Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
Companero,Mkuu nadhani sasa unafanya utani!...
Hata hivyo nitakujibu kwa ufupi pamoja na kwamba sielewi nia yako..
Ukomunist ni itikadi inayopinga Ubepari, ni mfumo wa kiuchumi ktk jamii unaolenga kuondoa tabaka za wananchi wake kati ya matajiri na maskini ambapo maskini ndio kiini cha uzalishaji huo. Haubebi chochote toka upande wa pili (Ubepari).
Ni mambo yapi ya Kikomunist, Nyerere alioyaweka?...
1.Uchumi wa nchi kuwa mikononi mwa serikali badala ya matajiri wachache!
2. Utumiaji maguvu ktk utekelezaji wa sera... Hapa nakuomba unielewe kuwa kama kitu ni RIGHT ya mwananchi basi right hiyo ni lazima uitumie utake usitake, usipopokea unavunja sheria. Mfano ndio hayo ya kuhamia vijijini.
hayo machache unasemaje mkuu! yametosha au kuna jipya!
Sitanii Mkuu. Tuna tabia ya kusingizia watu wamefanya hiki na kile. Tukiulizwa tutoe ushahidi tunashindwa hata kutoa hoja 3. Kama huo uliouelezea hapo ni Ukomunisti, je Ujamaa, Usoshalisti, Umaksisti, Ufashisti na 'Ubepari wa Dola' ni nini?
1. Uchumi wa Libya uko mikononi mwa Serikali, je Libya ni nchi ya kikomunisti?
2. Idi Amini Dada alitumia maguvu, je Uganda ilikuwa ni nchi ya kikomunisti?
Unajua ni makampuni mangapi ya kigeni Mwalimu hakuyataifisha na yaliendelea kuushikilia uchumi wa nchi? Umehesabu ni matajiri wangapi wa Kihindi na Kizungu waliendelea kushikilia uchumi wa nchi wakati wa Mwalimu?Umeorodhesha ni sera na programu ngapi za Kibepari kutoka WB na USAID Mwalimu alizitekeleza katika miaka ya 60 na 70?
Narudia, Mwalimu hakuwa Mkomunisti. Yeye mwenyewe alisema hivi:
European socialism was born of the Agrarian Revolution and the Industrial Revolution which followed it. The former created the "landed" and the "landless" classes in society; the latter produced the modern capitalist and the industrial proletariat.These two revolutions planted the seeds of conflict within society, and not only was European socialism born of that conflict, but its apostles sanctified the conflict itself into a philosophy. Civil war was no longer looked upon as something evil, or something unfortunate, but as something good and necessary. As prayer is to Christianity or to Islam, so civil war (which they call "class war") is to the European version of socialism--a means inseparable from the end. Each becomes the basis of a whole way of life. The European socialist cannot think of his socialism without its father--capitalism!Brought up in tribal socialism, I must say, I find this contradiction quite intolerable. it give capitalism a philosophical status which capitalism neither claims nor deserves. For it virtually says "Without capitalism, and the conflict which capitalism creates within society, there can be no socialism!" This glorification of capitalism by the doctrinaire European socialists, I repeat, I find intolerable.African socialism, on the to her hand, did not have the "benefit" of the Agrarian Revolution or the Industrial Revolution. it did not start from the existence of conflicting "classes" in society. Indeed I doubt if the equivalent for the word "class" exists in any indigenous African language; for language describes the ideas of those who speak it, and the idea of "class" or "caste" was nonexistent in African society..."Ujamaa," then, or "familyhood," describes our socialism. It is opposed to capitalism, which seeks to build a happy society on the basis of the exploitation of man by man; and it is equally opposed to doctrinaire socialism which seeks to build its happy society on a philosophy of inevitable conflict between man and man.
Haya endelea kubishana na Mwalimu kama unajua sana kuusemea moyo.