Boss gaming hata 1mbps ni luxury unless hujui online gaming inafanya vipi kazi.
Internet ya 5mbps latency 1ms na Internet ya 1gbps latency 50ms zikikutana kwenye game na skills sawa basi ujue 1gbps anakalishwa, nakwambia hivi kama competitive gamer ambaye maisha yangu yote na chase good ping, wiki nzima unaweza usitumie hata mb 100 na unacheza games masaa kwa siku. Games zinatumia data kidogo na zinataka ping nzuri.
Video za watoto wanazo angalia 720p-1080p hizo si 2mbps tu?
Mfano hii Video ya Neo ya watoto unaona hapo mb zake na resolution
View attachment 3358231
Video ya lisaa limoja
573MB kwa 1080p
280MB kwa 720P
Do simple math
573 x 8 = 4584 gawanya kwa 3600 ni 1.2mbps
280 x 8 = 2240 gawanya kwa 3600 ni 0.6mbps
Kwa hizo bandwidth labda uwe na watoto 10-15 ndio wakuzibie Bandwidth.
Na Games la GB 50 unadownload mangapi kwa mwezi? Unless una biashara ya library unaweza usidownload game miezi, maana game ni kitu unadownload kisha unacheza kwa muda mrefu, kama ni Fifa linatoka moja kila mwaka, Gta linatoka baada ya miaka etc.
Pia starlink
1. Huruhusiwi kushare wakijua wanaku suspend
2. Ina throttle ya 1TB mnavyokua wengi ndio jinsi mnamaliza 1TB mapema na ndio jinsi wana throttle speed.