Mkuu JMushi1, umeandika kwa mantiki iliyotulia vyema. Lakini usihau kuwa huyu Rais ni zao la jamii ya Watanzania. (Jiulize kwanza sisi Watanzania ni watu wa aina gani kutoa Rais wa aina hii?) Dhana ya kutokuwepo mtu aliye juu ya sheria inabakia kuwa dhana tu hapa nchini. Bila shaka unafahamu kuwa tangu uhuru Rais wa Tanzania amekuwa juu ya sheria - awamu zote. Watanzania kwa ujumla wetu tumeruhusu hali hiyo kuwepo huku tukishabikia watu (individual presidents) na kuwalinganisha kama vile tunatarajia miujiza ya kiuongozi toka kwao badala ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia miongozo thabiti ya kikatiba.
Muasisi mwenyewe alitahadharisha kuwa katiba “aliyotutengenezea” inamwezesha kuwa dikteta mbaya sana. Au anaweza kutokea dikteta mbaya zaidi kwa katiba hiyo. Ajabu ni kuwa hakuwa na utashi wa kutaka kuirekebisha. Tatizo kubwa zaidi ni mtindo wa uongozi aliouasisi wa raisi asiyehojiwa. Sasa kaingia “kichaa”. Na yeye (huyo kichaa) anautumia mfumo Huo kikamilifu. Tena yeye na chama chake hawana mpango wa kurekebisha urithi maridhawa walioachiwa na muasisi. Kazi kwetu!
Well said mkuu
Drifter . Kwanza nashukuru sana kwa nasaa zako. Nakumbuka wewe ni mmojawapo wa members ninaoheshimu nondo zao. Umepotea sana mkuu.
Umesema vyema kabisa mkuu. Mambo kama haya yanakasirisha sana. Kwasababu unaona kabosa viongozi pengne kwasababu ya ubinafsi wao, wako radhi taifa liendelee kudidimia. Na kama ulivyosema, muasisi aliona huo udhaifu, na alisema wazi. Sijuikwanini hakutaka kusimamia hilo? Kwasababu kiukweli katiba hata hii ilikuwa ya kikoloni. Haikuwa kwa manufaa ya Tanganyika na watanganyika, bali Malikia kwa kupitia Gavana ambaye ndo alikuwa na mamlaka kama ambayo rais anayo. Mamlaka yote yaliyokuwa chini ya Gavana na yale ya Waziri Mkuu yaliunganishwa na kuwa chini ya Rais wa Jamhuri.
Na yote haya ccm wanayafurahia kwasababu yanawafanya wao kuwa kama wakoloni sasa na jiwe kama Gavana.
Baada ya uhuru, kulikuwepo na justifications, lakini kwasasa hazina mantiki...Sababu mainly zilikuwa mbili, kwanza, kujenga umoja wa kitaifa, na pili, kuleta maendeleo ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi ambayo ilikuwa chini. Hayo yalifanyika kutokana na changamoto za wakati huo.
Kwamfano, katiba ya Marekani inatamka kuwa Rais, Makamu wa Rais, na “Maafisa wote wa umma wa Marekani” wanaweza kuondolewa madarakani na Bunge wakipatikana na hatia kwa makosa ya rushwa, uhaini au uhalifu mwingine mkubwa. Bunge limepewa mamlaka ya kumshtaki na kumuondoa Rais madarakani.
Lakini pia, kwa upande wetu, uwezo wa Bunge kudhibiti madaraka ya Rais na kuleta uwajibikaji unaathiriwa na mambo kadhaa wa kadha ambayo ni lazima yatizamwe kwenye katiba mpya.
mfumo wa kuteua Mawaziri na Manaibu wao kutoka miongoni mwa Wabunge na uwepo wa Wabunge mpaka 10 wanaoteuliwa na Rais kunaongeza ushawishi wa Rais katika utendaji wa Bunge na hivyo kuathiri uwezo wake wa kuisimamia na kuiwajibisha serikali pale inapobidi na kama inavyohitajika ili kuweka balance kati ya mihimili.
Rais pia anaweza kuteua wakuu wa mikoa na wilaya kutoka miongoni mwa wabunge. Bunge linaweza kushindwa kumdhibiti Rais na Serikali yake kwa kuwa Serikali yake ni Wabunge wenzao, tumeshuhudia jinsi lilivyo bunge la kupiga meza tu na rubber stamp. Hata majuzi rais alisema kuwa gesi imechukuliwa na mabepari, na wakati mkataba walisaini wao kwa sharia ya dharura waliyopitisha bila hata ya kuipitia. Waliopinga waliitwa wasaliti wa Taifa.
Pia, Wabunge wanaweza kushindwa kufanya kazi ya kuisimamia Serikali kwa matazamio ya kuteuliwa kuwa Mawaziri. Wabunge ambao ni Mawaziri, ambao wanaweza kuwa wengi kwa kuwa Katiba haijaweka ukomo wa idadi, wanamaslahi kuhakikisha kumlinda Rais na Serikali ambao wao ni sehemu.
Zaidi ya hayo, uteuzi wa Mawaziri miongoni mwa Wabunge unafanya Bunge kuwa sehemu ya Serikali na hivyo kushindwa kufanya kazi ya kuisimamia Serikali ipasavyo.
Kwa wenzetu, Ili kuleta uwajibikaji kati ya Bunge na Rais, mfano katiba ya Marekani inazuia Mawaziri kuwa Wabunge na hivyo kuwa na utofauti kati ya Bunge na Serikali. Hakuna Mbunge yeyote anaruhusiwa kuteuliwa Serikalini ila mpaka ajiuzulu nafasi yake. Rais wa Marekani hana mamlaka ya kulivunja Bunge. Mfumo huu, unasaidia kila upande kuweza kufanya kazi zake kwa madhubuti katika kusimamiana na kuwajibishana.
Pia vilevile Rais ana madaraka ya kupanga na kuamua mishahara na posho za Wabunge, hivyo kuwa na uwezo wa kutumia fursa hiyo kama njia ya kushawishi utendaji wa Bunge.
Rais anaweza kulivunja Bunge kama ilivoainishwa kwenye ibara ya 90(2)(a); (a) Bunge likikataa kupitisha Bajeti iliyopendekezwa na Serikali; (b) Likikataa kupitisha Muswada wa sheria ambao Rais anautaka au Bunge likisisitiza kupitisha muswada ambao Rais hautaki.
Kama ulivyosema mkuu, uko sahihi kabisa kuwa wananchi hawafahamu umuhimu wa katiba, wala hawafahamu inasemaje kuhusu mustakabali wao na ule wa taifa kwa ujumla. Lakini pia ni lazima tudai katiba mpya ambayo haina makandokando kama haya ambapo nchi ibado inaendeshwa kama vile iko chini ya mkoloni! Kitu kilitufanya tukasahau sana ni issue ya uhuru, na kwamba tulikuwa na Imani na kiongozi wa nchi kuwa ana nia njema na taifa! Lakini pia hiyo ni loophole ambayo inaweza kutumiwa na maadui wa taifa. Mfano hii situation tuliyonayo sasa ambapo tumeshaanza kuwa maadui sisi kwa sisi.