jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,379
- 25,476
I don't even know where to begin.
Rais tuliyenaye ni janga haeleweki. Na mambo anayofanya, mengi yanavunja katiba ambayo aliapa kuilinda na kuitetea kwa nguvu zake zote!
Kwanza katiba inakataa ubaguzi wa kila aina.
Kwa mujibu wa katiba yetu, ibara inayoelezea kuhusu haki za binadamu, pia inaelezea kuhusu kupinga ubaguzi.
Tafsiri iliyotolewa kwenye katiba kuhusu ubaguzi...
""Kubagua" kama katiba ilivyoainisha, maana yake ni kutizama utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia maoni yao ya kisiasa, kabila, dini, hali yao katika jamii nk. Kwa namna ambayo watu wa aina flani, wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni, na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti, au wanapewa fursa, au faida iliyo nje ya masharti au sifa za lazima"
Ni wazi rais anafahamu fika anachofanya kuwa ni ubaguzi. Ameamuwa tu kutokujali. Pengine madaraka makubwa yamemfanya kuwa more arrogant. Obama alisema juzi kati hapa kuwa hata yeye aliona ni kwa jinsi gani madaraka yalivyo hatari. Na kutegemea na akili ya mtu, wengi hulewa madaraka na kufanya wanachotaka na kuwa bullies!
Mambo kadhaa yaliyonifanya nikaamini kuwa rahisi jiwe anafanya makusudi kabisa na kuharibu taifa letu...Mfano aliwahi kutoa ahadi kuwa atapeleka maendeleo bila kujali sehemu hiyo wamechaguwa mtu mwenye mrengo gani wa kisiasa ama chama gani...Lakini pia matendo yake ni tofauti na wateule wake wanamsaidia kufikisha ujumbe wa kibaguzi kuwa wananchi wasipochagua watu wa ccm hawataepelekewa shghuli za kimaendeleo. Imesababisha hata viongozi wengine(mbali na kuhongwa), wakahamia kule kwenye more priveledges. Ni Imani yangu kuwa mwananchi yoyote yule anastahili kulindwa na katiba kwa mujibu wa katiba hiyo!
Ni wazi kabisa kuwa katiba inakataza ubaguzi hata wa kisiasa, lakini tunasikia kuwa wananchi wakiambiwa kuwa hawatapelekewa maendeleo kwasababu ya misimamo yao ya kisiasa. Huo ni ubaguzi. Katiba haiheshimiwi na ndiyo maana hakuna mwenye kupiga kelele. Wote wanamsikiliza jiwe tu. Utawala wa kisheria umewekwa kapuni.
Kama rahisi hayuko confused, kwanini atoe kauli kanganyifu? Pia matendo na meneno yake mengi yanaonyesha ubaguzi wa wazi kabisa.
Mtu mwenye busara akipata urais, hawezi kuongoza nchi kwa style kama hii! Wananchi wamefikia mahali ambapo wanachukiana wenyewe kwa wenyewe, na wakati tunafahamu kiongozi mzuri ni yule anayewaleta wananchi pamoja kufanya kazi kwa lengo moja na na kwa manufaa ya taifa lao!
Hivi majuzi tu, kuna kauli ya kiongozi wa ccm...
"Mbunge wa CCM akikwambia ataleta maendeleo amini hilo maana Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM" - Kheri James "
"Watu wa Tandale mkichagua kishabiki, hamumkomoi Mtu bali mnajikomoa wenyewe. Msipoichagua CCM hamuikomoi bali mnajikomoa wenyewe. Maamuzi ya nani anakufaa yabaki kuwa yako usiruhusu kuwapa nafasi Watu kukuchagulia. Ukilala na njaa, ukitembea kwenye barabara mbovu, ukikosa huduma bora za kijamii ni wewe pekee utakayeteseka." - Kheri James "
Ninasema kama katiba haitapewa kipaumbele kuliko hata vyama vya siasa, basi tutambuwe kuwa taifa letu siyo tu kwamba litabaki hapa lilipo bila maendeleo ya maana, bali litadidimia kabisa na haitashangaza kuona kuna mataifa yatakayotamani kututawala!
Misingi yote imewekwa na katiba! Na katiba imekataza ubaguzi wa aina zote pale serikali inapodeal na wananchi wake, iwe kupeleka maendeleo kwa wananchi wake, au hata kuwapa huduma muhimu za kijamii kama maji, barabara, umeme nk. Serikali inataka tuone kama vile ni msaada inatupatia au priveledge! Kumbe ni haki kwa mujibu wa katiba ya nchi. Na ni shughuli zinazotokana na kodi za wananchi wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa!
Katiba mpya ni muhimu sana kupita maelezo, wananchi walio wengi bado hawajui umuhimu wake kwasababu maisha yao yote wako chini ya minyororo ya maamuzi na utashi wa watu badala ya sheria na katiba ya nchi! Tutakuja kujutia jinsi ambavyo tulipoteza muda bila ya madai ya katiba mpya kwa nguvu zetu zote!
Ni muhimu tujenge taifa jipya lenye watu wenye kujielewa ili baadaye tupate viongozi bora ambao ni matunda bora ya katiba bora! Na reflection ya wananchi wanaojielewa.
Tunatakiwa tuwapime viongozi wetu kwa mujibu wa katiba na siyo majina mara sijui oooh mimi jiwe! Inasaidia nini? Unaongoza wanyama au ndege? Tunataka nchi yenye kuongozwa na katiba, period!