30 US dollars - Zanzibar airport za nini ?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kama kuna ufisadi ambao unaonekana kama biashara ya mtu basi ipo pale Zanzibar airport ,inajulikana dunia nzima kuwa airport fee inakusanywa kutokana na mauzo ya tiketi ,unapokata tiketi tayari mapato ya airport zote utakazopita huwa unayalipia kwa maana unalipia at the initial stage.

Lakini kinachoonekana Zanzibar airport unapoondoka kuelekea nchi za nje itakubidi ulipie 30 US dollars ,ukihoji unaambiwa kama huna kazitafute lakini haondoki mtu bila ya kutuwachia hiyo hela.

Kama WaZanzibai mupo na mnafahamu mrija huu ni kwa ajili ya kitu gani mtueleze ,wabunge na wawakilishi hili wamelifumbia macho na sidhani kama hawalielewi lakini inaonekana wanaogopa kuhoji ,kwa njia hii anaweza mtu akaweka meza na kiti na kudai kila anaesafiri alipe.

Huu ni wizi mkubwa unaofanyika katika airport ya Zanzibar ,kwa ufupi inaoinyesha ni aina ya unyanyasi ,ni unyanyasaji tu hakuna kingine.
 
huu ni ujambazi wa mchana kweupe......hebu tumuulize mkurugenzi mohammed malik atuhabarishe hii ni mipango ya serikali au ni mipango yake binafsi.
 
Kama kuna ufisadi ambao unaonekana kama biashara ya mtu basi ipo pale Zanzibar airport ,inajulikana dunia nzima kuwa airport fee inakusanywa kutokana na mauzo ya tiketi ,unapokata tiketi tayari mapato ya airport zote utakazopita huwa unayalipia kwa maana unalipia at the initial stage.

Lakini kinachoonekana Zanzibar airport unapoondoka kuelekea nchi za nje itakubidi ulipie 30 US dollars ,ukihoji unaambiwa kama huna kazitafute lakini haondoki mtu bila ya kutuwachia hiyo hela.

Kama WaZanzibai mupo na mnafahamu mrija huu ni kwa ajili ya kitu gani mtueleze ,wabunge na wawakilishi hili wamelifumbia macho na sidhani kama hawalielewi lakini inaonekana wanaogopa kuhoji ,kwa njia hii anaweza mtu akaweka meza na kiti na kudai kila anaesafiri alipe.

Huu ni wizi mkubwa unaofanyika katika airport ya Zanzibar ,kwa ufupi inaoinyesha ni aina ya unyanyasi ,ni unyanyasaji tu hakuna kingine.

Wizi mtupu. Sasa hayo mapato yanakwenda wapi, maana uwanja wa Zanzibar ni mmoja wa viwanja vibovu duniani, soma hapa
 
Lakini kinachoonekana Zanzibar airport unapoondoka kuelekea nchi za nje itakubidi ulipie 30 US dollars ,ukihoji unaambiwa kama huna kazitafute lakini haondoki mtu bila ya kutuwachia hiyo hela.

Hapa si ajabu nchi za nje ni pamoja na Tanganyika. Lakini nakumbuka hata Dar (DIA) zamani kulikuwa na utaratibu kama huu mbovu - uliondolewa baada ya kulalamikiwa.
 
Mwiba tafadhali angali ticket yako. Kama hio Airport charge ya $30 imeandikwa basi una haki ya kudai. Kama haijaandikwa basi huo si ufisadi ni sehem tu ya malipo ya airport. Kila aiport ina namna yake ya kuchukua pesa hio.

Kuna uwezekano kama una hops mbili au tatu basi zote zita appear ktk tickect yako. so Kama ZNZ wanachukua chao, Kenya watachukua chao au Bara nao watachukua chao...

Bara ilikuwepo zamani, siku hizi wameingiza moja kwa moja ktk ticket ya ndege.

Muhimu kuishauri SMZ kuwa hii $30 waiingize moja kwa moja ktk gharama za ticket, hii itaisaidia mianya ambayo ipo sasa ambapo wajanja wanaweza zikwapua anytime, au Viongozi wachache kujifanya mastaafu kutolipa hio gharama na wale wenye kujifanya kujuana na viongozi wa airport kutolipa.

Pia Muhim SMZ washauriwe kuwa wasitumie dola na watumie TZS utumiaji wa dola locally unatuumiza wananchi.

Baya ambalo sote yapasa kulisema ni kuwa wananchi tunapotoa pesa hizi twahitaji Huduma bora ktk Viwanja vyetu.
 
Back
Top Bottom