A Story kutoka Zero mpaka Hero, Uzi wa mirejesho (Msoto, Malengo, Ndoto)

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,635
4,997
A day am inspired kuandika tu.

Huu uzi lengo lake kuonesha safari ya maisha yetu halisia kiuchumi kutoka step moja hadi step nyingine, unachofanya ni kuonesha/kueleza hali hali ya kiuchumi uliyonayo sasa iwe ngumu au ya msoto na kueleza baadhi ya malengo yako unayotarajia kutimiza kulingana na muda fulani uliyojiwekea.

Ningependa uzi huu ukawe wa endelevu, kwa maana uliweka hali yako kiuchumi ya sasa unaweka lengo/malengo uliyojiwekea kuyatimiza kwa muda fulani then baadae hata ikipita miezi/Mwaka/miaka ukatimiza lengo unakuja kwenye uzi una-Quote ile comment yako na kuelezea ulivyotimiza lengo | pia sio lazima kueleza malengo yako unaweza eleza hali yako ya sasa kiuchumi ukitimiza lengo Fulani ukaja kueleza.

Hii itakuwa nzuri utapoweka update ya kutumiza lengo fulani anayesoma wakati huo atatafuta reply yako ya nyuma aone ulivyotoka ZERO mpaka HERO.

Vizuri wale member walio kwenye Scratch kama Umomi nk wakawa hii ndio uwanja wao.

PERSONAL/BINAFSI
_Kwasasa uchumi wangu hauko stable, ndio nimemaliza Chuo nipo naishi nyumbani kwa wazazi, Asset ninazomiliki kamradi kadogo tunamiliki watu watatu kwa siku napata 2000 Tzs. Mbali na biashara hiyo kingine nacho miliki hii simu Tecno N2 iliyoharibika system charger.

Nina malengo kadhaa ya muda mrefu na muda mfupi na Mikakati kadhaa ya kufikia malengo haya kwa muda uliopangwa.

Nila malengo makubwa sita (6), ambayo ni kumiliki Biashara hizi kabla sijafikisha miaka 40

1)Carwash za kisasa (nne 4).

2)Biashara ya usafishaji (I.e Costa 4).

3)Large Scale Poultry Farm.

4)Mastering Online Business (FX, Drop shipping, Freelauncer).

5)Kufungua kituo cha mafuta (Petrol Station).

6)Starting Fintech Company (Startup).

Mbali na malengo haya yaliyo katika mfumo wa Biashara kabla kutumiza miaka 35 ninataka nimiliki kihasi cha 2 Billion Cash zangu mwenyewe.

Malengo yote nimejaribu kuyapangilia kulingana na uzito wake kutoka 1 hadi 6 ili kuwa rahisi kutekelezeka simply siwezi leo hii nikasema nianze na Petrol Station nitakuwa siko serious, lazima nianze na Carwash, kupitia Carwash utanipa Mtaji wa Usafishaji nk nk.

Sasahivi nipo katika Mikakati ya kutumiza lengo la kwanza kati ya sita (6), kufungua Carwash ya kisasa ndani ya DSM Mungu atapojaalia kabla 2021kuisha nimepanga niwe nishafanikisha.

Malengo madogo na makubwa kipindi kufupi, nitaanza kureta update soon.

1)Lengo la muda mfupi kabla 2020 kuisha kuhama home.

2)Kabla 2021 kuisha kufungua Carwash kubwa ya kwanza Dar Es Salam.

Hapa nitakuwa nareta mrejesho wa malengo hayo sita (6) mpaka kufikia mwaka 2035 endapo hakuta tokea tatizo llolote, bila kusahau ka kumiliki 2 Billion Cash kabla 35.

Nataka nimuoneshe dogo fulani aliye darasa la tano (5) sasahivi ikaja kuanza kutumia JF kipindindi hiko 2035 aone kumbe mambo yanawezekana ukipanga malengo.

Huu uzi utakuwa kama deni litalonichapa bakora kilasiku nitahakikisha sitawaangusha.
 
Ok,
Upo kwenye stage nzuri kwanza ni kuutoa umaskini kichwani. Je, una uhakika ndani hichi kipindi utakuwa ushapata mtaji kutimiza lengo lako la awali?

Kwa sasa unaingiza 2000 kwa siku je, utahitaji kusave kwa muda gani kufikia lengo la kuwa na carwash ya kisasa.
Ukiweza anza hata na carwash local ya mtaji kidogo.

Safari moja huzaa nyingine. Ukiweza usiondoke home, ili kupunguza gharama za maisha. Maadamu ushajua cha kufanya unajua pesa yako uipeleke wapi.
 
Amka dogo, usije ukakojoa kitandani-joke
Kila mtu anaota kama wewe unavyoota. Tatizo ni jinsi ya kufikia hizo ndoto.
Tafuta vijana wenzio muungane. kama watano hivi. Wasio wavivu. anza hata kwa kuosha magari ,baada ya muda mtakuwa na car wash yenu
Au nendeni hapo dumila limeni nyanya
 
Amka dogo, usije ukakojoa kitandani-joke
Kila mtu anaota kama wewe unavyoota. Tatizo ni jinsi ya kufikia hizo ndoto.
Tafuta vijana wenzio muungane. kama watano hivi. Wasio wavivu. anza hata kwa kuosha magari ,baada ya muda mtakuwa na car wash yenu
Au nendeni hapo dumila limeni nyanya
Aiseeh
 
Lakini October man huwa unaandika vibaya sana.

Halisia alisia asset assert....... Sijamaliza kusoma bado.

Nini tatizo?
Mkuu usimlaumu sana elimu yetu ndio tatizo, unajiuliza mtu ameanza shule ya msingi, akaingia secondary, high school mpaka chuo lakini bado kuandika na kusoma kwake ni changamoto.

October man malengo yako ni mazuri sana ila kumbuka changamoto pia ni nyingi zisikukatishe tamaa, kikubwa mimi nataka nijifunze kupitia shuhuda mbalimbali nitakazo zisoma katika huu uzi.
 
Mkuu usimlaumu sana elimu yetu ndio tatizo, unajiuliza mtu ameanza shule ya msingi, akaingia secondary, high school mpaka chuo lakini bado kuandika na kusoma kwake ni changamoto.
October man malengo yako ni mazuri sana ila kumbuka changamoto pia ni nyingi zisikukatishe tamaa, kikubwa mimi nataka nijifunze kupitia shuhuda mbalimbali nitakazo zisoma katika huu uzi.
Sijalauumu.
Nimeuliza.
Kuhusu elimu nakataa hakuna mwalimu anayefundisha na kuandika vibaya.
Nakataaa.
Tusisingizie elimu.
 
Mkuu October man mimi nikupe tu ushauri

Kama unataka kufikia malengo yako vizuri anza kidogo kidogo kwa akili kubwa sana.

Unajua ukiwa hauna kitu usiogope kutake risk huna chakupoteza. Wanaotakiwa kucalculate risk ni wenye nacho/matajiri ambao wanalinda ukwasi wao usipotee

Ogopa sana wale watu unaotaka kufanya jambo au biashara wanakwambia hii biashara hailipi nakwambia ogopa sana hao ndio chanzo cha umasikini wa watanzania wengi

Watanzania wengi ni wafata mkumbo mtu hajawahi fanya biashara yoyote lakini kwa story za vijiweni ukiwasikiliza nikama wanajua kila biashara

Jaribu kuchunguza biashara nyingi zinazopingwa na wabongo nchi za njee ndio wengi wanatajirikia. Bongo hapa utasikia usilime matikiti, usilime nyanya, usilime mpunga, usifanye biashara ya nafaka serikali imeharibu soko, kama unataka presha fuga kuku usifuge sungura, kware. Biashara ya miamala mpesa usifanye kuna chuma ulete, usiweke pesa zako fixed acc faida ni ndogo, biashara ya mbao imejaa mikopo, madini kuna utapeli utafirisika, etc

Mimi ni kijana tu kama wewe mwaka jana ndio nilimaliza masomo yangu baada ya kumaliza nilikomaa kila njia nisimame nilifanya kila biashara ambayo niliona inaweza kunifikisha mahali, kwa kweli nimeanguka mara nyingi sana nimepoteza mitaji mingi sana lakini sikomi bado nasimama nasonga mbele

Kiufupi baada ya kufanya biashara ndogo ndogo nilifanikiwa kufungua store ya nafaka (mpunga,maharage, njegere etc) maeneo ya kawe ,Nimewekeza kwenye ufugaji kuku, huu msimu nimelima maharage ekari 5 pia mahindi ekari 5, japo sijalima kitaalam nimeanza hivyo hivyo. Mpunga kahama nimenunua msimu huu na kuhifadhi kwa mara ya kwanza. Nafanya forex japo sio kivilee,nimewekeza pia kwenye matofali ya kuchoma nyumbani ,betting nilikuwa nafanya sana now nimeacha.

Malengo yangu ya 2021 nikununua ekari kadhaa njombe nilime kilimo cha parachichi maana nilikiwa naangalia youtube nikaona jamaa amekusanya million zaidi ya 500 kwa kuuza hilo zao tena kwa kampuni moja na hakuweka kukidhi supply waliokuwa wanataka

Mwaka jana nilikuwa nalala sipati usingizi .usiku mzima nawaza tu kuhusu ajira. Lakini now nimejikuta mm ndio nimeajiri watu mfano pesa ya kupakia, kushusha mzigo, shughuli za shamba kulipa vibarua, kuhudumia mifugo kusambaza mchele mimi ndio nahusika kama boss.

Nilichojifunza matajiri wataendelea kutajirika sana kwa sababu tanzania kuna masikini wengi cheap labour wengi maana uchumi wetu unahali mbaya pesa haionekani

Just imagine vibarua wamefyatua matofali elfu kumi yale ya kuchoma kwa shillingi 250000 tu.

Kiufupi nikwambie tu anza na kitu chochote usikae na hayo mawazo kichwani hayawezi kukusaidia manufaa yake yataanza kuonekana ukishaanza yafanyia kazi

Nakutakia mapambano mema
 
Mkuu October man mimi nikupe tu ushauri

Kama unataka kufikia malengo yako vizuri anza kidogo kidogo kwa akili kubwa sana.

Unajua ukiwa hauna kitu usiogope kutake risk huna chakupoteza. Wanaotakiwa kucalculate risk ni wenye nacho/matajiri ambao wanalinda ukwasi wao usipotee

Ogopa sana wale watu unaotaka kufanya jambo au biashara wanakwambia hii biashara hailipi nakwambia ogopa sana hao ndio chanzo cha umasikini wa watanzania wengi...
Nimekumanya Boss.
 
Back
Top Bottom