Abdallah Ulega amewahimiza Mawaziri EAC Uwekezaji Mifugo, Uvuvi & Kilimo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

WAZIRI MHE. ABDALLAH ULEGA AHIMIZA UWEKEZAJI MIFUGO, UVUVI & KILIMO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahimiza Mawaziri Wenzake wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaosimamia Kilimo, Chakula, Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji kushirikiana na Sekta Binafsi kuongeza uwekezaji katika sekta za Mifugo, Uvuvi na Kilimo ili kuimarisha Usalama wa Chakula na kukuza uchumi wa Nchi hizo.

Waziri Ulega alitoa rai hiyo wakati akitoa neno la utangulizi katika Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Kilimo, Chakula, Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji uliofanyika jijini Dar es Salaam Mei 19, 2023.

Aliongeza kwa kusema kuwa, kwa upande wa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kufanya uwekezaji kwenye sekta za mifugo na uvuvi na kilimo ziweze kuongeza uzalishaji ili ziwe na mchango mkubwa zaidi katika pato la Taifa.

Mkutano huo ulikutanisha Mawaziri 7 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani Kusini, Jamhuri ya Kongo (DRC) na Burundi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.07.jpeg
    29.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.08.jpeg
    34.8 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.08(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.08(1).jpeg
    42.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.09.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-20 at 11.55.09.jpeg
    41.1 KB · Views: 6
Back
Top Bottom