90% ya wafanyakazi wa Serikali wanapiga soga na story maofisini. Je, tunawalipa mishahara ya bure?

Sisi wote ni wapiga stori tu. Wewe jiulize ni nani aliyepitisha miswada na sheria zote zilizoruhusu lundo na tozo kwa wananchi.

Hao viongozi wako wanatenga tsh ngapi kwa ajili ya matumizi(posho, mishahara n.k) na wanatenga tsh ngapi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kodi zote wanazokusanya zinaishia mifukoni mwa wanasiasa, wakati zahanati hazina madawa na vifaa tiba vya kutosha.

Wewe na wanasiasa wenzio ni matapeli tu, sasa "mumejiandaa kumlipa mtumishi wa umma kiinua mgongo kwa asilimia 33% , unataka afanye kazi ipi!?.
 
Binafsi ni mtumishi. Wakati wa jpm nlikuwa nafanya kazi kama.mchwa ila saiz saa5 nishamaliza narudi kulala home
 
Haya Darasa hilo hapo, na KPI hizo hapo.

Fanya MIUJIZA tuone.

Mshahara, Basic Tsh 484,000 ( Toa 3%ya Bima, 9% ya Kodi, 2% ya CWT na 3% ya PSSSF huku ukitegemea Kikokotoo Cha 33% baada ya kazi ya miaka 30)

Huna nyumba ya kukaa, umepsnga, una familia yako, Kodi ya pango ni miezi 6.

Fanya kazi Sikukuu, weekend au baada ya muda wa kazi HAKUNA MALIPO.

Narudia Tena, FANYA MUUJIZA TUONE.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    48.7 KB · Views: 2
  • IMG_20230206_165232.jpg
    IMG_20230206_165232.jpg
    319.2 KB · Views: 2
Haya Darasa hilo hapo, na KPI hizo hapo.

Fanya MIUJIZA tuone.

Mshahara, Basic Tsh 484,000 ( Toa 3%ya Bima, 9% ya Kodi, 2% ya CWT na 3% ya PSSSF huku ukitegemea Kikokotoo Cha 33% baada ya kazi ya miaka 30)

Huna nyumba ya kukaa, umepsnga, una familia yako, Kodi ya pango ni miezi 6.

Fanya kazi Sikukuu, weekend au baada ya muda wa kazi HAKUNA MALIPO.

Narudia Tena, FANYA MUUJIZA TUONE.
mpwayungu village ,tuwapigie debe waongezewe maslahi aisee
 
Mishahara lazima iendane na uwezo wa Ukuaji wa uchumi, Ofisi za serikali zimejaa uvivu, story, nyodo muda wa kazi, Lunch masaa mawili, Pesa kubwa mnazotaka wakati hamtoi huduma bora kwa wakulima na wafanyabiashara zitatoka wapi?

Nyongeza ya mshahara aliyoitoa Samia mwaka huu inabidi mshukuru sana, Tunaoenda kuumia na kulipia hiyo gharama ni sisi wafanyabiashara na wakulima, Zigo la kodi kulipia hiyo nyongeza ni kubwa sana, Ni zaidi ya mabilioni yameongezeka kwenye bili ya mshahara kwa serikali, Zigo linahamishiwa kwenye kodi ya sisi wakulima na wafanyabiashara ili tulipie gharama hiyo ya nyongeza ya mishahara

Kada ya utumishi wa serikali inaongoza kwa kuwapotezea muda wakulima na wafanyabiashara wafikapo kufuata huduma, Wafanyakazi wa serikali hamjali muda mnaotupotezea muda, Tutazalisha saa ngapi ili kodi ipatikane na Nyie mnufaike?

Wafanyakazi wa Serikali mlipoambiwa Fedha za ndani zinajenga nchi,mlifikiri zinatoka wapi? Ni sisi wafanyabiashara na wakulima tulibanwa koo kwa kabali kisawa sawa kwa kulipishwa kodi kuwezesha miradi ya barabara, Flyovers na vituo vya afya

Mtu anasema nyongeza ni ndogo, Unataka nyongeza kubwa kwa kazi gani ya maana unayofanya Jumatatu mpaka Ijumaa ofisini, Ofisi nyingi za serikali siku ya ijumaa ni kama haipo, Watu wanaunganisha ile muda wa kuswali ijumaa moja kwa moja nyumbani

Unataka pesa kubwa kwa masaa mangapi unayozalisha?

Unataka pesa kubwa kwa huduma gani bora unayatoa kwa wakulima na wafanyabiashara?

Ukiondoa kada ya Afya na ulinzi wa nchi na Raia, Wafanyakazi wa taasisi za serikali wamejaa nyodo, dharau na uvivu hasa akina Dada pale unapofika kuuliza huduma

Wengi ya wafanyakazi wa serikali wana uelewa mdogo sana bado hawajaelimishwa kuwa mishahara yao ni kodi za sisi wafanyabiashara na wakulima ukijumlisha na kodi toka wafanyakazi wa sekta binafsi

Ukifika ofisi za NSSF au Psssf kwa wazee wanaofuatilia mafao yao, Majibu ya wale akina Dada vijana na wale watoto wa kiume kwa wazee yamejaa dharau sana, Wanasahau kuwa bila kodi za wananchi wasingekuwa pale

Kwa miaka mitano iliyopita wafanyabiashara tumepigwa kodi za kutosha kuhudumia Flyover na mabarabara, Tumeumia kujenga shule na hospitali za kata

Je wafanyakazi mlipoambiwa Fedha za ndani mlijua zinatoka wapi? na ni nani analipa hizo kodi?

Ni muda muafaka wa wafanyakazi wa serikali kuelimishwa kuwa pesa za mishahara sio mikopo bali ni kodi za wakulima na wafanyabiashara

Hakuna Taifa linalolipa mishahara kwa pesa za mikopo, Bili ya mishahara kwa mwezi ni kodi zinazokusanywa toka kwa wakulima na wafanyabiashara

Mambo yafuatayo yasipokoma au kubadilika maofisini ni ngumu sana sisi wakulima na wafanyabiashara kuweza kugharamia nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa serikali

1. Uvivu na dharau, Kuchart na simu huku unatusikiliza kwa sikio moja, Baada ya Kuchart utasikia ulikuwa unasema nini vile au Wewe Bibi, Mzee tuliishia wapi, Hapo muda wa zaidi ya saa moja la kuzalisha limepotea na Biashara yako Umefunga kwa muda huo

2. Lunch masaa zaidi ya moja, Bado mtu amerudi lunch anapiga umbea huku akiendeleza kula mezani masalia ya chakula yaliyobaki na kuyafungasha toka canteen au kwenye mgahawa, Hapo muda wa kuzalisha ulishapoteza


3. Habari za njoo kesho au njoo baada ya week mbili, Huwezi endesha biashara yako hapo unasubiri kibali cha manispaa au Halmashauri kwa siku mbili, Hakuna uzalishaji

4. Bosi amesafiri hakuna wa kuweka saini, Hapa unakuta ni saini ya mtu mmoja tu wa Mazingira ili kuruhusu biashara iendelee lakini utasubiri mwezi na kusimamisha uzalishaji wa biashara yako

5. Kaa pale Subiri wameenda kula, Tuna semina uje kesho, Hiyo ni semina isiyo na kikomo ambayo hawamuachi hata mtu mmoja wa kusaidia wafanyabiashara na wakulima

6. Faili lako halionekani, Tunatafuta tutakupigia simu, Hiyo ujue ndio kimoja, Ni Jibu wanalotoa ili uondoke ofisini waendelee na soga na umbea wa mitaani bila kujua tayari wamepoteza kodi ya serikali

Kwa staili kama hizi, Tutazalisha muda gani? Mapato yataongezeka kutoka wapi? Muda wa kuzalisha watu wanakupiga kalenda na danadana, Siku ya Mei mosi unasikia tunataka nyongeza Kubwa, Nyongeza toka kwa kodi ya nani?
sasaivi kero inayo trend kwenye ofisi za serikali ni pale unapohitaji huduma alafu unaambiwa mtandao unasumbua tokea asubuhi. Yani hichi kitu kinanikera sana.
 
Unaweza kua unamtukana baba ako ujue mana nimetembeza sana mjegeje enzi zangu.. unamwambia baba ako ainame? Laana ya sodoma ikushukie
Mimi nimefira sana wapuuzi Kama nyie, yawezekana ulisha chezea sana
 
Back
Top Bottom