SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,136
- 7,904
Mara kadhaa niliwahi kuahidi kuleta uzi unaohusiana na mada hii, leo nimetulia kidogo nimeukumbuka. Ngoja nitiririke.
Kuna hii kasumba iliyojengeka kwenye mpira kudhani kuwa mchezaji yoyote hasa akitokea kupata mafanikio fulani kama mchezaji anaweza kuja kuwa kocha mzuri pale atakapostaafu. Mimi binafsi naamini IQ ya mchezaji ndiyo itakayoamua kama mchezaji atakuja kuwa kocha mzuri. Mchezaji anaweza kuwa alikuwa anafunga sanaa enzi za uchezaji wake kama kina Ole Gunar Solskjaer na bado asiweze kuja kuwa kocha mzuri. Ukocha siyo kama ukuu wa wilaya kwamba unaweza mwenyewe kuficha au mamlaka zinaweza kukubeba na kuficha madhaifu yako siku zikasonga.
Huko nje mifano ipo mingi sana ya wachezaji ambao enzi za uchezaji wao walikuwa mahiri sana ila walipoenda kwenye ukocha ilikuwa ni majanga matupu. Alan Shearer ambaye bado anashikilia rekodi za ufungaji bora huko Uingereza ila alipewa timu aifundishe ikashuka daraja.
Sir Bobby Charlton anayeaminika ni mchezaji bora wa muda wote kutokea pale Uingereza, huyu naye alipewa timu akaishusha daraja. Thiery Henry ana mafaniko mengi sana ya binafsi kama mchezaji na alizoipatia klabu zake na timu yake ya taifa na baada ya kustaafu alipewa mikoba ya ukocha katika timu ya AS Monaco, ila baada ya miezi 3 akafukuzwa baada ya kuitumikia kwa mechi 20 tu huku 11 akiwa amepoteza.
Kuna Tony Adams, mmoja wa wachezaji wanaoheshimika mno huko Uingereza hadi wamemjengea sanamu yake pale nje ya uwanja wa Arsenal wa Emirates ambayo aliitumikia kwa miaka 22 kama mchezaji. Huyu baada ya kustaafu, timu mbili alizofundisha amezishusha daraja.
Kuna Paul Gascoigne "Gaza" na Stoichkov. Kuna Paul Scholes na mwenzake Gary Neville, wote wawili zao la Alex Ferguson pale Man United lakini wote walishindwa vibaya sana katika ukocha. Kuna Lothar Matthaus, legend wa Ujerumani ambaye timu yake ya Celta Vigo ilishuka daraja ikiwa katika mikono yake ya ukocha. Hapo sijamtaja Diego Maradona, legend mwingine wa soka ila zama zake kama kocha zilikuwa ni za visanga tu.
Tanzania tumeshuhudia wachezaji kadhaa wa zamani waliowahi kuchezea timu kubwa mfano za Simba na Yanga ambao walikuja kuwa makocha. Mifano inayonijia haraka ni Fred Felix "Minziro" huyu amefundisha kwa muda mrefu sana ila hana rekodi yoyote ya kujivunia. Kuna Mohamed Hussein "Mmachinga" mchezaji ambaye kama liivyo kwa Alan Shearer bado anashikilia rekodi katika ufungaji bora katika ligi kuu ila mpaka leo hana mafanikio yoyote katika ukocha. Sina uhakika kama Mmachinga ameshawahi kufundisha ligi kuu ila mara ya mwisho nimemuona anafundisha kwenye bonanza kwenye kombe ya Ramadhani.
Kuna Jamhuri Kihwelo, naye baada ya kufundisha kwa muda mrefu hana lolote la kujivunia katika ukocha pamoja na kwamba enzi zake za uchezaji alipewa sifa kedekede. Kuna Joseph Lazaro na Juma Mgunda ambao naona kama bado wanajitafuta. Selemani Matola amekuwa chini ya miamvuli ya makocha wengine, hatujamuona akiongoza timu kama kocha mkuu kwa hiyo bado hatuwezi kumuhukumu.
Wachezaji pekee wa ndani ambao naweza kusema waliweza kupata mafanikio kama makocha ni Abdallah Kibadeni na labda Charles Boniface "Mkwasa". Huyu Mkwasa namtaja ila inabidi nirudi kuhakiki rekodi zake maana najua amefundisha sana Yanga na timu ya taifa ila sina uhakika kama kuna mafanikio yoyote yaliyopatikana chini ya mikono yake.
Ili mchezaji aweze kuwa kocha mzuri inabidi awe na IQ kubwa ya kimpira yeye kama mchezaji kwanza. Kupima IQ ya kimpira inabidi uwe na jicho la kuangalia mchezaji anavyocheza uwanjani. Naangalia uwezo wa kucheza position zaidi ya moja uwanjani, uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na ya haraka akiwa na mpira, anavyojiposition anapokuwa hana mpira, uwezo wa kuusoma mchezo na kuiendesha timu uwanjani.
Nikitumia sampo zilizoko katika vikosi vya Simba na Yanga msimu huu, wachezaji ambao kwa haraka haraka wananijia kichwani kuwa kwa mtazamo wangu wanaweza kuwa sifa hizo na hivyo wanaweza kuja kuwa makocha wazuri ni pamoja na Djigui Diarra, Khalid Aucho, Che Malone, Moses Phiri, Max Nzengeli, Aziz Ki, Dickson Job, Fabrice Ngoma, Luis Miquisonne, Clatous Chama na ziada naweza kuwaongeza Shomari Kapombe na Feisal Salum (Azam). Kwa sababu ligi ya NBC sasa hivi inajumuisha wachezaji kutoka nje, nimeona mifano yangu iwajumuishe pia.
Uzi huu umejikita zaidi kuangalia wachezaji wakubwa ambao walifeli kuwa makocha. Kwa wachezaji wa nje kuna ambao walikuja kufanikiwa sana kama makocha mfano Diego Simeone, Zidane, Cruyff, Guardiola, Ancelotti, del Bosque, Antonio Conte, Beckenbauer na Mancini.
Kwa Tanzania, wachezaji wa zamani ambao kwa sifa ambazo nimesikia walikuwa nazo kwa mtazamo wangu naona kama wangeweza kuwa makocha wazuri ni Edibily Lunyamila, Salvatory Edward, Hussein Marsha, Kenny Mkapa, Hamis Gaga "Gagarino", Malota Soma, Method Mogella, Yusuph Macho na Athumani China. Sina uhakika katika hawa kuna ambaye alishajaribu ukocha ila inawezekana nao wangeishia kuwa na mafanikio kama ya Jaluo na Minziro.