Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,917
- 30,259
TANU NA SANDUKU LA FEDHA LA ABDUL SYKES 1950s
Katika moja ya mijadala ya historia ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika niliwaahidi wasomaji wangu kuwapa historia ya sanduku la fedha la Abdul Sykes.
Nikasahau kwa muda.
Leo msomaji wangu mmoja kaniandikia kunikumbusha nitimize ahadi yangu:
Proved,
Ahadi ni deni na kesho kiyama Allah atatuuliza katika yale tuliyoahidi hatukutimiza.
Mniwie radhi kwani nilisahau.
Ili tupate picha ya Abdul Sykes niruhusini hapa niweke kipande kutoka kwa binti yake Aisha ''Daisy'' Sykes,'' kutoka makala aliyoandika mwaka wa 2018 katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake.
Aisha ‘’Daisy’’ Sykes Buruku ni binti ya Abdulwahid Sykes mmoja kati ya wazalendo 17 waliounda chama cha TANU kilichopigania uhuru wa Tanganyika.
Daisy kama anavyofahamika zaidi kwa jina hili, ni msichana wa kwanza Mwafrika kusoma Shule ya Wasichana ya Aga Khan mwanzoni mwa miaka ya 1950 na msichana wa pili kuingia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1960.
Daisy amefahamiana na wazalendo wengi mmoja wapo akiwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na machifu mashuhuri kama Mangi Mkuu Thomas Marealle waliokuwa wakifika nyumbani kwa baba yake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Katika kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha baba yake, Daisy aliandika makala kukumbuka siku zile zilizojenga haiba ya baba yake na ya wazalendo walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kwa miaka mingi Daisy amekuwa akiishi na kufanya kazi nje ya Tanzania.
Daisy anasema: ''Wageni mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.
(Angalia picha ya machifu wa Tanganyika hapo chini 1958).
Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.
Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo.
Lakini aliyeshika nafasi ya juu kabisa katika fikra zangu nikiwa mtoto alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na ni kupitia kwake ndipo tukapata kujua kwa mara ya kwanza kuwa kuna kabila linaitwa, ‘’Wazanaki.’’
Kila alipokuwa anakuja nyumbani kwetu kuja kwake kulikuwa jambo maalum kulikosababisha minong’ono watu wakizungumza kwa sauti za chini wakipeana taarifa kuwa, ‘’Nyerere anakuja au keshafika.”
Kwangu mimi hii ilikuwa ishara ya kutimiza kazi yangu kwani siku zote nilikuwa nikiambiwa kutengeneza kifungua kinywa cha chai na mayai kila alipokuja nyumbani akitokea Shule ya Mt. Francis, Pugu alipokuwa akisomesha.
Nakumbuka katika akili yangu ya kitoto kumuona Mwalimu Nyerere akiishi nyumbani kwetu kwa muda katika nyumba yetu ya Mtaa wa Stanley baada ya kuacha kazi wakati marafiki zake wa karibu baba na Dossa Aziz walikuwa wanamtafutia nyumba ya kuishi.
Ilikuwa katika kipindi hiki cha mimi kuanza kupata akili katika kukua kwangu ndipo nilipokutana na wanawake wazalendo waliokuwa wanaochipukia katika uongozi wa Tanganyika, wanawake kama Bi. Lucy Lameck kutoka Moshi, Mary Ibrahim na akina mama wa Kiislam kama Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Hawa bint Maftah, hawa kutoka Dar es Salaam, wote hawa kwangu mimi walikuwa bibi zangu.
Kitu cha kufurahisha ni kuwa hawa akina mama wa Kiislam wote walivutwa katika siasa na Bibi Chiku bint Kisusa, maarufu akijulikana kama Mama Sakina.
(Angalia picha hapo chini akina mama wamevaa mabaibui wako uwanja wa ndege wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO 1955 kulia wa kwanza ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Tattu bint Mzee na Julius Nyerere huyo katikati).
Alikuwa Mama Sakina ndiye aliyewapa hawa wanawake wa Kiislam niliowataja hapo juu utambulisho na wakaja kuwa watu maarufu.
Baba yeye ndiye alikuwa kiongozi wa mikakati hii yote kwa sababu bila yeye kuwatia hima kwa kutumia ushawishi wake ingekuwa vigumu kuweza kuwatia hawa wanawake katika kuwahamasisha wanawake wenzao wa Kiislam na wao watoke majumbani kuja mstari wa mbele katika mikutano wakiimba na kutoa vibwagizo vya kuunga mkono TANU na kudai uhuru.
Hili jambo lilikuwa jipya, jambo ambalo katika utamaduni wetu kwa wakati ule halikutarajiwa na ni kinyume katika utamaduni wetu kwa wanawake wa Kiislam kulifanya katika siku zile.
Prince Karim Aga Khan alipokuja kutembelea shule yetu mwaka wa 1956, wakati ule alikuwa kijana mdogo na akakagua dafatari langu.
(Angalia picha ya Prince Karim Aga Khan hapo chini katika ujana wake).
Jambo hili halijanitoka kamwe.
Lakini zaidi ya haya uhusiano wa baba yangu na jamii ya Ismailiyya ulikuja kujitokeza kwa nguvu sana kwa uamuzi wao mwaka wa 1960 kumuuzia baba Mercedes Benz 280S, DSQ 666, ambayo ilinunuliwa makhsusi kwa matumizi ya Prince Karim Aga Khan pale alipozuru Tanganyika mwaka ule wa 1956.
Kwa siku zile hili lilikuwa jambo adhim na kubwa sana, sisi tukiwa watoto wadogo tukipakiwa na baba ndani ya gari hii nzuri na ya kifahari iliyokuwa rangi ya kijivu, hili lilikuwa jambo lisilo na mfano wake.
Baba alijikita sana katika suala la elimu. Akiwa mjumbe katika bodi ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika taasisi iliyoasisiwa na babu yangu, Abdallah Kleist Sykes mwaka wa 1933, pamoja na wenzake kama Ali Jumbe Kiro, Mzee bin Sudi na wengineo ambao hawa wote walikuwa vile vile katika African Association, alijishughulisha katika kuwaelimisha watoto wa kike.
Shule hii ya Al Jamiatulul Islamiyya iliyokuwa New Street (sasa Lumumba Avenue) jengo lake lipo hadi leo kama kielelezo cha Waislam katika kujiendeleza katika elimu.
Uhusiano wa baba yangu na shule ya Al Jamiatul Islamiyya unakwenda nyuma wakati wa utoto wake yeye akiwa mwanafunzi katika shule hii iliyojengwa na baba yake.
Mwaka wa 1936 akiwa na umri wa miaka 12 na mwanafunzi hapo shuleni alichaguliwa kusoma risala mbele ya Aga Khan, Sultan Mohamed Shah, baba yake Prince Karim Aga Khan huyu kiongozi wa Ismailiya aliepo sasa, alipoitembelea shule ya Al Jamiatul Islamiyya.
Ikatokea kuwa katika jengo hili la shule hii ya Al Jamiatul Islamiyya ndipo nilipoingizwa na baba kuanza chekechea na nikaanza kusoma Qur’an hapo nyakati za asubuhi na mchana nakwenda kusoma shule Aga Khan.
(Angalia jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika hapo chini).
Uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na ulipopatikana ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.
Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.
Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa na kwenye ngazi nyingi wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.
Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake.''
Ndugu zanguni,
Huyo hapo chini ndiye Abdulwahid Kleist Sykes na Mama Daisy wakiwa kwenye dhifa Government House (Ikulu) katika miaka ya 1950.
Naamini mmemwelewa alikuwa kiongozi wa namna gani katika TAA hadi TANU.
Sasa tuje kwenye lile sanduku la fedha.
Kitabu kilikuwa kimetoka na siku hiyo nilikwenda nyumbani kwa Mama Daisy kumpa nakala yake ya kitabu.
Tulikuwa tumekaa kwenye varanda yake nyumba yake Barabara ya Ali Hassan Mwinyi iliyokuwa mkabala na Hellenic Club.
Alikipokea kitabu akawa anatazama picha ya mumewe kwenye jalada na akawa kimya kwa muda mrefu.
Bila shaka alikuwa anawaza maisha aliyoishi na baba yetu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.
Mama Daisy alikuwa shoga wa marehemu mama yangu Bi. Baya bint Mohamed na nyumba zao hazikuwa mbali kwani sisi tulikuwa Mtaa wa Kipata na si mbali na Mtaa wa Aggrey.
Nyumba zao zilitenganishwa na Mtaa wa Kitchwele (sasa Uhuru Street).
Naamini kuwa ile mimi mtoto wa shoga yake kuwa ndiye niliyekuja kuandika kitabu cha Abdul Sykes, mtu ambae historia ilikuwa imemfuta bila shaka fikra hii ilikuwa ikizunguka katika kichwa chake.
''Mwanangu Mohamed, baba yako alijitolea sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika,'' Mama Daisy alianza kusema.
Alikuwa na sanduku lake akiweka fedha zake na kila TANU wakija hapa kutaka kile au hiki yeye alikuwa anaingia ndani analifungua lile sanduku anatoa fedha kuwapa alikuwa hawarudishi mikono mitupu.
Mimi nikawa namwambia, Bwana Abdul taratibu lakini hakunisikia, hakuacha kutoa fedha kwa ajili ya chama chake.
Bwana Abdul alikuwa mtu karimu sana.''