A shoulder to cry on

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,729
386
Ni mdada mwenye umri wa miaka 32, hakubahatika kuolewa wala hana mtoto lakini amekuwa na jamaa aliyeishi naye kwa miaka takribani minne, kifupi ni mfanya kazi mwenzangu na rafiki mzuri pia kwani tunashea ofisi moja.
Kuna siku kama miezi sita iliyopita hakuja ofisini kwa siku kama 3 mfululizo, nikampigia akasema anaumwa, nikampa pole na kuwa namcheki mara kwa mara anaendeleaje.,aliporudi ofisini akanisimulia kuwa yule "shemeji" aliyekuwa akiishi nae wameachana kisa ni kuwa alimfumania akila uroda na shoga yake.
Hali hiyo ilimuathiri sana kisaikolojia na kuathiri utendaji kazi wake.,kazini wote tulimtegemea kwani ni "jembe" haswa na ni kama "google" ya ofisi kwani hakuna asichojua.,nikawa namfariji kwa maneno, na sometimes kumtoa outing kidogo ili kumtoa ile hali ya upweke.,urafiki ukawa urafiki na tukazidi kuelewana kwani kwa kiasi kikubwa niliweza japo kumpunguzia upweke.,sasa amekuja na idea ya kutaka kupeleka urafiki into the next stage "tuwe wapenzi", mimi nipo committed kwa mtu mwingine (anafahamu hilo) ambaye nimeshalipa hadi mahari bahati mbaya/nzuri anamalizia masomo yake nje ya nchi ndio tuje tufunge ndoa.,huyu wa ofisini amekuwa akinililia sana kwa kusema kwa kundelea kumkataa namrudisha kwenye matatizo ya awali (na kweli nimeanza ku-note kuzorota kwa ufanisi wake) na kibaya zaidi anatishia kujiua.,namhurumia kwa kweli nashindwa kuelewa nimsaidieje.

Wadau naombeni mchango wa mawazo..Nawasilisha
 
lolyz

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
338
197
M -bongotz - ukianzisha mahusiano ya upenzi ni kwa kumhurumia na si kumpenda sababu she was and she is your friend just that,mweleze hawezi kuwa ametoka kwenye mahusiano miezi 6 iliyopita ndio ajigundue kuwa anakupenda wakati hiyo 4yrs wote mlikuwa mnaonana.hapo nadhani anataka kufanya replacement sababu amekuona unajali na anataka au anafikiri unampenda kivingine wakati ulikuwepo km rafiki tuu..muulize anafikiri ww kuwa shoulder ni makosa ambayo yamemfanya yy kufall?....mweleze kuwa hutaki kuja kumuumiza mkeo mtarajiwa kama yy alivyofanyiwa na x wake unless kama una feelings kwake ambazo hujaziweka wazi.
 
feis buku

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
2,357
673
kuokoa ufanisi wake wa kazi ndo unataka kumuhurumia ili... mbona njyie viumbe hamueleweki??? ebu kua mwaminifu kwa mchumba ako! uyo wa ofisin si anajua uko na mtu na anajua maumivu ya kutendwa iweje atake ww umsaliti mpenzio!!!
 
sirmudy

JF-Expert Member
May 12, 2010
387
119
Ni mdada mwenye umri wa miaka 32, hakubahatika kuolewa wala hana mtoto lakini amekuwa na jamaa aliyeishi naye kwa miaka takribani minne, kifupi ni mfanya kazi mwenzangu na rafiki mzuri pia kwani tunashea ofisi moja.
Kuna siku kama miezi sita iliyopita hakuja ofisini kwa siku kama 3 mfululizo, nikampigia akasema anaumwa, nikampa pole na kuwa namcheki mara kwa mara anaendeleaje.,aliporudi ofisini akanisimulia kuwa yule "shemeji" aliyekuwa akiishi nae wameachana kisa ni kuwa alimfumania akila uroda na shoga yake.
Hali hiyo ilimuathiri sana kisaikolojia na kuathiri utendaji kazi wake.,kazini wote tulimtegemea kwani ni "jembe" haswa na ni kama "google" ya ofisi kwani hakuna asichojua.,nikawa namfariji kwa maneno, na sometimes kumtoa outing kidogo ili kumtoa ile hali ya upweke.,urafiki ukawa urafiki na tukazidi kuelewana kwani kwa kiasi kikubwa niliweza japo kumpunguzia upweke.,sasa amekuja na idea ya kutaka kupeleka urafiki into the next stage "tuwe wapenzi", mimi nipo committed kwa mtu mwingine (anafahamu hilo) ambaye nimeshalipa hadi mahari bahati mbaya/nzuri anamalizia masomo yake nje ya nchi ndio tuje tufunge ndoa.,huyu wa ofisini amekuwa akinililia sana kwa kusema kwa kundelea kumkataa namrudisha kwenye matatizo ya awali (na kweli nimeanza ku-note kuzorota kwa ufanisi wake) na kibaya zaidi anatishia kujiua.,namhurumia kwa kweli nashindwa kuelewa nimsaidieje.

Wadau naombeni mchango wa mawazo..Nawasilishakwa hali hii......, kweli kazi ipo...!

Endelea kumliwaza uendeleze ufanisi kazini ili output isishuke....!
 
fabinyo

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,828
1,662
kaka hapo naona unataka kulikoroga,huwezi anza mapenzi kwa kumuonea huruma huyo dada!!!simama imara,mwambie HAIWEZEKANI kuwa wapenzi zaidi ya hivyo mlivyo,ukifanya makosa utajuta bila sha maisha yako yote!Kwa sasa punguza ukaribu nae na nakuhakikishia kujiua hawezi,kama ameshindwa kujiua baada ya kumfumania mtu alikaa nae kinyumba miaka minne,tena nashoga yake iweje aweze kwako?
 
hayaka

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
474
100
mtu mzima hatishiwi nyau! anatishia kujiuwa, mbona hakujiuwa alipomfunia laazizi wake wa mwanzo?? mpe ukweli wake. sitisha ukaribu naye.
 
daughter

JF-Expert Member
Jun 22, 2009
1,277
738
Kama ambavyo yeye aliumwizwa kwa usaliti ndivyo ambavyo mchumba wako ataumia kama utaendelea 'kumhurumia' huyo dada. Usifanye ilo kosa tafadhali.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,218
91,810
ha haaaa eti anatishia kujiua....lol

subiri ufukuzwe kazi,uone kama atajiua lol
 
Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,237
13,376
sumu hawezi kunywa angekunywa toka mwanzo ............kuhusu ufanisi wa kazi wewe ndio umemwajiri atapambana na mwajiri wake..........anajua unamchumba tayari....... yeye anataka kulipiza kisasi kwa wengine........huruma yako isipitilize kaka utaharibikiwa mapema........mweleze ukweli na achana nae umempa support kubwa kusahau ya nyuma inatosha.........achana nae mapema kabla huyaanza kushawishika ukaja hapa na hadithi ya shetani alinipitia
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Asikublakimeli kwa kujiua kama kujiua si angejiua tangu mwanzo asikupe presha huyo kakangu wanawake wana mbinu nyingi usha play part yako kam rafiki otherwisely na wewe unampenda hebu akupishe huko
 
arabianfalcon

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,291
583
Pole sana kwa wakati mgumu ulokua nao,lakini jibu lake unalo wewe mwenyewe,huyo dada kama kweli anajua kuhusu ww kua una mchumba na bado anakutaka unadhani aanakujali huyo au anakutakia mema baina ya ww na mchumba wako? asikutilie kitumbua chako mchanga mwambie msaada wako umeshatoa na sio msaada wakumvua nguo asijishaue bure,wako tele wasokua na wenyewe ww unamwenyewe.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,182
14,319
Sumu huwa haipimwi kwa kuonja
Uwe na msimamo mkuu kuwa u have someone na ambaye mko tayari kufunga ndoa na kuanza maisha pamoja
Mbona unataka kuvunja uaminifu wako just kwa mtu ambaye anakuomba mapenzi kw aajili ya kumhurumia
Miaka yote hajakuona wewe anakuja kukuona leo tena baada ya kuachwa ndo anakuona wa maana
Uwe na msimamo na mwambie iishie hapo hapo kwa urafiki na sio next stage
hayo mapenzi ya kuanza kwa kuwa unamhurumia asipoteze ufanisi wake wa kazi sio mapenzi hayo
 
samito

JF-Expert Member
May 16, 2011
631
175
acha kumwendekeza huyo mshenzi. namwita mshenzi kwasababu alikubalije kuishi na mtu kwa kipindi chote hicho na wakati hawajaoana???? hukupaswa hata kumliwaza, she deserve that kwa muda ili ajifunze.
 
Shantel

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
2,020
1,107
Wanawake bwana usikute kule alitendwa kwa kulazimishia hivohivo sasa hapo kwa ko anataka kuingia hivohivo pasi na pnzi, mwambie ukweli kama haumfeel kabisa, usimwonee haya utaona kama umemuumiza ila kwa long terms utakuwa umemsaidia sana ,atakuja gundua badae, kama umempenda kidhati huna jinsi
 
nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Ndio maana nilishasemaga hakuna urafiki kati ya mtoto wa kiume na wa kike. Unless huyo mtoto wa kike awe tomboy. Lakini hawa wa kawaida kama mie mtaishia kitandani tu.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,218
91,810
Ndio maana nilishasemaga hakuna urafiki kati ya mtoto wa kiume na wa kike. Unless huyo mtoto wa kike awe tomboy. Lakini hawa wa kawaida kama mie mtaishia kitandani tu.

wewe huna guys ambao ni just friends???
ambao unaweza kwenda nao lunch hivi ,wakati wa lunch break oficin????/
 
nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,313
8,343
Sikumbuki kwenda lunch na mwanaume ambaye sina uhusiano nae aisee. Sembuse kuomba shoulder to cry on. Mh; Masholder ya wanawake wenzangu yameisha?

It does not mean kuwa si interact na guys ila ni strictly business; ofisini si dinner wala lunch. Mi mke wa mtu bwana.

wewe huna guys ambao ni just friends???
ambao unaweza kwenda nao lunch hivi ,wakati wa lunch break oficin????/
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,218
91,810
Sikumbuki kwenda lunch na mwanaume ambaye sina uhusiano nae aisee. Sembuse kuomba shoulder to cry on. Mh; Masholder ya wanawake wenzangu yameisha?

mhhh thats strange...wanawake wengine hawana ma best friend wa kike....
so inatokea their best friends ni wanaume....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom