Abdalah Kibadeni azushiwa kifo!

Abdalah Kibadeni azushiwa kifo!

Status
Not open for further replies.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,024
Reaction score
59,684
Kocha maarufu nchini, Abdallah ‘King' Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.

Taarifa ziliripotiwa na mitandao zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara.

"Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.

"Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.

"Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi," alisema Kibadeni na kuongeza.

"Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu"
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Abdalla ‘King' Kibaden amefariki dunia leo.

Kibaden ambaye alichaguliwa kuwa kocha wa Simba mwaka 2013, pia aliwahi kuwa kocha wa Kagera Sugar na Ashanti United.

Baada ya Sunderland kufungwa 5-0 na Yanga 1968 iliamua kubadilisha kikosi chake kwa kuwaondoa wachezaji wakongwe na kusajili wachezaji chipukizi.

Miongoni mwa chipukizi hao walikuwa Abdallah Kibaden, Willy Mwaijibe, Omary Gumbo,nk. mwaka huo Abdallah Kibaden alichaguliwa katika timu ya taifa ya Tanzania na vile vile alikuwa mwanasoka bora wa Tanzania.

Mchezaji huyo ambaye ana elimu ya ufundi magari Daraja la Pili (Motor Vehicle Mechanics Grade II) amewahi kuajiriwa katika kampuni mbalimbali, ajira ambazo kupatikana kwake kulichangiwa na kipaji chake cha soka.

Wasifu wa Kibaden

Oktoba 11, 1949: Alizaliwa Kiburugwa, Mbagala jijini Dar es Salaam.

1959: Alitungiwa jina ‘Kibaden' na watoto wenzake kwa kucheza soka ya nguvu akiwa mdogo na mfupi. Jina lake halisi ni Abdallah Athuman Seif. Kibaden maana yake ni kitu cha baadae.

1969: Alijiunga na Simba FC, iliyokuwa ikiitwa Sunderland.

2011: Alikwenda Hijja.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

CHANZO:
attachment.php
 
R.I.P Kibaden

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mkuu mbona heading umeuliza kama vile huna uhahakika! Is it real story King amefariki? Lol RIP kibadeni
 
Ngoja nitafute vyanzo vingine, may be Michuzi blog has details, sio ww unauliza swali alafu unalijibu
 
Mkuu mbona heading umeuliza kama vile huna uhahakika! Is it real story King amefariki? Lol RIP kibadeni

Sina uhakika ila nimeona kuwa ndio trending news kwenye mitandao now.
Nimeitoa kwa Salim Kikeke wa bbc swahili
 
Ngoja nitafute vyanzo vingine, may be Michuzi blog has details, sio ww unauliza swali alafu unalijibu

Nimeiotoa hii taarifa bbc swahili kwa salim kikeke. Nisaidie kufuta hicho kiulizo
 
I.W.R.Allah awajaze familia ya al marhoum mioyo ya subira na uvumilivu...mtihani huu ni wetu sote...mwenzetu ametangulia tu....
 
Mkuu Saint Ivuga
Nimeongea na Kibadeni masaa machache yaliyopita na alikua anajiandaa kwenda mazoezini na timu yake ya mtaani na akaniambia kazushiwa kifo but yeye Salama salimini.
So ni habari ya uzushi mkuu na amesema ataongea na baadhi ya vyombo vya habari leo.


s
 
Last edited by a moderator:
Nimesikia taarifa za kifo za kocha wa Zamani wa Simba Abdallah King Kibaden Mputa..Nimefanya jitahada za kutafuta Ukweli kwa Kumpigia Simu yake ya Mkononi ''Jambo la kwanza akaniambia Mimi Mzima wa Afya nipo yupo Nyumbani kwangu Sinza poleni kwa kusumbuka sijui kwanini watu wanazusha hayo''
 
Hizo taarifa za kifo wewe umezisikia wapi?,hivi kwanini watu hupenda kutangaza taarifa wasizo na uhakika nazo?..pole Sana king Mputa...
 
imekuwa je tena King Kibadeni???
Hama sinza sasa labda wamekuchoka long time, anyway pole sana kama vp fanya press conference kesho.
 
Nimesikia taarifa za kifo za kocha wa Zamani wa Simba Abdallah King Kibaden Mputa..Nimefanya jitahada za kutafuta Ukweli kwa Kumpigia Simu yake ya Mkononi ''Jambo la kwanza akaniambia Mimi Mzima wa Afya nipo yupo Nyumbani kwangu Sinza poleni kwa kusumbuka sijui kwanini watu wanazusha hayo''

Si Dalili Njema Na Ukweli Ni Kwamba Jamaa Ni MENDE Sana Na Ana Tatizo La Kupelekwa Kwa Professor Patrick Wa Johns Hopkins.
 
Kuna habari kuwa aliekuwa kocha wa Simba na Ashanti kwa nyakati tofauti amefariki dunia. Wenye habari kwa undani tunaomba mtujuze tafadhali
 
Kwani alikuwa mgonjwa?
 
Sisi tunaishi chanika mbona izo abari atuna labda kama alipelekwa India akafia uko
 
Hata Ezekiel Kimwaga kasema kaongea na Kibaden na ni mzma .
"Tanzania nchi ya uzushi uzushi"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom