41% ya Wanawake hawazungumzi na Wamama wakwe zao

"Kicheche kama wema malay.a asiye na hadabu kaidatisha tandale mpaka mama(Diamond) anaenda club"--Tabla ft Stive Rn'B.
 
hayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa umetokea wapi tena huku si uliniambia unakwenda kucheki muvi lol ,ila jana hujaniambi akelele za nini jana hivo

Nimeghairi kwenda muvi, sijui niko addicted na JF?!
Sasa nivea usiku wote huo ulikuja chumbani kwa mi kakaako ulikuwa unatafuta nini?! Au .....
 
Last edited by a moderator:
Nimeghairi kwenda muvi, sijui niko addicted na JF?!
Sasa nivea usiku wote huo ulikuja chumbani kwa mi kakaako ulikuwa unatafuta nini?! Au .....
si kelele unajua damu nzito kuliko maji nikajua unatukanwa mwenzangu nikugombelezee lol niliaibika niajeee
 
hapo umenena mkuu mamasboy kaa nao mbali kabisa wanakera sana hao umbwa.anaweza kukutukana mbele ya mama yake akidai eti wewe atapatana na wewe chumbani bitch

Kwa hiyo Mama's boy hawapaswi kuoa?

Watoto wa pekee kwa mama zao hawana haki ya kupata Mke kisa mama zao wanawapenda sana.

But patamu panakuja wapi wanawake wa siku hizi mnaolewa kwa vigezo as mume awe na shule nzuri, kazi ya kueleweka, atoke maisha ya getini as familia bora kwao,, na wengi wenye hivyo vigezo ni mama's boy... Hapo ndo utamu unapokolea.. Mamas boy wanaboa lakini ndo wenye huwezo wa kumudu majukumu na mnavyopenda harusi za kutokelezea mnachagua mume kwa kuangalia financial status mjiandae sana kugombana na mama wakwe zenu as Mama's boy ndo wana sifa mnazotaka japokuwa hapa mnajifanya kupinga..

Nimeshaona mengi tu as hao watoto wa mama wanavyopendwa na wadada wakati wanajulikana kabisa Mama zao ndo roho yao.. Hali ya maisha imebadilisha akili za wadada as kila mmoja anataka aolewe kwenye maisha mazuri, watoto wake wasome shule nzuri na hata yeye avae vizuri watoto wa mama ndo wana access ya hivyo vitu...
 
japokuwa umegoma kufanya nilichokuomba ufanye ngoja tu nichangie!
si unajua mi na we ni kama uji na mgonjwa vile!
unajua hili saga kati la mama na mkamwana wake lina sababu nyingi sana
nyingi mojawapo ikiwemo hiyo ya "sisi enzi zetu tulikuwa hatufanyi hivi"
1.UTEGEMEZI
iwapo binti ameolewa na mwanaume ambaye yeye ndo kila kitu kwa familia yake mara nyingi akioa mama mkwe lazima zisiive na mkamwana since anahisi yale yote mtoto wake alikuwa anafanya kwake hayatafanyika na pengine hayafanyiki kweli since sasa mwanaume majukumu yameongezeka na he has his own family to take care of so obvious hii likkitoke kina mama wengi hukimbilia kulaumu wake za watoto wao kuwa ndo wanabana kumbe wakati mwingine maisah tu maskini mwanaume hawezi tena kujigawa na ana vipaumbele vingine

2.KUJIHAMI
haya matafiti haya,na mastory mitaani kuwa mama mkwe na binti yake hawaivi,siku hizi na kwenye kitchen parry binti anaambiwa kabisa kuwa hala hala kidole na macho kuna mkweo huko na mawifi ,matokeo yake binti anaingia kwenye ndoa tayri kashaandaa makucha!kwamba mimi ndo mimi na wlaahi watanikoma,maskini ya Mungu kumbe ile familia si ajabu si ya aina hiyo basi yemrai kashaambiwa na dada zake na story maofisini au saluni basi,huko ndani watajibebaaaje!mwanaume hapo hata akisema naenda kumsalimia mama au mama anakuja ye kanuna!
hapo huyo mama wa watu akupendaje zaidi na yeye kuanza kurudisha chuki!matokeo yake inaenea kwa wote

3.MWANAUME KUKOSA MSIMAMO WA KIUME
mwanaume akishaoa tayari anatakiwa kuwa na misimamo yake yeye kama baba wa familia na baba ndani ya nyumba ile,haijalishi alikuwa anapendwa na kuipenda familia yake mwanzo kiasi gani
ukioa unapaswa kumlinda mke wako,kutetea hadhi ya nyumba yako,mama yako alikuzaa na sasa umekua na umeoa!kwa hiyo kuendelea kuruhusu mama wa mwanaume kuwa na power kwenye nyumba yako kiasi cha mke kujihisi anapwaya lazima tu kinuke!NANI ANATAKA KUPANGIWA CHAKULA NA MAMA WA MUMEWE?NANI ANATAKA KUPANGIWA MUDA WA KUONGEA NA MUMEWE?
NANI ANATAKA KUAMBIA CHAKULA ANACHOPIKA MUMEWE HAKUZOEA KULA HIVO
NANI ANATAKA KUKOSOLEWA NAMNA ANAVYOHANDLE MUME WAKE
mbaya zaidi mwanaume unakaa kimya na kuona ni sawa tu!hukemei,sana sana unasa=upport ''MWAMBIE HUYO MAMA"
hapo lazima kuchafuke!huyo binti hawezi tena kuwa na amani humo ndani,maana hujihisi kaingiliwa kwenye himaya yake!

4.TABIA BINAFSI
wapo kinamama ni wana midomo ya asili tu!
hamtegemei mwanae,binti anakaa nae vizuri,mwanaume ana msimamo lakini basi tu mradi vurugu!
huyu anaweza kufunga safari kuja kwa kijana wake mradi tu aone mwanae anagharamia vipi mavazi ya mkewe,familia ya mwanamke inasaidiwa vipi,mwanamke anahudumiaje mume na watoto
hapa ndo sentesi kama mimi enzi zangu sikufanya hivi'
anasahau kuwa na yeye kwenye ndoa yake alikuwa na mapungufu,and afterall hiyo ni ndoa ya mwanae na huyo binti so namna mdada anaamua kuweka mambo ya ke ni vile yeye anataka!HER OWN WAYS!ana haki ya kutokuingiliwa ,aachwe akue na kujenga nyumba yake anavotaka,ikitokea namna anayotaka binti inaconcur na ya mama mkwe gud for her na iwapo inatokea kinyume mama mkwe akubali tu matokeo since na yeye alijenga yake kwa namna aliyotaka!

5.WANAWAKE KUJISAHAU
nenda mbele rudi nyuma wadada siku hizi kuna kujisahau sana!sana!mno!
sawa unafanya kazi,sawa una biashara,sawa mjini mafoleni mengi,sawa una deadlinea za kumeet,sawa una presentation next week,sawa una pesa kumzidi mumeo au sawa nae!
MAJUKUMU YA MKE KWENYE FAMILIA YANABAKI KUWA PALE!
hayo niliyotaja hapo juu najua ni changamoto kwelikweli na umama au umke bora!
lakini tujitahidi kwa namn ayoyote ile gap isionekane kiasi kikubwa hivi mpaka mama wakwe wapate pa kusemea!
anaona mwanae hapikiwi
mwanae hafuliwi
mwanae akirudi h.gal ndo anafungua mlango
mwanae haandaliwi chakula
wajukuu hawaogeshwi
wajukuu hawakaguliwi daftari
familia haisali pamoja
kutwa mama kiguu na njia!hatuna jumapili siye wala jumamosi!jumatatu -ijumaa tunatoka home saa kumi na moja,kurudi sa nne tuko bwaksi au tumechoka!
jumamosi asubuhi tunaamka saa nne tunaoga hao funguo zi wapi saluni ,tunarudi saa tisa dada ninyoshee naenda harusini!ukiruddi saa nane usiku
jumapili unaamka saaa sita mchana ,huanda watoto kwenda kanisani,huandai chai ya familia yako ikifika saa kumi na mija dada ninyoshee kile kitenge changu cha sare huyo kwenye kitchen party!
HUYO BIBI WA WATU ASISEMEEE?
lazima aseme mwali wangu!manake unamtesea mwanae!na wajukuuu!we uko na yako tuu!

LOL!kwa leo yanatosha!
my own experience
nilipoolewa tu nilianza kuishi na mama mkwe wangu,huu ni mwaka wa 9!



UMESOMEKA VZR SANA

NIKUAMKIE NISIKUAMKIE??

:madgrin: :madgrin:
 
Kwa upande wangu mi naona ni tatizo la pande mbili

1) kwanza kila mtu anatakiwa kutambua na kuheshimu wazo la kwamba familia ni taasisi inayojitegemea, ambayo nguvu yake iko katika ukaribu na upendo wa wanafamilia, ina uongozi, ina makubaliano maalum ya jinsi ya kuyaishi maisha haya na kulea watoto, mabadiliko ya makubaliano hayo ni lazima yajadiliwe na viongozi wa familia na waafikiane na hapo ndipo itakapoitwa familia bora;-dear mother; He is not that little boy u used to love and instuct about ins and outs anymore. He is a leader and its ur duty as a parent to make him a gud one. She is his partner in 'life' so do to her as u would to him.

2) Wanandoa wanatakiwa kujua wao ni mwili mmoja, lao moja wazazi wake wako na wako wake. Baba/Mama yako akikasirika ama kaudhika hubishani naye anaongea na unamjibu kwa adabu. Kwa kweli mama mkwe hata kama mbaya kiasi gani kama wewe ukiishi naye kwa akili, adabu na upole atakuheshimu tu!

I will tell u a story of three ladies in my life.
1) Mama wa mke wangu: I used to see them in church since long time ago. I have seen the love and respect she showed her family and I've always knew her daughter will be a very gud wife.

2) My mum: Bibi yangu ni mbabe na mkorofi mwanzo mwisho na ana bifu na wakweze wote isipokuwa mama yangu. Anapenda sana starehe na familia yetu ilikuwa strict na isiyo na hela kihivyo lakini anapenda kuja kwetu kwa sababu pale ndio title yake kama bibi/mama inaonekana na kuheshimika.

3) My wife: Ameweza kuingia kwenye familia yetu hadi mama na baba wanamrefer as a daughter tofauti na wengine. I dont know kama anapata shida na 'ma mkwe' wake kwa sababu sijawahi kuhisi hivyo ila nakumbuka kanifanya mpaka sasa nakuwa my parents favorite child yani wazazi wanapenda kuja kwetu kuliko kwengine.
 
...acha nipite mie sina uzoefu, mama mkwe wangu yupo poa ile mbaya na namchukulia kama mama yangu..........
 
Kwa hiyo Mama's boy hawapaswi kuoa?

Watoto wa pekee kwa mama zao hawana haki ya kupata Mke kisa mama zao wanawapenda sana.

But patamu panakuja wapi wanawake wa siku hizi mnaolewa kwa vigezo as mume awe na shule nzuri, kazi ya kueleweka, atoke maisha ya getini as familia bora kwao,, na wengi wenye hivyo vigezo ni mama's boy... Hapo ndo utamu unapokolea.. Mamas boy wanaboa lakini ndo wenye huwezo wa kumudu majukumu na mnavyopenda harusi za kutokelezea mnachagua mume kwa kuangalia financial status mjiandae sana kugombana na mama wakwe zenu as Mama's boy ndo wana sifa mnazotaka japokuwa hapa mnajifanya kupinga..

Nimeshaona mengi tu as hao watoto wa mama wanavyopendwa na wadada wakati wanajulikana kabisa Mama zao ndo roho yao.. Hali ya maisha imebadilisha akili za wadada as kila mmoja anataka aolewe kwenye maisha mazuri, watoto wake wasome shule nzuri na hata yeye avae vizuri watoto wa mama ndo wana access ya hivyo vitu...
kila siku huwa nakwambia nakuadmire sana aina yako ya kufikiri!sana!una mawazo ambayo natamani vijana wengi wa rika lako wawe hivo!!
 
Tatizo huwa linakua kubwa zaidi haswa;
1. Mama mkwe anapokuwa ni mjane.
2. Alikua anatunzwa vizuri na mwanae kabla hajaoa.
3. Mama mkwe umri umeshasonga kiasi cha kufikia umri tegemezi.
4. Mtoto wa kiume kabla ya kuoa alikua na shida(kiafya, kisaikolojia n.k), ambayo ni mama yake pekee ndio alikua ana uwezo wa kuitatua.
5. Mtoto wa kiume anapokuwa ndio wa pekee.
6. Tofauti za mitizamo ya kidini,kikoo na kikabila.
7. Kiburi cha wanawake pindi wanapoolewa, ile hali ya kuitwa Mrs Brown jina ambalo hata mkwewe hutumia(huwa wanyenyekevu sana kabla ya ndoa na ndio maana mama mkwe hakua mkorofi kabla).

Kuna mama mmoja yuko kwenye hii situation ambayo iko in bold, yani ninamsikitikia mpaka huwa nasema, mtoto wa kiume si mwenzio. Kama wewe ni mama wa kukutunza ni mtoto wa kike.........
 
Kwakweli tatizo kubwa ni wivu hasa pale mama anapohisi yeye anaumuhimu mkubwa katika maisha ya mwanae wakati huohuo mke wa mwanae nae amejipa cheo cha umuhimu mkubwa katika maamuzi yote ya mumewf na hapo tunapata kisa cha muwamba ngoma kuvutia kwake, lakini suluhisho ni dogo tu ambalo ni kila mtu kuwa na mipaka yake (mama, mtoto na mke)
 
Back
Top Bottom