Abdul Kareem Popat ndio sababu hasa ya Azam FC Kukosa mafanikio

AbaMukulu

JF-Expert Member
Jan 1, 2018
2,048
3,568
Abdul Kareem Popat amekuwa CEO wa Azam FC kwa zaidi ya Miaka 7. Huyu ndio CEO ambae hana presha kabisa ya kupoteza kazi yake kutokana kutopewa presha ya mafanikio pale Chamzi Complex.

Kipindi chote cha uongozi wake Azam FC imeambulia kikombe kimoja tuu cha FA (Azam Confederation Cup) mnamo 2019. Miaka yote ya uongozi wa Popat Azam FC imeshindwa kutwaa Kombe la Ligi na kushindwa kufuzu hatua ya makundi kwenye mashindano ya CAF Champions League au Confederation.

Tukumbuke Namungo imeshiriki mara moja kwenye Kombe la CAF Shirikisho na kupenya hatua ya makundi, na kwa maana hiyo Namungo anahesabika kama timu bora kwa Tanzania baada ya Simba na Yanga pale makao makuu ya CAF.

Popat amekuwa akishindwa hata kutengeneza benchi la ufundi la maana pale Azam FC, ndio maana hakuna kocha aliekuja na kudumu zaidi ya mwaka mmoja.

Popat pia amekuwa akifanya makosa makubwa kwa aina ya wachezaji anaowasajili. Alifanya hivyo kwa kusajili Ibrahim Ajibu mchezaji ambae hakuwa na lolote zaidi ya kuimbwa kwenye miziki ya singeli .

Msimu huu tena licha ya kujitahidi kwenye benchi la ufundi chini ya kocha Yusuf Dabo, lakini anarudia kosa kwa kwenda kumsajili Yanick Bangala kutoka Yanga.

Bangala ambae msimu juzi alikuwa MVP wa Ligi, lakini kiwango chake kimekuwa kikiporomoka na mwisho wa siku kuanza kusugua benchi. Bangala amesugua benchi huku akiwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Inashangaza sana Popat haoni hili. Pili Bangala amehusishwa na migomo ya chini kwa chini ndani ya Klabu ya Yanga. Amekuwa akifanya hivyo kwa kushirikiana na Shaban Djuma. Na wachezaji hao wote wameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jangwani.

Ni mtu mmoja tuu pale Chamazi haoni madhara haya hasi ndani ya uwanja na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo atakayoyaleta Bangala, nae ni Popat.

Kwa rasilimali ambazo Azam FC inazo basi ilikuwa inahitajika itawale soka la bongo na Afrika.

Inawezekana wamiliki wakina Yusuf Bakhresa na wenzio hawaoni haya madhaifu ya CEO wa timu yao. Ni bora wamuweke pembeni na kutafuta CEO mwingine. Nyota ya Azam FC ilikuwa inaanza kuchomoza lakini Popat anaanza kuizimisha kabla hata safari ya msimu ujao haijaanza.
 
Swala la Bangala kushuka kiwango na kuwa na utovu wa nidhamu limeripotiwa na mwandishi nguli wa soka nchini Edo Kumwembe.
 
Inashangaza sana Popat haoni hili. Pili Bangala amehusishwa na migomo ya chini kwa chini ndani ya klabu ya Yanga. Amekuwa akifanya hivyo kwa kushirikiana na Shaban Djuma. Na wachezaji hao wote wameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jangwani.
Migomo maana yake kuna mahitaji ya kimkataba walikuwa hawatimiziwi na kama walikuwa wanashurutisha wengine wajiunge nao ina maana halikuwa ishue binafsi bali la timu nzima ila wengine walikuwa woga kuyaongelea. Usimsambazie fitna kisa mmempoteza. Ni kweli kiwango chake kilishuka ila naamini ilikuwa ni kwa sababu hakuwa anacheza kwa juhudi kutokana na ishu za ndani zilizokuwa zinaendelea.
 
Kwaiyo ukiwa unadai njia ya mgomo ndio njia pekee ya kutumia kudai?
 
Migomo maana yake kuna mahitaji ya kimkataba walikuwa hawatimiziwi na kama walikuwa wanashurutisha wengine wajiunge nao ina maana halikuwa ishue binafsi bali la timu nzima ila wengine walikuwa woga kuyaongelea. Usimsambazie fitna kisa mmempoteza. Ni kweli kiwango chake kilishuka ila naamini ilikuwa ni kwa sababu hakuwa anacheza kwa juhudi kutokana na ishu za ndani zilizokuwa zinaendelea.
Bangala hakuwa na ishu binafsi yoyote na Yanga.
Hiyo ni dhana mfu unayotaka kuiweka hapa. Na bado ni mfanyakazi wa Yanga ndio maana imeripotiwa Azam FC wanatoa 100m za madafu kumchukua Bangala.

Kiwango kimeshuka mazima wala sio kwa sababu nyingine.
Bangala kaisha. Hafai kwenda Azam FC
 
Hizi habari za migomo ni Yanga wenyewe wanazileta ingawa unajiuliza mbona kipindi hayo yanatokea walikuwa kimya kama vile ndani ya taasisi kila kitu ni shwari, wakati huo huo walikuwa wanawasema Simba kuanzia uongozi hadi wachezaji kumbe ndani kwao huko kunanuka uvundo.

Na hii post yako kuhusu kiwango cha Bangala nitakuja kukukumbusha.
 
Kama njia zingine zimeshindikana ndiyo au mnapelekana nje ya taasisi. Halafu Bigirimana mmeshindwa kumlipa pesa zake mkaamua kumrudisha kimya kimya
Ametangazwa lini kuwa amerudishwa uyo bigirimana? Atuwezi kufanyia kazi habari za kwenye vijiwe vya kahawa, kila mtu utayemuona Avic town anapita zake utamuhusisha na yanga?
 
Hizi habari za migomo ni Yanga wenyewe wanazileta ingawa unajiuliza mbona kipindi hayo yanatokea walikuwa kimya kama vile ndani ya taasisi kila kitu ni shwari, wakati huo huo walikuwa wanawasema Simba kuanzia uongozi hadi wachezaji kumbe ndani kwao huko kunafuka moshi.
Chanzo cha habari nimeweka ni Edo kumwembe.
Sasa sijui hao Utopolo fc wanahusika vipi.
Halafu migogoro ya ndani ya timu mara nyingi humalizwa ndani ya timu.

Sio lazima itatuliwe hadharani.

Swala la kiwango cha Bangala, akishasajiliwa rasmi ni swala la muda tuu.
 
Hizi habari za migomo ni Yanga wenyewe wanazileta ingawa unajiuliza mbona kipindi hayo yanatokea walikuwa kimya kama vile ndani ya taasisi kila kitu ni shwari, wakati huo huo walikuwa wanawasema Simba kuanzia uongozi hadi wachezaji kumbe ndani kwao huko kunafuka moshi.

Na hii post yako kuhusu kiwango cha Bangala nitakuja kukukumbusha.
Nyie simbwa mangapi yanafanyika na mko kimya, Taasisi sio vikundi vya umbea umbea kupuyanga kila kitu na ndio maana sakata lenu na chama viongozi wako walifunika kombe, hivyo usitake kujifanya unawafundisha watu kazi
 
Nakwambiaje ishu ya Chama hauijui. Kuna watu wako huru kuikosoa timu yao kama Simba? Ni Yanga huko ndiyo mna mitazamo kuwa siyo uzalendo kwa timu yako kukosoa maamuzi na mienendo ya timu. Mnanung'unikia mioyoni mwenu mwisho wa siku mnakufa kwa magonjwa ya moyo.
 
Bangala hakuwa na ishu binafsi yoyote na Yanga.
Hiyo ni dhana mfu unayotaka kuiweka hapa. Na bado ni mfanyakazi wa Yanga ndio maana imeripotiwa Azam FC wanatoa 100m za madafu kumchukua Bangala.

Kiwango kimeshuka mazima wala sio kwa sababu nyingine.
Bangala kaisha. Hafai kwenda Azam FC
kama kiwango kimeshuka mnataka milioni 100 ya Nini, mnaweza kudhani mnamkomoa mchezaji kumbe mnajikomoa wenyewe kwa kumlipa mamilioni ya pesa. Inaelekea maswala ya Luc Eymael na kesi ya Morison CAS hayajawafundisha
 
Abdul Kareem Popat amekuwa CEO wa Azam FC kwa zaidi ya Miaka 7. Huyu ndio CEO ambae hana presha kabisa ya kupoteza kazi yake kutokana kutopewa presha ya mafanikio pale Chamzi Complex.

Kipindi chote cha uongozi wake Azam FC imeambulia kikombe kimoja tuu cha FA (Azam Confederation Cup) mnamo 2019. Miaka yote ya uongozi wa Popat Azam FC imeshindwa kutwaa Kombe la Ligi na kushindwa kufuzu hatua ya makundi kwenye mashindano ya CAF Champions League au Confederation.

Tukumbuke Namungo imeshiriki mara moja kwenye Kombe la CAF Shirikisho na kupenya hatua ya makundi, na kwa maana hiyo Namungo anahesabika kama timu bora kwa Tanzania baada ya Simba na Yanga pale makao makuu ya CAF.

Popat amekuwa akishindwa hata kutengeneza benchi la ufundi la maana pale Azam FC, ndio maana hakuna kocha aliekuja na kudumu zaidi ya mwaka mmoja.

Popat pia amekuwa akifanya makosa makubwa kwa aina ya wachezaji anaowasajili. Alifanya hivyo kwa kusajili Ibrahim Ajibu mchezaji ambae hakuwa na lolote zaidi ya kuimbwa kwenye miziki ya singeli .

Msimu huu tena licha ya kujitahidi kwenye benchi la ufundi chini ya kocha Yusuf Dabo, lakini anarudia kosa kwa kwenda kumsajili Yanick Bangala kutoka Yanga.

Bangala ambae msimu juzi alikuwa MVP wa Ligi, lakini kiwango chake kimekuwa kikiporomoka na mwisho wa siku kuanza kusugua benchi. Bangala amesugua benchi huku akiwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati na kiungo mkabaji.

Inashangaza sana Popat haoni hili. Pili Bangala amehusishwa na migomo ya chini kwa chini ndani ya Klabu ya Yanga. Amekuwa akifanya hivyo kwa kushirikiana na Shaban Djuma. Na wachezaji hao wote wameonyeshwa mlango wa kutokea pale Jangwani.

Ni mtu mmoja tuu pale Chamazi haoni madhara haya hasi ndani ya uwanja na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo atakayoyaleta Bangala, nae ni Popat.

Kwa rasilimali ambazo Azam FC inazo basi ilikuwa inahitajika itawale soka la bongo na Afrika.

Inawezekana wamiliki wakina Yusuf Bakhresa na wenzio hawaoni haya madhaifu ya CEO wa timu yao. Ni bora wamuweke pembeni na kutafuta CEO mwingine. Nyota ya Azam FC ilikuwa inaanza kuchomoza lakini Popat anaanza kuizimisha kabla hata safari ya msimu ujao haijaanza.
Malengo yao mengine kabisa, tofauti na unavyofikiri wewe. Hiyo ni team ya kampuni siyo kama simba na yanga.

Azzam inajiendesha kibiashara zaidi siyo kishabiki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom