson kuwa kocha msaidizi chini ya kocha mkuu Brendan Roggers!
 
Karibu nyumbani Kinana Kafanya kazi

Uchumba ulianza hivi



images



Welcome Meeeeeeeeeeeeennnnnnnnnnnnnnnnn:target::target::target::target:😛op2:😛op2:😛op2:😛op2:😛op2:
Ni kama anasema,Aisee Salva unajua hata wewe umekula shavu kwa kuwanyuka wapinzani?Kama vipi liwalo na liwe naachana na umma naangalia tumbo langu,naja kwa mafisadi kuwalamba miguu nitwaandika vizuri,nitawapamba na hatimaye na mimi nikale vyuku magogoni kama wewe bhana!!!!!!....My take,Eee Mungu tuokoe na hili balaa la njaa!!!
 
Hii ya Kibanda tamu sana, maana kuelekea chaguzi zijazo ndege wanaofanana lazima waruke pamoja, hivyo imekuwa ni rahisi sana kwa FreeMedia kuondokana na Kibanda ambaye atafiti vizuri mnoo huko New Habari. Kila la kheri Kibanda,mwandishi nguli
 
Duh! Alikuwa Balile, akaja Peter Nyanje (yeye alienda the Citizen kama sikosei). Pia kuna Kulwa Karedia alienda Habari corporation. Sasa Kibanda. Yangu macho.

Namwaminia Ansbert Ngurumo.

Mkuu The Invincible'

Hata mimi namwaminia sana Ansbert Ngurumo.

Kilichomuumbua huyu Kibanda hata asiondoke kwa heshima ni pale alivyoanza kushambulia Chadema kumbe tayari alikuwa na ajira mpya mfukoni.

Tunatumaini huko New Habari kila siku atakuwa anatoa makala ya kumsifu Kinana.
 
Last edited by a moderator:
Aende zake akagange njaa new habari kwa msomali bashe...kuna jembe Ansbert ngurumo atachukua nafasi yake.namuomba ansbert ngurumo atoe maswali magumu kuhusu kibanda.
 
Kibanda anaweza kuwa kakosea.Problem ni pale ambapo tutampinga kwa sababu tu ya kuliangalia Tanzania daima kichadema zaidi.Hata huyo mhariri mkuu ajaye awe objective tu.Asiandike kwa maslahi ya mwajiri wala wapambe wa mwajili.Kutimiza hili kwa ukamilifu kabisa bila kupingwa hasa humu Jf ni kama vile haiwezekani.Napenda magazeti yasiyo ya vyama kama tanzania daima yawe huru zaidi kukosoa na kusifia pale panapostahili.Sio always kukosoa upande mmoja na kusifia upande mwingine.Kama tunataka Tanzania daima litufurahishe kila siku basi either liwe la chama chetu au chama chetu kie very perfect.
 
Nakumbuka kuna kipindi nilimwandikia sms baada ya kusoma makala yake, nikamwuliza kwanini anaandika kama mwandishi wa Mtanzania? Kumbe ndio alikua anelekea. Kimsingi ametumika sana hata akiwa Tz daima! Nakumbuka Sitta na Mwakyembe walikua wanalilalamikia sana Tz daima!! Kila la kheri huko uendako mpendwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom