Sababu ya Dube kuomba kuondoka Azam

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Klabu ya Azam imethibitisha kupokea barua ya PRİNCE DUBE akiomba kuondoka kwenye klabu hiyo. Taarifa ya klabu inasema Azam FC wamemjibu na kumwambia anaweza kuondoka ila kwa kufikiwa kwa vipengele vya mkataba, yani kama klabu nyingine au yeye mwenyewe anaweza kuilipa Azam FC pesa waliyoweka kwenye mkataba kama mchezaji anataka kuvunja mkataba au timu kumnunua “buy out clause”. Dube ana mkataba wa miaka 2 na miezi 6 kwenye mkataba wake unaomalizima 2026.

NYUMA YA PAZIA NINI KINAMUONDOA DUBE AZAM FC
Dube amekuwa akiweka shinikizo la kutaka kuondoka kwa muda mrefu tangu wakati wa Pre-season na kuna klabu ya Kariakoo imekuwa ikimhitaji kwa udi na uvumba baada ya kuondokewa na mfungaji wake mahiri aliyeenda kutafuta malisho kwingineko barani Afrika

Dube ambaye hayuko pia kwenye mahusiano mazuri na kocha mkuu Yusuf Dabo amekuwa akisumbuliwa sana na simu za Kigogo wa timu hiyo ya Dar es Salaam tangu wakiwa Pre-season na kwakuwa hayuko kwenye mahusiano mazuri na Dabo anaona njia ya kumtia adabu ni kuondoka na kujiunga Kariakoo.

Wachezaji wenzie wamewahi kumsihi asiondoke ili wapambanie ubingwa lakini majibu yake ni viongozi hawamheshimu kwakuwa wameshamzoea kakaa sana na kocha Dabo hawaelewani njia pekee ni kuondoka tu.

Hali ilivyo Azam FC watamgomea Dube msimu huu nadhani baada ya hapo uzoefu unaonyesha watamruhusu aende anakotaka pengine kwa pesa kidogo sana nje ya kile cha kwenye mkataba. Waliwahi kuondoka Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo “Ridondo” kwa mtindo kama huu au unaokaribiana, hata usajili wa Salum Abubakar Salum “Sureboy”.

Nadhani Dube na klabu inayomhitaji wanapaswa kuwa na subra kiasi tu, mabosi wa Azam FC huwa hawapendi zogo na timu za Kariakoo analotaka litakuwa ni suala la muda tu.

Ningeshangaa sana watu wakae na Jose au Fredwaaa na Prince yuko Chamazi? Lazima tu ingekuwa hivi katika hali ya kawaida LAZIMA.

Mwenye Kisu kikali atakula nyama. Lakini pia wachezaji wanapenda kucheza mashindano makubwa ya Afrika na kufika mbali, wanapenda kushinda vikombe vya ligi pia. Kwahiyo wanashawishika kirahisi kwakuwa Kariakoo wanafanikiwa.

C and P
 
Dube analeta utoto, kama unajua una mkataba na timu yako huwezi kukurupuka tu kutaka kuondoka, hizo ni bangi.

Hata kama anatakiwa na hiyo timu ya wafuga majini, awaambie viongozi wa wafuga majini waende kuongea na Azam wamalizane..

Hiki walichofanya kwa Dube ni kama wamemtuma kuvuruga mambo makusudi ili wapate mlango wa kuingilia..

Ili waanze kufanya mazungumzo na Azam, kwa kigezo mchezaji hana raha hapo alipo, kumbe wao ndio walimuagiza akose hiyo raha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
kama Azam walivyofanya kwa Feisal.
 
Itakua ni revenge ya Feisal, acha Azam nao wakomeshwe walishiriki sana kuharibu stability pale jangwani wakati team inapambana CAF
 
Samahani Mkuu, mimi nadhani hizo timu za Bongo zilizoingia kwenye hili sakata zote zina makosa tena makubwa. Maana nakumbuka hata wakati Feisal Salum anataka kuondoka Yanga ulitumika uhuni kama huu. Shida ni kwamba tunataka kuendesha mpira kama familia badala ya kufuata sheria. Naona kuna masuala ya kisasi kwenye hili sakata. Msingi ni kurudi kwenye kuheshimu mikataba haya mambo hayatajitokeza tena.
 
Yaani mtu mpaka kaandika barua na bado mnataka mseme kakurupuka??? Kwa hiyo hapo afanyeje??, fikra za baadhi ya wabongo anaeweza kuzielewa ni mtu asiejielewa kabisa

Yaani mtu kaandika barua kuijulisha klabu bado mtu anaona sio sawa, sa sijui kingine kipi huwa kinafanywa
 
Dube analeta utoto, kama unajua una mkataba na timu yako huwezi kukurupuka tu kutaka kuondoka, hizo ni bangi.

Hata kama anatakiwa na hiyo timu ya wafuga majini, awaambie viongozi wa wafuga majini waende kuongea na Azam wamalizane..

Hiki walichofanya kwa Dube ni kama wamemtuma kuvuruga mambo makusudi ili wapate mlango wa kuingilia..

Ili waanze kufanya mazungumzo na Azam, kwa kigezo mchezaji hana raha hapo alipo, kumbe wao ndio walimuagiza akose hiyo raha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mwaka Jana kuna ujinga kama huu ulikuwa unautetea au siyo wewe?
 
Dube analeta utoto, kama unajua una mkataba na timu yako huwezi kukurupuka tu kutaka kuondoka, hizo ni bangi.

Hata kama anatakiwa na hiyo timu ya wafuga majini, awaambie viongozi wa wafuga majini waende kuongea na Azam wamalizane..

Hiki walichofanya kwa Dube ni kama wamemtuma kuvuruga mambo makusudi ili wapate mlango wa kuingilia..

Ili waanze kufanya mazungumzo na Azam, kwa kigezo mchezaji hana raha hapo alipo, kumbe wao ndio walimuagiza akose hiyo raha.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kuwa tu mpole comrade. Huu mchezo hautaki hasira. What goes around, comes around.
 
Itakua ni revenge ya Feisal, acha Azam nao wakomeshwe walishiriki sana kuharibu stability pale jangwani wakati team inapambana CAF
Majini FC wameshawekewa dau, kama wanaamini kwenye revenge waambie waende kwa Samia kuomba msaada.
IMG_20240305_124834.jpg

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Yaani mtu mpaka kaandika barua na bado mnataka mseme kakurupuka??? Kwa hiyo hapo afanyeje??, fikra za baadhi ya wabongo anaeweza kuzielewa ni mtu asiejielewa kabisa

Yaani mtu kaandika barua kuijulisha klabu bado mtu anaona sio sawa, sa sijui kingine kipi huwa kinafanywa
Mchezaji kaomba kuvunja mkataba ,Azam wamempa dau avunje mkataba wake anatokea mhehe sijui msambaa anapinga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom