A confused president and a constitutional crisis!

A confused president and a constitutional crisis!

Angalia teuzi za jiwe kaka
Waislamu wanamwangalia tu!
Bila shaka atakaa miaka yake michache iliyobaki na kisha atakwenda zake
Lakini umma utabaki!!
 
Haya mambo ya siasa za kijinga ndiyo yametufikisha hapa! Hatuchagui viongozi wenye kujielewa wala kuelewa katiba ya nchi! Bunge lingekuwa na watu makini zaidi ya hizi rubber stamps za jiwe(na ccm kwa ujumla kuteua na kuchagua viongozi kwa umahiri wa kutukana wenye mawazo tofauti ya kisiasa), mngeona mambo! Ungekuta limeshamwajibisha jiwe kitambo sana kwa mujibu wa katiba yetu!

"Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria ya 1992 Na.20 ib.8 Sheria ya 1995 Na.12 ib.4 46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii. (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais...

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge."
 
Hakuna kipindi ambacho nchi yetu imekuwa na rais mdanganyifu, asiyekumbuka juzi aliongea nini na leo anaongea nini. Rais anayetaja takwimu za uongo siku nyingine akizirudia zinakuwa ni tofauti na alizozitaja mwanzo. Rais mbinafsi anayeamini mawazo yake ndio msingi bora kumbe anaharibu. Rais asiyeona haya kuwagawa na kuwabagua watanzania kwa utashi wake wa kisiasa. Rais anayejitanaibisha ni rais wa wanyonge lakini ni kinyume chake...
Yapo mengi tu ila wacha niishie hapa......

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, hizi hapa chini ni sababu ambazo bunge lingeweza kumuwajibisha rais, lakini mfumo wetu ambao hata jiwe anaupendelea, ni kuweka vilaza humo wa ndiyo mzee na wa kupiga meza kwa hoja za kudidimiza taifa letu! Kati ya vipengele vyote hapo chini, yani aa, bee na chee, vyote jiwe yumo, lakini hakuna ufuataji wa katiba!

Rais anaweza kushitakiwa endapo...

"a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge."
 
Umeandika upuuzi mrefu lakini hakuna hata mahali ulipoonyesha jinsi katiba ilivyovunjwa.
Hupaoni kwasababu macho ya kuangalia umeyakalia na kichwa cha kufikiri umekikanyagia na unatumia visigino kufikiri! Isembo!
 
Mkuu, hizi hapa chini ni sababu ambazo bunge lingeweza kumuwajibisha rais, lakini mfumo wetu ambao hata jiwe anaupendelea, ni kuweka vilaza humo wa ndiyo mzee na wa kupiga meza kwa hoja za kudidimiza taifa letu! Kati ya vipengele vyote hapo chini, yani aa, bee na chee, vyote jiwe yumo, lakini hakuna ufuataji wa katiba!

Rais anaweza kushitakiwa endapo...

"a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge."
Sasa kwa bunge hili lilolojaa waoga wa kufuatiliwa na Nissan nyeupe unadhani itawezekana mkuu?
Pia hao waliojaa wagonga meza kuvimbisha matumbo yao tu nakupitisha sheria ambazo sasa hivi ni hasara kwa maendeleo ya Tanzania?
Bunge letu tukufu linahitaji kuongozwa na spika kama yule mwanamama wa Uganda mwenye uthubutu hata wa kumkosoa rais, hapo tutapata wabunge jamii ya kina Tundu Lissu na Zitto Kabwe
 
I don't even know where to begin.

Rais tuliyenaye ni janga haeleweki. Na mambo anayofanya, mengi yanavunja katiba ambayo aliapa kuilinda na kuitetea kwa nguvu zake zote!

Kwanza katiba inakataa ubaguzi wa kila aina.

Kwa mujibu wa katiba yetu, ibara inayoelezea kuhusu haki za binadamu, pia inaelezea kuhusu kupinga ubaguzi.

Tafsiri iliyotolewa kwenye katiba kuhusu ubaguzi...

""Kubagua" kama katiba ilivyoainisha, maana yake ni kutizama utashi, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia maoni yao ya kisiasa, kabila, dini, hali yao katika jamii nk. Kwa namna ambayo watu wa aina flani, wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni, na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti, au wanapewa fursa, au faida iliyo nje ya masharti au sifa za lazima"

Ni wazi rais anafahamu fika anachofanya kuwa ni ubaguzi. Ameamuwa tu kutokujali. Pengine madaraka makubwa yamemfanya kuwa more arrogant. Obama alisema juzi kati hapa kuwa hata yeye aliona ni kwa jinsi gani madaraka yalivyo hatari. Na kutegemea na akili ya mtu, wengi hulewa madaraka na kufanya wanachotaka na kuwa bullies!

Mambo kadhaa yaliyonifanya nikaamini kuwa rahisi jiwe anafanya makusudi kabisa na kuharibu taifa letu. Mfano aliwahi kutoa ahadi kuwa atapeleka maendeleo bila kujali sehemu hiyo wamechaguwa mtu mwenye mrengo gani wa kisiasa ama chama gani...Lakini pia matendo yake ni tofauti na wateule wake wanamsaidia kufikisha ujumbe wa kibaguzi kuwa wananchi wasipochagua watu wa ccm hawataepelekewa shghuli za kimaendeleo. Imesababisha hata viongozi wengine(mbali na kuhongwa), wakahamia kule kwenye more priveledges. Ni Imani yangu kuwa mwananchi yoyote yule anastahili kulindwa na katiba kwa mujibu wa katiba hiyo!

Ni wazi kabisa kuwa katiba inakataza ubaguzi hata wa kisiasa, lakini tunasikia kuwa wananchi wakiambiwa kuwa hawatapelekewa maendeleo kwasababu ya misimamo yao ya kisiasa. Huo ni ubaguzi. Katiba haiheshimiwi na ndiyo maana hakuna mwenye kupiga kelele. Wote wanamsikiliza jiwe tu. Utawala wa kisheria umewekwa kapuni.

Kama rahisi hayuko confused, kwanini atoe kauli kanganyifu? Pia matendo na meneno yake mengi yanaonyesha ubaguzi wa wazi kabisa.

Mtu mwenye busara akipata urais, hawezi kuongoza nchi kwa style kama hii! Wananchi wamefikia mahali ambapo wanachukiana wenyewe kwa wenyewe, na wakati tunafahamu kiongozi mzuri ni yule anayewaleta wananchi pamoja kufanya kazi kwa lengo moja na na kwa manufaa ya taifa lao!

Hivi majuzi tu, kuna kauli ya kiongozi wa ccm...

"Mbunge wa CCM akikwambia ataleta maendeleo amini hilo maana Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM" - Kheri James "

"Watu wa Tandale mkichagua kishabiki, hamumkomoi Mtu bali mnajikomoa wenyewe. Msipoichagua CCM hamuikomoi bali mnajikomoa wenyewe. Maamuzi ya nani anakufaa yabaki kuwa yako usiruhusu kuwapa nafasi Watu kukuchagulia. Ukilala na njaa, ukitembea kwenye barabara mbovu, ukikosa huduma bora za kijamii ni wewe pekee utakayeteseka." - Kheri James "

Ninasema kama katiba haitapewa kipaumbele kuliko hata vyama vya siasa, basi tutambuwe kuwa taifa letu siyo tu kwamba litabaki hapa lilipo bila maendeleo ya maana, bali litadidimia kabisa na haitashangaza kuona kuna mataifa yatakayotamani kututawala!

Misingi yote imewekwa na katiba! Na katiba imekataza ubaguzi wa aina zote pale serikali inapodeal na wananchi wake, iwe kupeleka maendeleo kwa wananchi wake, au hata kuwapa huduma muhimu za kijamii kama maji, barabara, umeme nk. Serikali inataka tuone kama vile ni msaada inatupatia au priveledge! Kumbe ni haki kwa mujibu wa katiba ya nchi. Na ni shghuli zinazotokana na kodi za wananchi wote bila kujali misimamo yao ya kisiasa!

Katiba mpya ni muhimu sana kupita maelezo, wananchi walio wengi bado hawajui umuhimu wake kwasababu maisha yao yote wako chini ya minyororo ya maamuzi na utashi wa watu badala ya sheria na katiba ya nchi! Tutakuja kujutia jinsi ambavyo tulipoteza muda bila ya madai ya katiba mpya kwa nguvu zetu zote!

Ni muhimu tujenge taifa jipya lenye watu wenye kujielewa ili baadaye tupate viongozi bora ambao ni matunda bora ya katiba bora! Na reflection ya wananchi wanaojielewa.

Tunatakiwa tuwapime viongozi wetu kwa mujibu wa katba na siyo majina mara sijui oooh mimi jiwe! Inasaidia nini? Unaongoza wanyama au ndege? Tunataka nchi yenye kuongozwa na katiba, period!
Asante kwa post nzuri.Tumekusikia mama
 
Miaka 5 ni mingi sana kwa Rais wa dizaini ya Jiwe. Kila hotuba yake moja lazima izue mijadala pingani isiyohesabika!
 
Jiwe anajua anachofanya. Ndo maana anadhoofisha upinzani kwa ufisadi wa kununua wanasiasa ili kupunguza au kuondoa kabisa wakosoaji wake.

Hata haki ya wananchi kuchagua wawakilishi ni kama haipo kwa sasa. Maigizo na wizi wa wazi kwny chaguzi umetamalaki
 
Inaonesha kuwa kumbe watu walio madarakani siyo lazima wawepo kwa ajili ya watu wanaowaongoza. Kila kitu hutegemea utashi zaidi kuliko taratibu zinazowekwa.
Na, hivi katiba yetu iliandikwa lini, na nani, na ilipataje mambo ya kuandikwa humo?
Wananchi "majority" yao sidhani hata wanajihusisha, yote yafanyikayo ni kwa utashi na hisani zaidi.
 
Hivi kwa nini huu ubaguzi unaendelea na sisi kama Taifa tumekaa kimya? Ilianza kupigwa marufuku mbunge wa jimbo moja kuongea na watanzania wa jimbo lingine. Sasa imekuja ya kupiga marufuku kupeleka maendeleo kwenye jimbo la chama tofauti na chama cha kiongozi wetu wote.
 
Kaya yetu kwa sasa haiongozwi kwa kanuni na sheria za kaya yenyewe bali kwa utashi wa aliyekalia kiti.
 
Awamu hii kuna mambo mabaya sana yameinuka.
ukanda/ukabila
upendeleo wa waziwazi wa kikanda na itikadi
demokrasia imebanwa mno
uhuru wa vyombo vya habari hakuna
Tusali, kufunga na kuomba sana kwani hata Mungu hawezi kuwa kati yetu tena.
 
Hivi kwa nini huu ubaguzi unaendelea na sisi kama Taifa tumekaa kimya? Ilianza kupigwa marufuku mbunge wa jimbo moja kuongea na watanzania wa jimbo lingine. Sasa imekuja ya kupiga marufuku kupeleka maendeleo kwenye jimbo la chama tofauti na chama cha kiongozi wetu wote.
Huwa najiuliza sana mkuu. Nadhani kuna tabia ambazo ni general kwetu sisi waafrika ambazo bila shaka ziliwavutia hata wageni kututawala.

Pia utamaduni wa kutizama individuals Zaidi bila kufahamu kwamba taifa letu linaongozwa kwa taratibu zake, mfano katiba ambapo hakuna aliye juu yake hata rais wa nchi.
 
Awamu hii kuna mambo mabaya sana yameinuka.
ukanda/ukabila
upendeleo wa waziwazi wa kikanda na itikadi
demokrasia imebanwa mno
uhuru wa vyombo vya habari hakuna
Tusali, kufunga na kuomba sana kwani hata Mungu hawezi kuwa kati yetu tena.
Yote hayo mkuu wangu ni kinyume kabisa na katiba hii tuliyonayo. Tatizo ni bunge.
 
Yote hayo mkuu wangu ni kinyume kabisa na katiba hii tuliyonayo. Tatizo ni bunge.

Bunge lenyewe halionyeshwi wazi kwa wananchi tena kama ilivyokuwa awamu ya4..tatizo ni Huyu "kichaa" tulonaye na watanzania wasipoamka na kudai haki zao kwa protests and strikes hakika tutatawaliwa na sio kuongozwa..hili limejidhihirisha wazi Trillion 1.5 inafanya kazi ya kununua wabunge madiwani na viongozi wengine wa serikali...ili apate nguvu ya kubadilisha katiba aendeleze utawala wake usio na misingi ya sheria.. sijui Huyu mtu. Tanzania is a country that is going down in history like never before, having this lunatic who has proven himself a maniac is a disgrace to mental health Tanzanians...He must go

Over
 
I see there is a serious problem somewhere. Nyakati za nyuma, wananchi walijali kidogo kuhusu katiba ya nchi. Enzi za chama kimoja, kulikuwepo na wale kina Njelu Kasaka. Walisimamia katiba and they were proud of it. Kuna namna viongozi wetu wanacheza na akili za watanzania. As if baada ya multiparty system, hakuna tena katiba ya kuongoza nchi. Hili ni tatizo kubwa, hakuna uzalendo. Na uzalendo unajengwa na katiba bora mtu asikudanganye.

Kwasasa nchi ni kama inaongozwa na waswaga ng'ombe na ng'ombe ndo wananchi! Sijawahi kusikia wananchi wakiwa proud kuhusiana na katiba yao ambayo imebeba haki zao zinazovunjwa kila kukicha.
 
Back
Top Bottom