A failed assassination plot against Dr. Ulimboka...

Inawezekana kabisa maadui wa Dr. Uli wakajificha katika mgongo wa serikali ambaye pia ni adui wa madaktari wote. Lakini nikuulize swali moja, mkikosana na jirani yako na akakuambua kuwa 'leo utanitambua'. Jioni ukamwona katika kituo cha mafuta akinunua petroli wakati hana gari wala pikipiki na usiku huo nyumba yako ikaungua kwa moto. Neno liwalo na liwe likitumiwa na kiongozi mkubwa lina tafsiri nyingi mno ambazo zote zinakubalika na anaelewa kabisa uamuzi wowote utakaochukuliwa utakuwa na madhara aidha kwa serikali au kwa wananchi
 
Hatupo pamoja nawe kwa hili. Wala sikubaliani nawe.
 
Ni sahihi. Nafikiri tusi-focus sehemu moja. Tupepese macho yetu kote kote. Bahati mbaya tu ni kuwa hatuna uhakika na uchunguzi utakaofanywa na hao watakaofanya
 
Hatupo pamoja nawe kwa hili. Wala sikubaliani nawe.

Sawa! Lakini chochote kati ya haya chaweza kuwa. Sisimamii mguu moja kwa sababu ya chuki yangu dhidi ya serikali. Naweza kumpoteza muhusika halisi wa tukio kwa sababu ya ushabiki wa kisiasa.
 

Maneno yako ni sawa mkuu. Ndiyo maana nikasema jambo litizamwe kwa pande zote mbili ili kuziba uwezekano wa mianya inayoweza kumfanya muhusika mkuu akasevu kisanga. Nautizama upande wa pili pia kwa sababu njama yenyewe na utekelezaje wake haijakaa ki serikali serikali, imefanywa ki huni huni hivi.
 
Nonsense of the first order!!!!!!!!!!!!!!!!!

Of course..ikumbukwe kuwa kama "polisi njaa" wangetumika then kusingekuwa na coordination na uongozi wa polisi...Mfano alipopolekwa kituo cha polisi bunju Dr Uli hakupewa msaada wowote na kituo ilhali wakijua alikuwa amedhurika vibaya - hii inamaanisha tayari walikuwa na mwongozo kutoka juu kuwa wasihangaike kumpeleka hospitali. Pili, ukiangalia uongozi wa juu wa polisi na wizara ya mambo ya ndani inatetea huku wakijichanganya - hii inamaanisha uhusika wao hauna mashaka hata kidogo. Tatu, Polisi aliyepewa kibano pale Moi alisikika akiongea na Radiocall kuwa " Ulimboka kafikishwa MOI lakini bado yuko hai.....ikimaanisha kuna mpango uliokuwepo ambao walidhani angekuwa keshafariki hadi kufikia muda huo. kwa hiyo ni kuwa alikuwa anauarifu utawala kuwa jamaa bado hajafa. Yaani inasikitisha ila at the same time inaonesha jinsi ambavyo serikali ya tz haina akili hata kidogo na hasa baada ya JK aka (raisi mdhaifu) alipojipeleka hospitali kama kawaida yake na yale maneno yake ya kukariri" Serikali inampa pole dokta na tunamtakia kupona haraka na naomba madaktari wawe na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu" alafu huyoooo anasafiri leo nje ya nchi asikilizie soo kwa njia ya simu. Shame shame shame on the weak presida mwiba kura
 
Tunajua kuwa huu ndo upotoshaji mlioupanga kupindisha unyama huu. Mtajilaumu sana kwa kuwatuma wachakachuaji wa mafunzo kutekeleza mpango huu
 

Siku zote polisi kuna uzembe na dharau fulani. Vituoni huwa hakuna hata karatasi. Hata babu yako angepelekwa pale polisi Bunju akiwa katika hali kama ya dk Ulimboka hakuna chochote cha maana ambacho kingefanyika. Naomba nishangae kidogo, hivi serikali haijui kuwa kuna mamia ya madaktari wagomaji na si Ulimboka pekee? Je, haijui kama kwa kumuua Ulimboka huyu angeweza kuibuka Ulimboka mwingine matata zaidi?
 
nimefuatalia na kusikiliza hili suala la Dr. Ulimboka kwa makini sana. Tunapoleekea Watanzania ni kubaya mno ukiangalia matatizo ya nchi kama madagasca, Tunisia, Libya na Hata Syria ni vitu kama hivi kuanza na mtu mmoja kama ilivyo kwa Dr. Ulimboka.

Si ajabu kuanzia leo ukaiona jumuia ya Madaktari wakiingia mtaani kutaka kuiwajibisha serikali na watu wengine wakaungana nao. Mkakati waliofanya hawa jamaa waliomteka Ulimboka ni Dhaifu na wa kijinga sana.

Ukanushaji uliotolewa na Serikali pia ni dhaifu na hatutufanyi tuamini kuwa serikali haiusiki na kadhia hii. Pia yule Mpolisi aliedundwa kule AAR ni sehemu ya kuonyesha udhaifu kwa jeshi letu la Polisi. kwa Hili naomba tuwaunge madaktari Mkono kwa hali na mali ili kukomesha udhaifu huu wa serikali badala ya kutatua matatizo ya msingi inaongeza moto kwenye matatizo yanayotusibu.

Nilishuhudia live pale KCMC jana Madakatari wakiwatimua wenzao mawodini jana mara tu baada ya kupata taarifa za Dr Ulimboka kutekwa. Ukiangalia ule utesaji uliofanywa kwa Dr. Ulimboka unafanana kabisa na utesaji mwingine wanaofanyiwa majambazi,wanaobambikiwa kesi kulazimishwa kukiri na Polisi wetu wa vitengo maalumu. Huku kutoana kucha , kubanwa korodani ni kazi ya Tiss na Polisi.

MPANGO DAHIFU HUO NAOMBA KUWASILISHA
 
Nijuavyo mimi katika hali ile regardless who it was Kituo cha Tegeta as a matter of procedure walitakiwa wampeleke hospitali. Cha kushangaza tunaona Mwanaharakati wa haki za binadamu ndo aliyekwenda kumpeleka hospitali

Pia kuhusika kwa mtu toka ikulu

Pia state propaganda machinery TV ya taifa haikucover hiyo story

Pia kauli ya Pinda before and after the incident
 
Kwa staili ya uongozi wa JK, yeye binafsi sidhani kama anahusika, kwa kuwa watendajhi wake hukosa busara mara nyingi sana na kwa kuwa hana tabia ya kumlinda mtu, au kumpa mtu maelekezo ya nini cha kufanya, mpaka ashindwe ndio anaingilia kati (rejea swala la katiba, rejea mgomo uliopita vongozi wa kada mbalimbali waliropokwa wee mwinsho wakaumbulia na maamuzi na msimamo tofauti) Kuna Maswali muhimu ya kujiuliza ambayo yanasaidia kutafakari:

1. Je, haiwezekani ikawa ni chombo fulani cha dola au taasisi ya serikali (au kiongozi wake) kimeona kitengo chake kinadhalilishwa kwa kushindwa kuzuia vuguvugu hili na wanaona wajichukulie hatu wanazo ona wao ili kulinda kitengo na nafasi walizonazo? Hasa hasa ukizingatia watu wanavyopoteza kazi serikalini kwa kushindwa kusimamia maeneo yao ya kazi (yani hakuna garantee ya post uliyonayo). wako tayari hata kumshauri waziri mkuu vibaya kama walivyofanya kipindi kilichopita.

2. je kutokana na kuongezeka kwa uadui wa kisiasa (wa ndani au/na nje ya CCM), haiwezekani ikawa madui wametake advantage ya situation ku-set more fire? Na kuhakikisha wanafanya kitu ambacho kitaimarisha mgomo na kuifanya serikali ionekane dhaifu na inatumia mbinu chafu? Na hivyo kupelekea watu wa rika la kati (midle class) ambao ndio chachu hasa ya mapinduzi, ingawa sasa hawashiriki kikamilifu katika siasa kwani wako busy na uzalishaji mali.

3. Je watakuwa ni baadhi ya wale waliothiriwa kwa njia moja au nyingine na migomo hii?

Je hawadhani JK angependa busara itumike zaidi kuliko nguvu na maneno ya kejeli? Au kutaka kuonyesha mabavu kwa watu ambao serikali hii ni yao na si yenu nyinyi mlioko madarakani ambao ni dhamana tu mmepewa na haohao wanaolalamika?
 

Kwa vyovyote vile ilivyo, aliyeshika dola ndio ana wajibu wa kulinda mali na maisha ya wananchi wake. Ikishindikana kufanya huvyo lawama anabeba nani?
 
Tunajua kuwa huu ndo upotoshaji mlioupanga kupindisha unyama huu. Mtajilaumu sana kwa kuwatuma wachakachuaji wa mafunzo kutekeleza mpango huu

Ni matumaini yangu kuwa unajua kusoma vizuri. Upotoshaji uko wapi hapo? Nimejaribu kuweka uwezekano wa yote mawili kuwa moja wapo huenda likawa sahihi. Ndugu yangu, itikadi na imani ya kisiasa ikizidi katika akili ya mtu anakuwa mjinga au mpumbavu. Na mjinga siku zote huamini kila neno.
 

Habari nzima ni point kasoro hapo kwenye red,kuhukumu kwa kudhania siyo sahihi kwahiyo hukupaswa kuwapongeza...ni maoni yangu tu.
 
Kwa vyovyote vile ilivyo, aliyeshika dola ndio ana wajibu wa kulinda mali na maisha ya wananchi wake. Ikishindikana kufanya huvyo lawama anabeba nani?
Ndahani, hawsaaaa, ila kwa mchezo ninaouona, kunauwezekano watu wakaingia kwenye mtego sijui ni akina nani hasa watakaonasa, JK na Pinda wakienda vibaya imekula kwao, lazima swala la Uwajibikaji litawakumba... Sina uhakika kama Mh Pinda alivyoongea jana kwanye Bunge, kama tayari alikuwa ameshapata inteligence briefing ya kutosha ikihusisha swala la Ulimboka?? Na kama alikuwa anajua, ile kauli ni mafuta kwenye moto. Nawasihi wtumie na waonyeshe busara na hekima ya hali ya juu ndiyo silaha pekeee yakutatua matatizo yaliyopo sasa, haijalishi chanzo
 

Kwa mtazamo huo basi, washukiwa wa kwanza unafikiri ni kina nani? Kinachoniumiza ni kushindwa kwa serikali kumaliza matatizo ya madaktari kwa diplomasia.Badala yake kufanya kitendo kama hicho baada ya kutishiana nani ndiye mshukiwa mkuu?
 

Naomba kujifunza kupitia kwako. Inamaana unaamini kwa % 100 kuwa serikali imeshindwa kumkamata dk Ulimboka na kumpeleka katika vyombo husika ikaamua kumuua? Je serikali inaamini kuwa njia pekee ya kukomesha mgomo ni kumuua dk Ulimboka wakati ikijua kuna mamia ya madaktari nyuma yake? Tujiulize kwa pande zote mkuu.
 
Ukiona hakuna tamko lolote la CCM wala Bakwata kulaani unyama huu, wala huwezi kuangaika kujuwa kwamba hii ni "Inside Job".
 

Mkuu umeongea ukweli mtupu,
kuna vibaraka wanajaribu kupotosha watu kwa kuitetea serikali uaji ya wanyonge,
sasa kila mtu anaenda anaelewa kwamba serikali yetu ni adui yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…