Ground station sio kama bomba la maji kwamba ukiweka maji tu yanapita na kumiminika..
Ground station ina computers na antenna...
Antenna za ground station starlink...
Ground station ina computers, softwares , modems na routers zinazobadili mawimbi ya satellite kuwa mawimbi ya kawaida ya internet ambayo itakuwa connected na fiber... hio process yote inatumia resources , muda na power ku process...
Starlink ground station yake moja huwa ina hizo parabolic dish 9 huku nane zikiwa zinatumika na moja ikitumika kama backup/reserve...
Kila antenna moja ina kikomo chake cha bandwidth takribani 20Gbps...
Lakini kuna baadhi ya ground station zinakwenda hadi 1Tbps...
Twende kwenye math, tufanye tu ground station ya Kenya ina uwezo wa ku process 1 Tbps ambayo ni sawa na 1,000,000 Mbps...
Haya tufanye kila mteja Kenya awe na speed ya internet 50 Mbps.. tugawe hapo..
1,000,000,000 Mbps/50 Mbps = 20,000 User terminals..
Ground station moja yenye uwezo mkubwa kabisa wa ku process 1 Tbps inaweza hudumia terminals 20,000 kwa wakati mmoja...
Sasa unachobisha hapo ni kitu gani ndugu?
Kenya watumiaji wamefika 19,000.. kwa rough estimations unaona kabisa starlink wapo sahihi ... na hesabu haidanganyi... kumbuka pia hio ni math katika nadharia...(theoretical maximum)
Lakini tukienda kiuhalisia kuna factors ambazo zitapelekea 1 Tbps ground station kuhudumia watu chini ya 20,000..
Pia kumbuka Starlink huweka mipaka kwa idadi ya watumiaji wanaoweza kuunganishwa ili kudhibiti latency na kuhakikisha huduma inaendelea kuwa ya haraka...