8th Sullivan Summit Arusha Tanzania

Rev.Kishoka,
Nina hakika umefuatilia sana hoja zangu za nyuma na utakubali kuwa mimi huwa sina ushabiki wa mtu wala siwezi kuweka dhamana yangu kwa mtu yeyote. Yes, hapa hapendwi mtu awe kabila, rangi ama dini yeyote maadam yuko je ya maslahi ya Tanzania.

Hayo yote uliyoyazungumza hapo juu ni maswala yanayotuhusu sisi na watawala wetu kina JK Karamagi, Kasungura na kadhalika na hayawezi kuhusishwa moja kwa moja na Sullivan hata kidogo.
Katika mikutano yote ya kiuchumi hawa watu huwepo, huwezi kumwondoa Karamagi ubavuni mwa JK ktk misafara inayohusu maslahi ya nchi. Kuwepo kwake ktk picha ni dhahiri ulitaka nani awepo maanake ndio viongozi wetu hawa. badala ya sisi kutazama timu nzima ya viongozi wetu na kuitoa makosa tunaangalia Sullivan ambao wanaingia tu baada ya sisi kujitwika mizigo kisha tunalumu wao walikuwa wapi?.. could they hve stopped Mkataba wa Buzwagi, IPTL or any other bila kuhusishwa? Na wala sii kweli kuwa Sullivan ina mahusino na Barricks kibiashara kwani barricks ni public company ambayo hata wewe unaweza wekesha fedha zako isipokuwa tunatazama ni akina wwekeshji wkubwa wa kampuni hii mbo ni Ex Presidaa Mzee Bush, Prime minister wa Canada Brain Moroney na Kashogi wengine wote akina sisi ni fisi tunaosubiri mifupa.
Sasa, kama tungetaka mabadiliko ya aina yeyote basi kwanza tungeanza kuwatazama viongozi wetu kwa maana hakuna mkutano ama mkusanyiko wowote wa kitaifa unaoweza kuwepo bila mafisadi hawa kutuwekea kifua na ukitazama ziara zote za Jk zimekuwa na hawa watu hata msafara wa Rome JK aliongozana na baadhi mafisadi.Je, tunaweza ku uestion ziara hiyo kwa sababu kulikuwepo na watu ambao sisi tunafahamu hawana uzalendo wala imani na nchi yetu?..
Binafsi ninaamini kabisa kuwa kama tutaweza kushirikiana na hawa jamaa pamoja na kwamba hawana fedha ila vichwa vyao tunaweza piga hatua sana.
India wasingepata Uhuru wao bila mchango wa Indira Ghandhi ambaye alikuwa akiishi South Africa...na ktk mafundushoi yke wahindi wamepata kuwa kitu kimoja kila kona ya dunia na mafia wanaoogopeka. Wachina vilevile, Maleysia, Thailand -U name it wote leo hii wamegundua kuwa jumuiya zao bila kujali tofauti ndogo ndogo kati yao ni muhimu ktk dunia hii ya Utandawazi. Sisi ndio kwanza tunavuana nguo kutazama nani katiwa jando utafikiri suala la ushirikino linahusina na ngono.
Na siku zote Sullivan wameshindwa kujenga kitu kwa sbabu siku zote wameonekana ni politians na wababaishaji waliokosa nafasi US sasa wamekimbilia Afrika baada ya kuona mali tulizokuwa nazo...Yew, hao wazungu na wahindi hakuna anayewatazam kwa jicho hilo hilo kwa sababu tu wameingi na fedha. Yaani mikataba yetu hutolewa kama posa za kiswahili, mwenye mfuko mkubwa ndiye huchukua mke hata kama hakuna mapenzi!

Mimi napinga mtazamo huu kutokana na kile nilichojifunza toka kwa wenzetu. Tazama wachina wamesikia tu kuwa Bongo kuna biashara safi wamekuja kama ssungusungu unafikiri waliyajua vipi haya kama sio kupitia mtandao wao?...
Leo hii wahindi wanarudi Tanzania kama vile hkuna kewsho kutokana na taarifa zinazosambazwa na jumuiya zao. majuzi Agha Khan alikuja warudisha wahindi wa dhehebu la Islmailia kibao huko Bongo wewe muulize mtu yeyote hapo Bongo atakwambia kuwa mwezi June kuna wahindi kibao walishuka Bongo... Hii imetokana na mshikamano wao toka enzi. Kumbuka hata wakati wa Idd Amin alipowafukuza wahindi haikuwa adha kubwa kama wangekuwa watu weusi kwa sababu hawa jamaa hujiandaa kwa vitu kama hivi na wamekubali kuwa wao ni WAHINDI na they need each other!
leo hii sisi ndio kwanza mtu mweusi ni adui yako wa kwanza na atyi hapendwi mtu wakati sisi wenyewe hatuna sura wala mfuko. hata huyo malaya wa mtaani hutegemea hata sura ama mguu wa kumvuta mteja!.. We are POOR brother lazima tulikubali hilo na kinachofanyika sasa hivi ni sisi kujipanga upya. Tukubali nafasi yetu kama weusi ktk dunia hii ya Utandawazi kisha tujenge nia na malengo ambayo hata yakifikishwa Marekani kesho kuna watu watakao simama kututetea.
Umeuliza kuhusu Tanzania itafaidika nini na hawa Sullivan!... Je, tumewahi faidika kwa uhusiano mwingine wowote na mzungu ama mwarabu? na kwa nini tuweke question leo hata kitu hakija launch ama kwa sababu hawa jamaa hawana mfuko?... ule ule mtazamo wa pos y kiswahili mke kama angekuwa Bill Gates sidhani kama kuna mtu angeuliza malengo na faida ya mkutano huo...simply because anazo fedha za kumwaga.
rev. binafsi ningeomba tuwape nafasi hawa jamaa kwani toka mwaka 1970 nchi za kiafrika zimekuwa zikiwatenga na kuwaona wao kama ni tishio kubwa tawala zetu. Nina hakika kabisa kuwa kina Karamagi wanaweza kuwa na woga zaidi wa Sullivan kuliko sisi kwani hawa viongozi wetu ni wezi wakubwa na kuna hatari kubwa ya ufisadi wao kupata upinzani mkubwa toka nje ama kuwekwa wazi.
Turudi ktk maneno ya mwl. Nyerere kuwa maendeleo hata siku moja hayaletwi na fedha!..tusiwatenge ama kuwawekea dhana kwa sababu tu hawana fedha.
Bill Gates hakuanza na mtaji mkubwa, mzee wetu Mengi alikuwa na fedha kuliko Bill lakini leo ni billionea mkubwa duniani!

PS:- PC yangu ina matatizo ktk baadhi ya herufi zinagoma, naomba samahani pale maneno yanapokuwa hayaeleweki.
 
Mkandara,
Nakuomba usome kitabu cha Kwame Nkrumah "Neocolonialism, the last stage of imperialism." Andrew Young kishaacha kazi serikalini na sasa ni kutafuta tu ulaji. Haiamkiniki kuwa George Shultz ndiye hero wake. Martin Luther King Jr. anageuka mara tisini huko kaburini mwake. Hatutaki Afrika ambayo itaendeshwa kwa amri za corporate America. Tunahitaji wawekezaji, ndiyo, lakini si wawekezaji ambao watatuacha na magofu kama ilivyo hivi sasa na Barrick. Mimi naunga mkono mkutano wa Sullivan kufanyika Tanzania, lakini sikubaliani na uwekezaji ambao kila faida ya raslimali zitaishia nje. Mount Meru imeshachukuliwa na kampuni ya Andrew Young. Guess what, most of the guests wataishia pale, fedha za faida zikirudishwa Marekani na sisi tukibaki na tips peke yake.
Capitalism siri yake ni accumulation of capital. Katika mchezo huu sisi tunachezewa kweli kweli!
 
Jasusi,
Nakubaliana na mawazo yako kulingana na mtazamo wako isipokuwa unachoshindwa kuelewa ni kwamba Tanzania ama nchi yeyote maskini au Tajiri haiwezi kuepuka uwekeshaji wa big corporates hata kidogo isipokuwa ni sisi wenyewe kuzitazama mikataba yetu kuwa na maslahi kwetu zaidi. Hii ni dunia mpya kabisa na shurti sisi tukubali mabadiliko hayo laa sivyo tutabaki nyuma siku zote.
Huwezi kuwalaumu Barricks ikiwa wao ndio wamekubaliwa kutunga mkataba na kisha sisi kutekeleza yale yaliyokuwemo. I mean tumekuwa kama wahindi kuwa mke ndiye hutoa posa na mahari kisha tunataka kulaumu mume aliyepokea fedha hizo. Utaratibu wa mikataba yetu ndiyo muhimu zaidi sio mwekeshaji ambaye tayari tumekwisha onywa na mataifa mengine, Barricks sii wageni ktk biashara hii na wamezungumzwa sana miaka ya 80 kwa uporaji wao nchi za South America hasa huko Peru. Sisi tumeingizwa mkenge na watawala wetu, Barricks ni wafanya biashara ambao siku zote kulalia ni part of business... tusifikirie hata siku moja kuwa wawekeshaji ni charity foundation.
Tukirudi ktk swala la Andrew Young umesema kanunua Mount Meru, sasa ulitaka anunue nani? na una uhakika gani kuwa fedha yake yote itakwenda Marekani hata kama hajaanza hiyo biashara. Je, angekuwa Bill gates kungekuwa na tofauti ktk uendeshaji wa Mount Meru na maslahi yake? zaidi ya hapo Mount Meru haichukuliki, ipo Tanzania kama zilivyo hotel nyinginezo... mbona sijasikia mtu akizungumzia Kempiski au Moven Pick ama kwa sababu hizi ni za waarabu, besides ikiwa tunahitaji fedha za Utalii nchini je, zinapatikana kwa njia zipi na ni sheria gani ambazo zimewekwa kwa wawekeshaji wote toka nje?...Ikiwa ni kodi atalipa kama wengine na sidhani kama Andrew Young atakuwa akikiuka sheria kwa sababu yeye ni mweusi ila kama kuna mapungufu basi makosa ni yetu sisi ktk kuweka sheria za uwekeshaji ktk mahotel. Tusijenge sababu na sheria kwa sababu tu mwekeshaji ni Andrew Young. Binafsi ninatazama uwekeshgaji huu kama ni blessing kwa sababu kwa mara ya kwanza Mu AMERICA mweusi ameweza kuwekesha Tanzania na kuna uwezekano mkubwa wa watalii wenye asili ya kiafrika kutembelea Tanzania.
Sasa kama tuna akili na Ujanja zaidi ni kuboresha zile sehemu za Utumwa, tujenge historia ya msafara wa utumwa toka Kigoma,Tabora hadi masoko ya Bagamoyo na Zanzibar. Kisha tuweke siku maalum ya kukumbuka utumwa huo na kuanzisha jahazi litakalo weza beba watu toka Bagamoyo hadi Zanzibar kupitia mahandaki na njia zile walizouzwa babu zetu. Waamerika weusi wataifanya siku hiyo kuwa EXODUS kwao na utaona jinsi watakavyo miminika kila mwaka... haya ni mawazo yangu tu nikitumia hoja yako moja ya Andrew Young!
Huyu Andrew Young anaweza kuvuta zake lakini nasi tuwe tayari kubuni biashara ktk huo mtililiko wa trickle down. Ajira moja huzaa nyingine na nyingine badala ya sisi kutegemea Mount Meru kubadilisha uchumi wa Tanzania.
 
Mkandara,
Nakuomba usome kitabu cha Kwame Nkrumah "Neocolonialism, the last stage of imperialism." Andrew Young kishaacha kazi serikalini na sasa ni kutafuta tu ulaji. Haiamkiniki kuwa George Shultz ndiye hero wake. Martin Luther King Jr. anageuka mara tisini huko kaburini mwake. Hatutaki Afrika ambayo itaendeshwa kwa amri za corporate America. Tunahitaji wawekezaji, ndiyo, lakini si wawekezaji ambao watatuacha na magofu kama ilivyo hivi sasa na Barrick. Mimi naunga mkono mkutano wa Sullivan kufanyika Tanzania, lakini sikubaliani na uwekezaji ambao kila faida ya raslimali zitaishia nje. Mount Meru imeshachukuliwa na kampuni ya Andrew Young. Guess what, most of the guests wataishia pale, fedha za faida zikirudishwa Marekani na sisi tukibaki na tips peke yake.
Capitalism siri yake ni accumulation of capital. Katika mchezo huu sisi tunachezewa kweli kweli!

Phew, huyu ndie Jasusi wa 2008, au siku zote yuko hivi?

Usidanganywe na rangi, wakati mwingine utatamani kushirikiana na mzungu zaidi kuliko hawa weusi wenzetu. Usione akina Oprah na wengineo kujua Afrika ya kusini kuliko kwingineko kote Afrika ukafikiri hawajui kuwa kuna nchi zingine za weusi kama wao!
 
Kalamu,
maneno yako sii mageni kwani ndio maisha ninayo ishi, Watu weusi hatupendani nahasa sisi Wadanganyika maanake tumeshindwa hata kusimamisha jumuiya moja nchi za nje! nambie nchi yenye hata Jumuiya moja ambayo Watanzania wote wanaikubali bila kuwepo na tuhuma kama hizi!... na siku zote wapinzani husema:- Usidanganywe na rangi, wakati mwingine utatamani kushirikiana na mzungu zaidi kuliko hawa weusi wenzetu...
 
Kalamu,
maneno yako sii mageni kwani ndio maisha ninayo ishi, Watu weusi hatupendani nahasa sisi Wadanganyika maanake tumeshindwa hata kusimamisha jumuiya moja nchi za nje! nambie nchi yenye hata Jumuiya moja ambayo Watanzania wote wanaikubali bila kuwepo na tuhuma kama hizi!... na siku zote wapinzani husema:- Usidanganywe na rangi, wakati mwingine utatamani kushirikiana na mzungu zaidi kuliko hawa weusi wenzetu...

Mkandara:
Zamani, miaka ya 80s nilikuwa ninafarijika sana kukutana na mweusi mwenzangu nilipo kuwa huko majuu, na hasa hasa awe ni mTanzania mwenzangu. Siku hizi ni taabu sana hata kujitambulisha. Ni bahati mbaya sana, sijui ni kwa nini!
 
Huko tunakokwenda, tutaitwa na historia na tutaitwa na kizazi kijacho kuchukua msimamo. Katika kuchukua msimamo huo kuna kati yetu ambayo tutaitwa kulipa gharama kubwa na labda hata gharama kuu zaidi ili kuwapa watoto na watoto wa watoto wetu nafasi ya kufanikiwa. Kama wale wa kabla yetu walipochukua msimamo na kutaka tuwe huru ili tuwe na nafasi ya kujiamulia mambo yetu vivyo hivyo na sisi tutaitwa tuchukue msimamo ili hatimaye tujiamulie mambo yetu. Katika kufanya hivyo tutaitwa kuwapinga wakoloni weupe na weusi na kama dhamira kali tutawabumunda na kuwashinda kidemokrasia na kuwapitia kipigo kama kile cha Mfalme Kima alipombumunda Shetani Mfupa Mweupe!
 
LOooo! Jamani, mwaka huu 2007 unakwisha kwa maajabu, au tuseme 2008 inakuja na mambo makubwa.
Ni nani anayeweza kunipa tafsiri ya ujumbe mzito alioutoa hapo chini Mzee Mkjj?
Au ni 'Roho Mtakatifu'(kwa wanaoamini), kashuka, au yupo tayari kushuka 2008?
 
Kalamu,
Wala sikulaumu kwa sababu ndivyo tulivyolelewa..sisi Wakerewe ndio kabisaaa, tutakutafutia hata mganga (kamati ya ufundi) tukuondoe mweusi unayeendelea. Kusema kweli tulijazwa ujinga na mzungu toka utumwa kiasi kwamba Manyapala weusi wakati wa utumwa walikuwa na roho mbaya kuliko mzungu kwa sababu huyu nyapala hakujua thamani, afya na uzima wa mtumwa ndio muhimu zaidi . He had no idea kabisa kuwa future yake na yule mtumwa ni utumwa ktk mashamba ya mzungu.

Taratibu tutakuja jenga umoja hasa ktk vijiwe kama hivi na labda itafikia siku ukimwona mwafrika mwenzako utampa maji na kitanda apumzike badala ya kumwogopa...
Nimeona huko nyuma kuna watu wamesema sana kuhusu Adrew Young na Barricks labda niweke tena kipande hiki cha historia ya kampuni hii ili kesho tusije danganywa tena. Kisha Sutton haikuwa na wala sii kampuni ya Sinclair...
hata hivyo tuendelee na mada.

Historia ya Barricks:-
Barricks's Hunt for Gold worldwide – or: yesterday we hunted in America, today and tomorrow everywhere. Casting: Peter Munk, (Boss of Barrick, Ex-Bankrupt-Fellow and Ex-Inside Trader), Adnan Khashoggi, (Arms Dealer and First Class Crook), G.H.W. Bush (Ex US President), Karl Otto Poehl, (Ex-German Federal Reserve Bank President), Brian Mulroney (Ex Canadian Prime Minister)​
The continuously rising price of Gold, now above 540 US Dollars per ounce, has driven mine companies to search for Gold.

The "yellow metal" is predominantly found in the Southern Hemisphere,
and often the production of gold is accompanied by destruction of the environment, because it needs Cyanide, a very toxic substance, two teaspoons of a 2% solution kill a man. An overflow of cyanide containing fluid from a gold mine in Romania a couple of years ago led to massive pollution of a river, killing all the fish, reminding us to the perils of gold production..

In focus are now two gold mines of a Canadian mining company by the name of Barrick, one in Chile, Pascua Lama, and the other one in Australia, close to Lake Cowal.

Lets first of all have a look at the company and it's actors.

Barrick Gold was founded and largely financed by Adnan Khashoggi in conjunction with a Peter Munk in 1983 in Toronto/Canada.
Khashoggi has quite a bit of luggage to carry.
He is well known as an international arms dealer, however let's focus also on his financial deals, or his crooking, to be precise.
Apart from being involved in the Iran Contra Affair, in which weapons were sold to Iran via Israel by the Pentagon and the proceeds were used to finance a right wing terror group in Nicaragua, called the Contras, Khashoggi was deeply involved in the Bank of Credit an Commerce International (BCCI), a massive washing machine for dirty Dollars from shady arms deals and drug cartels.
The Medellin drug cartel of Columbia was a most welcome client of that bank.
The bank was forcibly closed in 1992.
No problem for Khashoggi, he knew other crooks to work with.

Next came Rakesh Saxena, adviser to the Bangkok Bank of Commerce, together with the CEO Krikiat Jalichandra, who was sentenced to 30 year in prison one year ago for defrauding the bank to the tune of 2,2 billion US Dollars and thus causing the Asian Banking Crisis in 1997.

Khashoggi got from the duo Jalichandra/Saxena a non repayable loan amounting to 140 million US Dollars in 1994. He is therefore now wanted by the Thai authorities for fraud.

And he continued to work with Saxena, who fled from Thailand to Canada just in time.
They bought in 2000 the General Commerce Bank in Vienna/Austria, together with the international stock fraudster Amador Pastrana and the convicted criminals Regis Possino, Raoul Berthamieu, and Sherman Mazur, and turned into a center of international stock fraud, the fraud amounting, according to press reports, to one billion US Dollar.

The bank was forcibly closed in 2001.

One billion in one year.

The other cofounder and now boss is Peter Munk. He also has a bit of luggage to carry.
He owned a stereo equipment producing company in Nova Scotia/Canada, supported with public funds, and at the brink of bankruptsy he quickly sold the shares before they plunged, stock fraud or insider traiding is another word for that.

Doesn't matter, what is more divine, than to forgive and despite this scandal and through the connections of his partner in bankruptsy he rose from the ashes – in the aristocratic circles of London and then in Australia and finally came back home to Canada with Adnan Khashoggi, two dubious birds of the same feather albeit different faith, founding Barrick Gold.

The company was rumbling along until G.H.W. Bush, the senior, came for help and for less than 10.000 Dollars they bought from the state a piece of land, whose underground had gold worth 10 billion US Dollars, later on this was called by US President Bill Clinton's Interior Secretary Babbit "the biggest gold heist since the days of Butch Cassidy". And with this "Gold Heist" Barrick shot from insignificance to a global player.

After Bush lost the election to Bill Clinton in 1992, he became a direct player on board of Barrick, a new home away from home and well paid.
With him Karl-Otto Poehl, former President of the German Federal Reserve Bank and the former Canadian Prime Minister Brian Mulroney.

Now the ship Barrick with its prominent officers could set sail and travel to it's next destination, Africa, Zaire to be precise. This country, now called Democratic Republic of Congo, was at the brink of civil war-doesn't matter, better prices for the mineral rights especially when you negotiate with two parties, old robber Mobuto Sese Seko and new stealing hand, Laurent Kabila.
However the civil war lasted too long, so let's go for the next destination, Tanzania.
The company Sutton, at this time advised and later on owned by Barrick was owning a mine by the name of Bulyanhuly.
A good thing to exploit, if there were not thousands of small scale miners with their families, who were digging already for gold.
Sutton chased them away with Bulldozers and police, allegedly 50 miners died during this clearing operation.

Barrick does not want to hear the allegation, because, according to them, they are untrue. May be it was a festival?

However investigative journalist Greg Palast in conjunction with the human rights lawyer Tundu Lissu in Dar-es-Salaam brought a report in the British newspaper "Observer" and called it nothing else than a scandal..

Barrick sued, Greg Palast and Lissu insisted and a delegation of NGO's, visiting Tanzania in 2002 had some indications, that the story was in fact true, however their work was not actively supported by the Government, to say the least.

With Bush's and Mulroney's support, Barrick got a huge World Bank loan, to develop the mine, a friend in need, even when on the payroll, is a friend indeed.

Now Barrick is active in Australia and Chile, in both countries facing massive resistance, bigger than the poor miners in Tanzania could build up.

In Chile, Barrick wants to dig for gold high up in the Andes Mountains and remove glaciers there, that are vital for the water supply of a community in the desert.

And in Australia Lake Gowal is habitat for endangered species.

I looks, as if Barricks is facing stiff resistance globally now.


Dr. Alexander von Paleske
Head, Department of Oncology
Princess Marina Hospital
Gaborone/Botswana/Africa
Ex-Barrister-at-Law, High Court Frankfurt.
 
Mkandara, asante.
The way I see it, its our own mess up. Rather, a mess up of a few people for their own interests. But its gonna haunt our nation for a longtime. I truly believe that.
Daaaymmmn.
 
Bob Mkandara,

Stage tuliyonayo Watanzania sasa hivi ni kutembea juu ya maganda ya mayai! I agree there is a need to reach out to Wanugu! Lakini si kuwa tunamlaumu AY au kumuita Fisadi/Kuwadi wa Ubepari! Bali ni kukosa kwetu imani na viongozi wetu na yeye AY kuwa Mnene kwenye shirika ambalo linatuhumiwa kutuhujumu kwa kutumia udhaifu wa sheria zetu na uroho wa viongozi wetu.
 
..ulikuwa na bahati,siku nyingine haitokuwa ya bahati!kuwa makini zaidi na hasira zako!kama ulivyoshauriwa tafuta sehemu muafaka ya kuzitolea!

..nashauri ufanye mazoezi ya viungo,kucheza mpira,kulima kama una shamba,kumwagilia mimea kama unayo au kupanda ngazi za ofisini badala ya lift,hasa pale unapokasirika.usije siku ukuamkwida bosi wako,sidhani kama kibarua kitakuwepo baada ya hilo!

Hi Mfuatiliaji/Dar si lamu,wazee samahanini.. Nilichelewa kuona tatizo hilo. Si tatizo dogo hilo hata kidigo!!!!!!. Tukiendelea hivyo ni kuwa kweli hatutafikia "ukombozi wa taifa letu" kama tunavyotaka. Utafiti wa kileo unatuonyesha kuwa kazi ya "adui" ni kumfanya mshindani wake azalishe hasira, chuki, na hisia hasi nyingine(negative emotions)kwani NDIO NJIA PEKEE YA KUMPATIA USHINDI. PLS PLS FUATILIA KWA UNDANI USHAURI WA UNDANI WA HISIA HASI NA JINSI UNAVYOWEZA KUWA MTUMWA WA FIKRA MBELE YA ADUI YAKO. Niseme wazi kuwa maadui wa Tanzania wanatpatia hapo.Wantutisha tunatishika, Tunawachukia, tunawaogopa, wantutishia na kutufanya tuwe vijitumwa vyao..so wana JF pls pls tupambane kwa dhati kabisa but tunye mapambano kisanyansi. Tupambane kwa dhati kabisa BILA UZALISHAJI WA HISIA HASI. Soma makala "Afya ya fikra kwa mtanzania mpya" www.duniahai.com au "utumwa wa fikra na uporwaji wa rasilimali za taifa". Mimi binafsi siamini tutaufikia ukombozi bila ya kuweza kumudu our negative emotions...Lazima kujenga EI yaani emotion intelligence zaidi ya IQ pekee. Pls Tusikubali Kuingizwakwnye MTEGO! Ukimuogopa mtu..utamtumikia milele. Ukiingizwa kwenye mkondo wa Hasira na Adui..utamtumkia milele!! Ni sanyansi..na Ni chombo kabisa Kinachotumiwa na Maadui Kupatia ushindi. soma kisa cha stockholm..kwenye Mtandao niliokupa..Stockholm syndrome ni kisa cha kweli...Kuna zoezi la kufanya hapo kwa ajili ya kupevuka kihisia tayari kwa ushindi wa kishindo kwa taifa letu..All the best Sir!!!
 
Wandugu hapa ndipo anapotakiwa kijana wa kitanzania kuamka na kuamua kukomboa taifa hili.

Kuhusu watu kufukiwa kule Bulyanhulu ,ni kweli kabisan na kwa wale wanaomlaumu Lissu na Mrema tunawaonea kwani hawajawa waoga ila serikali ilifungua kesi mahakama ya kisutu tangu mwaka 1998 hadi leo na kesi hioyo haijawahi kusikilizwa ila kila kukicha inatajwa tuu.

Mtakumbuka kuwa Lissu amekataa kwenda hapao mahakamani na mahakama yenyewe iliwahi kutoa hati ya Lissu kukamatwa kwa kosa la kuidharau mahakama mwezi september mwaka huu na hadi leo amri hiyo haijatekelezwa na mahakama wala polisi.

Huu ni uoga wa serikali kwani wanajua kuwa kitendo cha kuendelea na kesi kitaufanya ukweli kuwekwa hadaharani na serikli na hao wakina AY wao kuumbuka tena mbele ya mahakama , mimi binafsi nimewahi kuona mikanda na CD zinazoonyesha jinsi watanzania walivyofukiwa na wazazi wao wakilalamika juu ya hatua hiyo.

Ushauru wangu mwakanai wakati wanakuja hao wakina AY hapa Arusha kuna haja ya sisis watanzania kufanya kampeni ya kuwapinga hawa jamaa kwani ni wauaji na wabakaji wa uchumi wetu.

Naomba tuanzishe harakati hizo na ziwe za kimataifa ili huyu AY JK waweze kuqwekwa hadharani na tumwambie huyu AY kuwa hatuwataki hapa kwetu laa sivyo tunaumizwa.....
 
Rev. Kishoka,

Sasa limekuwa kosa la AY kufanya kazi na kampuni ambayo sisi wenyewe tumeikaribisha na kuingia nayo mkataba?... mjomba hii ni sawa na ndugu zako kunambia mimi nisiwasiliane na mkeo (shemeji yetu) ati kwa sababu anakuchuna hali wewe mwenyewe umeridhika kuwa ATM....naweza kukupoteza hata wewe ktk urafiki wetu hali ndugu zako nimewajua kupitia wewe.
Ebu nambie kweli unafikiri AY anayo nguvu yoyote akiwa ktk advisory board ya Barricks? ni kipi anachoweza kusema kikachukuliwa na Barricks kuwa ni ushauri mzuri ktk biashara yao. Na unategemea kweli yeye mwenyewe atoe ushauri unaopingana na mkataba ama sheria za kodi tulizozitunga sisi wenyewe!... jamani jamani kwa mapenzi gani na sidhani kama malalamiko ya wananchi yanamfikia! pengine hii ndiyo nafasi na wakati muafaka kwetu kuzifikisha salamu zetu kwake. Tusianze kulaumu mtu tukamjaza vyeo na hisa ambazo hana hata kidogo ili mradi ni mweusi tunatafuta penyo mahala pa kutoea.
If anyone to blame ni rais wetu Mkapa kama tunavyoweka lawama zetu kwa JK kuhusiana na Karamagi. Kama nilivyoonyesha hapo juu AY hana uwekeshaji ndani ya Barricks wala hayupo ktk board of directors ila ni mshauri ktk maswala ambayo hakuna kati yetu anayefahamu, na yupo ktk advisory board ya kampuni nyingi kiasi kwamba inaonyesha sii mwajiriwa wa Barricks - fulltime.
Mti wa Mafisadi upo wazi kabisa na umeota ndani nyumbani kwetu...Mkapa alikuwa rais waziri wake wa madini alikuwa JK, leo hii JK ni rais na Karamagi ni waziri wake wa madini. Kama kuna ukweli wowote unaotafutwa nadhani shina lipo wazi kabisa machoni kwetu. Hawa jamaa wanakuja bila kufahamu matatizo yetu na ndio maana wanatoa ma zawadi kemkem kutokana na taarifa wanazozipata toka kwa wazungu hao kina WB na IMF..hatuna mawasiliano ya karibu na wanugu na pengine half ya watakao hudhulia mkutano hawafahamu kinachoendelea.

Na imekuwaje issue ya mafisadi mbona sijasikia tena yakizungumziwa ama ndio yameisha tiwa kaburini na hitma ishasomwa!
 
Mkandara, nimesoma threads zako ingawa umeandika mengi ever since nilipotembelea JF. Mimi ndiyo nilianza kazi ya kufanya utafiti kuhusu AY na Sullivan and I want to tell you why ili usiendelee kudhani kwamba eti 'Waafrika hatupendani'
1. Nyerere alishasema mtu akikusifia sana mwogope! In 1 year time, JK amepewa tuzo 3 'tofauti' lakini ukiangalia behind this all is AY! Now that stinks to high heaven! So I wanted to know what motivates him.
2. Sullivan summit imepewa uzito mkubwa sana nchini, na kuonekana kama italeta wawekezaji wengi na wazito. Na hii itatukomboa. Umeongelea kirefu umuhimu wa hawa wawekezaji etc. Nilitaka kujua what is Sullivan summit. Nimepata information that it is a front for GWI llc. It's a way for AY to make his clients meet decision makers. So let us not delude ourselves! Sullivan summit naandaliwa na GWI na primary goal of GWI is to protect the interest of its clients (NOT Tanzania).
3. AY kama mtu ambaye ana -pop up in many of the activities and happenings in Tanzania and Tanzania- related in US, ni muhimu tujue, je ana msimamo gani katika jamii yake? Hii ndiyo ilikuwa lengo lingine la uchunguzi wangu. Imeonekana kuwa he is an economic hitman together with his 'pals' - Jeter and Carlton Masters.

Ingawa bado sijamaliza lakini naomba nijaribu ku-share what I have seen so far:
1. Kusema kwamba eti hatujafaidika na wazungu so mweusi mwenzetu... is totally off point. Ay is primarily American and only then is he African. In fact he is Black American. So let us not romanticize the issue. I found more information jinsi alivyohusika na dealings za Wal-Mart katika kujaribu kutetea Wal-Mart ilipowafukuza na kuwaonea wafanyakazi wao! Soma hapa
In February, 2006 Young accepted a position as chairman of Working Families for Wal-Mart, a grass-roots organization sponsored by the corporate giant as a public response to widespread criticism that many of the company's American employees and their children are on public assistance, that the company uses child labor, that the company discriminates against female and African-American employees, and that workers manufacturing Wal-Mart products are subjected to abusive conditions and sub-poverty wages.
In an interview in 2006 a Los Angeles Sentinel correspondent asked Young whether he worried that Wal-Mart causes smaller, mom-and-pop stores to close. He replied with comments that were criticized as racist:
“ Well, I think they should; they ran the 'mom and pop' stores out of my neighborhood, ... But you see, those are the people who have been overcharging us selling us stale bread and bad meat and wilted vegetables. And they sold out and moved to Florida. I think they've ripped off our communities enough. First it was Jews, then it was Koreans, and now it's Arabs; very few black people own these stores.
”
Following the wide-spread publication of these comments, Young announced on August 17, 2006 that he had ended his involvement with Working Families for Wal-Mart.[1]
This is relevant because there should be no illusions. This man doesn't care even about his own people. He wanted to use the race card but it was too lame. Yeye alikuwa anatetea WalMart! Unafikiri atatutetea eti sisi ni waafrika wenzake etc! It was a looong time ago when he walked with MLK! He has turned ever since!

2. Corporate America is good for us Tanzania. Mimi naamini kabisa in free market economy, and I agree that Tanzania tunahitaji uwekezaji. But I want you to understand that Americans are shrewd (I specialized in American studies - their history, culture and politics, so I learnt a few things about their psyche)They are the first free marketers! And they WILL take advantage of us. Why are they now pushing into Tanzania? Because they know that we have a weak president. THey are aware that a few awards have already dazzled him, he is bought now! He does not attend the EU meeting but rushes to US to get a third rate award! And check how smart they are! They gave awards to Condi Rice and Hilary Clinton to give it credibility, but in Africa who gets the award? Obasanjo - the bastion of democracy LOL! Wanatuchezea akili. Americans have a great smile and pat you on the back but don't give a dam. Kama mtu anaweza kupost hapa picha zilizowekwa kwenye magazeti leo ya JK, AY na Jesse Jackson nitafurahi. Naomba nichambue body language iliyopo. JK is leaning in, and touching a button on his touch. Jesse Kackson is rod straight, looking out of the photo not making eye contact, AY in the middle has a hand on Kikwete's elbow(?) but is looking in the other direction. They DON"T care! And JK looks overwhelmed, eager to please! They have him where they want.

Mkandara usinione naongea tu, these are serious issues that appears to be uninteresting but every political or business encounter IS about psychology!

3. Investment in Tanzania - wewe ndiyo uliongea about India and China. For your information both countries walipata akina GE, Bill gates etc BAADA ya wao kujiendeleza. We need skilled, educated workforce. We need empowered Tanzanian private sectors ndipo tunaweza kuwaita hawa multinationals. Sasa hivi you have TATA in India,unafikiri walikua vipi? By inviting Mercedes etc? No, India protected its market (and still is akina Wal-Mart hawawezi kuingia supermarket chains are Indian) and once its mature to open it up. Tumefungua our market wameingia and they raped us! You know why because as Nyerere said free market economy in Tanzania is like putting a heavy weight (multinationals) in the ring with a feather weight (Tanzania).
Problem is we don't have visionaries as leaders. Tunakimbia tu. IMF and World Bank are pushing the agenda, you think who are they protecting? Bretton Woods conference was about America and Europe NEVER about Africa and Asia! once we wake up and smell the coffee tutafika mbali.

Asanteni kwa kukusoma yote niliyoyaandika and excuse spelling mistakes! Naomba kuwahakikishia naendelea kufanya uchunguzi. Na yote hayo ni kwa kuwa nina upendo mkubwa sana na nchi yangu!
 
Mkandara usitwist Maneno...uchambuzi wa Hapa ulikuwa unakwenda vema sana kuhusu mauhusiano mbalimbali wa namna hii Tanzania inavyotumika. Ukisoma vema maelezo watu hawana USongo na mwekezaji kuwa Mnegro au whatever...Hata mwekezaji akiwa Mbongo lkn FISADI anawekwa wazi...angalia JF ilivyomuanika BWM juu ya kiwira...ni local investor lkn watu wamehoji...Hatuwezi kukaa kimya eti aliwekeza Mnegro...Mbona watu wamesema humu kwa projects za Waarabu hasa hizo za mahoteli ambazo wewe unadai hawajasema....au umevaa miwani ya MBAO?..HAKUNA Biashara alioinvest MWARABU ambayo ilikosa shutuma...Zantel walikaa ZNZ 5 hawakuruhusiwa Bara...untill late 200x, Hoteli za Kilimanjaro vs Mengi investor....Kule arusha ktk wanyama....ohh LOliondo..).
Pls mkandara usipindishe mada au maneno acha tafiti ziendelee
Udhaifu wa wabongo nakukubalia kila nchi lkn hilo lisifanye Juhudi Mpya za KUWAAMSHA NA WIZI UNAOENDELEA BONGO USISEMWE...
 
Susuviru:
I like your number 3 in the above posting. Uwekezaji tunaoupata kwa wakati huu kwa sehemu kubwa hauna manufaa sana. Hakuna 'technology transfer' yoyote ya maana inayotokea. Mifano ya India na China uliyoitoa inatupatia mwanga mzuri sana.

I should say, I am convinced by your arguments here that you know what you're talking about. Heko!
 
Susuviri,
Nakuelewa sana kuwa umejaribu kutafuta ukweli kuhusu Sullivan na kuwakilisha hoja zako, nanyi pia muwe radhi kupokea hoja zetu kwani ukweli wenu hauwezi kabisa kuwa ndio final... nachojaribu kusema mimi kila mara hujribu kutoa pendekezo ama solution badala ya kulaumu tuu kama jamaa wengi wanavyofanya. Sullivan sio AY wala AY sio Sullivan kwani kuamini hivyo ni sawa na kuamini kwamba Nyerere foundation itahukumiwa kwa kumtazama Salim A Salim.
Pili, hayo maelezo yanayohusiana na AY huko Wal mart mbona nachokiona mimi ni kuwa AY ametetea watu weusi na kawakandya Walmart ama kiingereza changu hakikwenda shule?...

He said:- Well, I think they should; they ran the 'mom and pop' stores out of my neighborhood, ... But you see, those are the people who have been overcharging us selling us stale bread and bad meat and wilted vegetables. And they sold out and moved to Florida. I think they've ripped off our communities enough. First it was Jews, then it was Koreans, and now it's Arabs; very few black people own these stores"

Hapa kawatetea vipi Walmart against blacks?
Labda unamsikia tu huyu mzee jinsi anavyochukia Ubepari na utumwa wa mawazo toka enzi za Dr. Martin Luther King. He was the bridge connection between blacks na white in US wakati wake na naweza kusema ndiye mweusi pekee aliyeweza shika nafasi kubwa wakati mbaya wa siasa za rangi nchini humo na matatizo ya Uhuru nchi za kiafrika yalikuwa ktk kilele chake.
Kisha swala la kusema AY ni Black American una maana gani kwani lini amekuwa mwafrika?....jamani tunachozungumza hapa ni uhusiano kati yao na sisi.. Hata angekuwa mwafrika bado ungesema ni Mganda ama Mrwanda kama tunavyowakataa wengine. Kisha usijaribu kabisa kumweka chini AY ktk uongozi wake kwani kayafanya mengi against his own country kwa sababu ya Uhuru wa nchi za kiafriKa na hasa South Africa na Rhodesia. Ni Andrew Young aliyeweza kuboresha mahusiano kati ya Marekani na nchi za kiafrica na yawezekana kuwa kiongozi pekee mweusi aliyewahi kuheshimiwa zaidi barani Africa kuliko hata Rev. Sullivan mwenyewe.
Hii ni ndoto ya Sullivan na wengi tunaikubali isipokuwa baadhi ya watu ambao wanafahamu ujio wa mawazo ya huyu mtukufu Rev. Mungu amlaze mahala pema peponi - ni mwisho wa mzungu kutawala uchumi wa Africa.

Chuma,
Sijapindisha kitu hapa ila natoa mawazo yangu ambayo yanapingana na hoja zenu kwa hiyo ni bora kama una ukweli nje ya hoja zangu anika kuliko kutoa dhana za kufikiria kuwa mnegro ni tapeli hata kama hujawahi ku deal naye kutokana na maneno yaliyojengwa na wazungu wenye chuki na mahodari wa kutenganisha ili wapate kuhodhi, hii ni baada ya kuona kuwa maslahi yao yapo hatarini. Hao Barricks wenyewe nimekupeni picha yao haya nambie kuna zuri linaloonekana kutoka kwao?...mbona bado tumewakumbatia ama kwa sababu wao ni wazungu watawala wenye ma Phd akina Bush.
Tembelea http://www.thesullivanfoundation.org/summit/, soma malengo yao na kitu gani wanachojaribu kuuza kisha tujenge ngome zetu kulinda maslahi yetu laa sivyo tunachojaribu kujenga hapa ni chuki tupu. Mbona JK na Lowassa kila wanapotembelea nchi za nje hukutana na foundation mbalimbali za wazungu ambazo pia ni matapeli lakini msiwaone wao isipokuwa hawa weusi.
Nitarudia kusema matapeli tunao wenyewe ndani ya nchi tumeshindwa kunyoosha hata kidole leo kwa umalaya wetu tunarukia foundation hii kwa sababu tu ni watu weusi na hawana fedha!...Tuko radhi kulala na Bill Gates mwenye ukimwi kuliko AY asokuwa na kitu ila mapenzi yake kwetu.
Damn! ama kweli tuko mbali sana kufikia uhuru wa kifikra!
 
Mkandara,
Hatuwezi kuwalaumu viongozi wetu peke yao kwa kutuingiza katika mikataba hii feki bila kuwamulika "wakubwa" walioingia nao katika mikataba hiyo. Hatuwezi kujilaumu kwa udhalimu na unyonyaji unaofanywa na Barrick bila kuwaangalia "who is who" katika kampuni hizo. Ndiyo maana tunawataja akina AY na kwa nini wanammwagia misifa JK.
That is what this debate is all about. Tuzungumzie ujinga wetu lakini pia tuwajue wajanja na jinsi wanavyotutumia.
 
Back
Top Bottom