How do you rate Mbowe as a leader?
Nyani , it's difficult to rate him by fixed quantity
Kama kiongozi amekitoa chama cha tatu kwa upinzani kuwa chama kikuu cha upinzani, kudos
Ameweza kukisimamisha at the the time of trial and tribulations.
NCCR and CUF could not withstand. As a leader he has endured a lot
Kwa upande mwingine ni mtu anayeongoza kwa 'acquired skills siyo embedded leadership traits
Mbowe ameongoza chaguzi zaidi ya tatu bila matokeo ya kuridhisha. Arguably wapo wanaosema kuna ongezeko la Wabunge na madiwani. Wapo sahihi, lakini je wanafikiri nini kuhusu muda?
Mbowe asilaumiwe kwasababu mfumo wetu ambao sanduku la kura linachukuliwa kituoni na kurudishwa bila chombo chochote kushtuka, ni aghalabu kuna kushinda kwa aliye nje ya mfumo
Katika mazingira hayo, kuna haja ya kuwa na maono tofauti. Kilichopo ni 'insane' so to speak
Hapa ndipo alaumiwe, kwa kukumbatia insanity!
Wakati akiwa kwenye peak kulikuwa na pressure ya katiba, ambayo ingekuwa jawabu kwa sehemu kubwa ya matatizo ya chaguzi, siyo absolute but by far
Mbowe akakubali kirahisi uundwaji wa tume na chama kile kile kinachonufaika na mfumo uliopo
Alikuwa na mass support ambayo ingempa leverage na si kumuunga mkono JK kirahisi tu
Katika wakati ule , alipaswa kukataa ili kuwepo na 'uwanja sawa' utakao sawazisha hali
CCM wakatumia Bunge kuvuruga mchakato makusudi na Upinzani wakarudi square one
Pili, lengo la chama cha siasa ni kuchukua uongozi wa nchi. Kuna taratibu za mkato na za mbinu
Kwa sheria za nchi yetu njia za mkato ni chaguzi ambazo zimefeli.
Njia za mbinu ilikuwa ni upinzani uwe na wabunge wa kutosha. Mbowe hakuona hilo
Nguvu nyingi zikaelekezwa kwa kupokea wahamiaji na personality akiwa kiongozi
Hata kama mgombea asingeshinda,ni wazi asingeshinda, kulikuwa na uwezekano wa kuwa na wabunge wengi wa upinzani. Mabadiliko katikati ya uchaguzi ilikuwa kosa la kifundi, alishiriki
Makosa ya kutokuwa na vyombo huru yameendelea kuwagharimu Wapinzani
Mfano, kwanini walisusia uchaguzi wa Singida-Nyalandu, wakashiriki wa Kinondoni na Siha.
Busara zipi zilitumika. Utaona ombwe la uongozi na kukosekana kwa dira ya nini kifanyike
Chama kinapopita katika misuko suko kuna ulazima wa kufanya 'reform' kuona kama kuna wenye mbinu tofauti. Reform inaongozwa na uchaguzi ili kupata mandate
Baada ya chaguzi nyingi kupita nadhani CDM wana uwezo wa kujua kama kuna haja ya mabadiliko au la. Mbowe hajatumia busara kubaini hilo
Kwa vile mandate ya wanachama haionekani ni rahisi kwake kutuhumiwa
Kila anayenunuliwa hoja yake kubwa ni hiyo. Hivyo, anawapa hoja kwa gharama ya chama
Sasa nikijibu swali lako naweza kusema kuna 'ambivalence' kwa kutazama uongozi wake
Ni ngumu kumpa fixed quantity kwasababu kuna so many variables, kwa mfano, yeye kama kiongozi, busara na hekma, wananchi kwa ujumla, wapinzani,vision , mifumo ya vyama n.k.
CDM wanachoweza kufanya ni kuwa na uchaguzi wa reform ya uongozi.
Hii haina maana ya kumuondoa, kama atapewa mandate haina tatizo.
Yeye kama kiongozi anaweza kujipima kama bado ana kitu cha kufanya au ni wakati wa kutoa kijiti kwa wengine. Hilo ni baina yake na wanachama wao