US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kama ni kweli US/EU walimtoa Saadam Hussein kwa uongo wa kusaka WMD, kisha wakamtoa Ghadafi madarakani kufuatia kuwaunganisha Waafrika, na Mugabe wakamtoa kwa ku over stay?, kufuatia JPM anavyotetea rasilimali za nchi yetu tusiendelee kunyonywa, kufisadiwa na Tanzania kufanywa shamba la bibi, Jee mabeberu hawa wakiamua kutaka kumtoa rais Magufuli madarakani, kwa kisingizio chochote na kusingizia kutetea demokrasia, jee wataweza?. Jee sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa Taifa hili tutakubali?.

Marekani, US, na washarika wake, EU, kupitia mashirika yao ya kibeberu ikiwemo IMF, WB, US AID, CIA, NATO, etc, ndio nchi inayoongoza kwa imperialism, wakiamua kiongozi fulani hawamtaki kwa maslahi yao, watamtafutia sababu, wakikosa, watamtungia uongo wa ukiukwaji wa haki za binadamu, mradi wapate justification ya kuingilia mambo ya ndani na kumuondoa. Watatafuta sababu zozote na kutumia mbinu zozote kumtafutia sababu, ili wamuondoshe!.

Jana nimesoma nyaraka mbili za EU na US, ambazo kiukweli zimezungumza mambo makubwa, ikiwemo nia ovu ya kutaka kumuondoa rais Magufuli madarakani kwa kisingizio cha kujenga demokrasia. Wengi wemejikita katika hoja ndogo ya ushoga, lakini ni wachache sana wenye uwezo wa ku read in between the lines, na kubaini the hidden motive behind which is the real motive, huo ushoga ni sugar cotting tuu ya kupaka sukari ili ulambe utamu usijue shubiri iliyomo ndani ya nyaraka zao, lengo ni kutaka kumng'oa rais Magufuli madarakani kwa mlango wa nyuma, baada ya rais Magufuli, kutishia interests zao, ila kutumia kisingizio cha kukuza demokrasia.
Tamko la EU
European Parliament resolution on Tanzania - JamiiForums
11. Expresses serious concern about the pressure exerted by the Tanzanian Government on the EU Head of Delegation, Roeland van de Geer; welcomes the decision of the European Union and its Member States to conduct a comprehensive review of EU policies towards Tanzania; insists on the importance of political dialogue to seek tangible commitments from the Tanzanian authorities towards creating an enabling environment for the operation of civil society, political parties and the media; calls on the Commission to ensure that an explicit reference to non-discrimination based on sexual orientation is included in the future ACP-EU partnership agreement post-2020;

14. Calls for the EU to continue to closely monitor the human rights situation in Tanzania, particularly through regular reporting by its delegation; calls on the European Union Delegation and Member States to do all they can to provide emergency protection and support to human rights defenders at risk;

15. Instructs its President to forward this resolution to the Council, the Commission, the Vice-President of the European Commission / High Representative of the Union for Foreign Affairs and Security Policy, the EU Special Representative for Human Rights, the ACP-EU Council, the institutions of the African Union, the institutions of the East African Community, and the President, Government and Parliament of Tanzania.

8. Calls on the Tanzanian authorities , most notably President Magufuli’s declaration that girls who give birth should not be allowed to return to school.

9. Urges the President of Tanzania to make the country’s Human Rights Commission operational as soon as possible

10. Calls on the Tanzanian authorities to release political prisoners.
Hapo number 8,hawa EU ni bure kabisa!, Rais Magufuli ndiye aliyesema hasomeshi watoto wanapenda kucheza michezo ya kikubwa hivyo kupata ujauzito. Sasa hawa wazungu, una call authority gani iingilie?.

Number 9 wanampangia kazi Rais Magufuli?!.

Number 10 kuna watu wameshitakiwa for political crimes or ni criminal issues?.

Hawajui kuwa rais Magufuli hapangiwi?. Kama katiba alioapa kuilinda, ameweka kando, na kufanya kile anaona kinafaa, who the hell is EU?!.

Naona hawa wazungu wanajifurahisha tuu, kama vipi wazuie tuu misaada yao na watunyime viza za Shengen, tutakwenda UK na China.

Tanzania ni sovereign state, tuna uhuru wa kujipangia mambo yetu wenyewe, kama hatutaki ushoga wasitupangie na kutulazimisha bali tufundishwe tuu somo la managing diversity ya kuwafundisha Watanzania kuwa ushoga ni ulemavu wa hormones za jinsia na viungo vya uzazi, tufundishwe kuwakubali mashoga kama walemavu wengine wote, tusiwabague wala kuwanyanyapaa hivyo tukubali kubadili sheria zetu kuhusu ushoga willingly baada ya kuelimishwa na sio kulazimishwa na kuingiliwa.

Wamarekani nao wakafuatia Baada ya EU, Serikali ya Marekani nayo yaugeukia utawala wa Rais Magufuli - JamiiForums
Maseneta wa Marekani wamemuandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo wakiishutumu Serikali ya Tanzania. Wasema tangu 2015 inaongozwa kwa sera za ajabu

- Wadai Serikali inaminya haki za watu na demokrasia. Wakaongeza kuwa tangu mwaka 2016 nchi hiyo haina Balozi rasmi nchini Tanzania hivyo ni lazima Balozi ateuliwe.

- Wasema kuwa Ubalozi wao uanze kufanya juhudi za kuhakisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka 2020.

- Wataka Marekani ihakikishe hakuna fedha zinatolewa na taasisi yoyote ya kimataifa kufadhili sera zinazoonekana kuwa kinyume na haki za binadamu

The United States too must act to address these challenges. First, the Administration should appoint an Ambassador to Tanzania to lead our strategies, programs and diplomatic outreach on the ground. The post has been vacant since late 2016. Second, we should begin undertaking actions that support fair and credible elections in 2020. The U.S. embassy and USAID mission in Tanzania should immediately be allocated resources to facilitate and implement a full array of democracy, rights, and governance programs — including on-the-ground independent election planners and long-term observers who can monitor and report on the pre-election environment, electoral processes, and eventual election outcomes.

Finally, we must develop a strategy with likeminded diplomatic partners in Tanzania and multilateral fora to speak out against President Magufuli’s war on democratic freedoms and civil liberties, and urge the Tanzanian government to take concerted action to ensure that all political and civic rights guaranteed under the Tanzanian constitution are fully respected. This should include using our voice and vote in International Financial Institutions to ensure no funding is provided that supports intolerant, unfair or inequitable public policies.


Mr. Secretary, Tanzania’s current political trajectory is deeply troubling. The progress that Tanzania has made in the last decade and a half in the areas of democracy and respect for civil liberties is undergoing a reversal before our very eyes. We can and should take immediate steps to help halt this backsliding. We stand ready to support the Administration’s efforts to stem the growing tide of repression and ensure adherence to internationally recognized civil liberties and human rights norms and standards in Tanzania.,
Huu ni mpango wa kumpindua rais Magufuli kwa kupitia mlango wa nyuma wa kutumia kisingizio cha kukuza demokrasia, jee Watanzania Wazalendo tukubali?.

Sisi Tanzania tumeishazoea kutishwa nyau, sasa hatuogopi tena, kwani Marekani ndio nani? si ni nchi tuu kama Tanzania?, kwa nini watuingilie, watupangie?. Huu Waraka unampango wa ina ovu ya kutaka kumuondoa rais Magufuli madarakani kwa mlango wa nyuma, kama walivyofanya kwa Ghadafi na Saadam, kwa kutumia vibaraka kwa mgongo wa human rights defenders!.

Tanzania ni nchi huru, a sovereign state. tusikubali na wasitupangie, wasituingilie, tunachofanya ndio the African democracy, kama vipi, tuwatimue tuu waende tuu na ubalozi wao wafunge, rafiki yetu wa kweli na wa dhati, China si yupo?.

Kwani walipotususa kuhusu ile demokrasia yetu ya uchaguzi huru na wa haki wa Zanzibar na pesa za MCC wakatugomea, tulikosa nini?, si tunadunda tuu, tena ndio kwanza tunajenga my flyover, tunajenga SGR, Stigler Gorje na kununua midege ya kufa mtu, tena tunafanya yote haya kwa kutumia fedha zetu wenyewe za ndani, hivyo wasitutishe na vimisaada vyao njaa, Tanzania ni nchi tajiri sana, japo wananchi wake ni masikini wa kutupa, ila ni masikini jeuri, waacheni tuu hao Wamarekani waseme mchana, usiku watalala, huku Tanzania tukiendelea kudunda kuelekea kuwa nchi ya viwanda ya uchumi wa gesi na uchumi wa kati tukielekea kuwa a donor country, ile nchi ya ahadi, mabomba nchi nzima, yatatoa maziwa na asali.

My Take.
1. Marekani na EU wataingilia mambo yetu ya ndani kwa ku fund vibaraka watakaokuwa dissidents na kuleta chokochoko.
2. Wataingilia uchaguzi wetu kwa kutupangia kibaraka wa kuchaguliwa.
3. Watakata misaada yao ili kutushinikiza kufuata mambo yao ikiwemo kuruhusu ushoga.
4.Wata fund disidents, kuwa vibaraka wao kujifanya wanapigania demokrasia ili waweke watu wao.
4. Wizara yao ya mambo ya nje, kupitia ubalozi wao, wataanza kutoa security allerts za matishio ya mashambulizi ya kigaidi ili kuonyeshea wanatujali sana.
5. Kutatokea mashambulio maeneo ya mikusanyiko mikubwa ya wageni, uwekezaji mkubwa au vivutio vikuu vya utalii, ku destabilize the goverment kwa kuonyesha kuwa Mugufuli hawezi kuilinda nchi hii ili kupata justification ya intevention kutuingilia.

A way Forward.
1. Tanzania kama nchi huru ili kulinda uhuru wetu, kwanza tukatae misaada yoyote ya US na EU ili kuonyesha hawatuwategemei kwa lolote au kwa chochote, tuwambie wazi wazi we dont want them here anymore, they should go away together with their blood stinking money disguized as development aid.
2. Na badala yake tumtegemee China ambaye ndiye rafiki wa kweli na wa dhati na hata ikibidi kumkabidhi nchi yetu, tumkabidhi Mchina atutawale kiuchumi.

3. Tuwafukuze nchini mwetu, EU na US wafunge balozi zao na mashirika yao ya Misaada, ikiwemo USAID, wafungashe virago vyao warudi zao kwao.

4. Tuandae the charter of Tanzania demokracy ikieleza shughuli za siasa kwa mwaka mzima ni right kwa chama tawala tuu, vyama vya upinzani visubiri mpaka wakati wa uchaguzi.

5. Tuirudishe Tanzania kuwa nchi ya chama komoja cha siasa kuepusha vibaraka wa mabeberu kushika nchi yetu hii ya kijamaa, mbona China na Korea Kaskazini wameweza na wana maendeleo makubwa, ili kuzuia US na EU wasitupenyezee vibaraka wao kwenye vyama vya upinzani na kuingilia uchaguzi wetu.

6. Japo Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru, tuifanye more inclusive ili kupunguza kelele za rafiki zetu wazuri wengine kama nchi za Scandnavia na Nordic ambao wangependa kuona demokrasia ya kweli na haki ikitendeka kupitia uchaguzi huru na haki.

7. Tusibadili kwanza sheria zetu kuhusu ushoga, bali tutoe elimu ya managing diversity kwa kuelimisha watu wetu kuwa ushoga ni ulemavu tuu kama ulemavu mwingine wowote, watu wanazaliwa nao, hivyo tusiupromote bali tuukubali upo, tuuvumilie na kuwavumilia bila kuwabagua au kuwa nyanyapaa.

8. Tuvimonite very closely vikundi vyote vya utetezi wa haki za binaadamu, NGO's na political activists, funded by USAID, na EU, wafanye utetezi wao kwa viwango vya Kitanzania with Tanzania democracy na sio vigezo vya kizungu. Mfano mzuri uchaguzi wa rais wa Tanzania, kunakuwa na mgombea mmoja mwenye vingora, state media, state logistic support, state machinery, na watu, fedha, magari ya state yanayobadilishwa number na gharama za state, kushindana na wagombea wengine kwenye uchaguzi huru na wa haki, na mshindi hupatikana kihalali.

9. Kwa vile US wataongeza funds kupitia US AID, tuwamonite funds hizo ziwe kufund shughuli za kijamii tuu na sio political ili wasituingilie mambo yetu ya ndani.

10. Kinga ni bora kuliko Tiba
Dalili ya mvua ni mawingu.
Mchelea mwiba mguu huo tende.
Chururu si ndo ndo ndo.
Haba na haba hujaza kibaba.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye.

Nyaraka hizi ni mawingu, ni mwiba, ni ndo ndo ndo, ni haba na haba, ni kilio tuu cha mwana, jee Watanzania wazalendo wa kweli wa Taifa hili, hata baada ya kuona dalili, tusubiri mvua inyeshe, tusubiri mguu uote tende, tusubiri chururu, au tusubiri kibaba kijae, na kusubiri kuja kulia?.

Jumamisi Njema.

Paskali
Update
Huyu ndio mwandishi msomi Pascal Mayalla naomfahamu, kwa kuchanganua mambo ipasavyo.

Swali zuri sana, ila ni wachache wanaweza kuongea fikra za moyoni. Kwa mtazamo wangu swali hili ni kipimo tosha cha UZALENDO NA UKWELI ndani ya nchi yetu.

●Ila napinga hio SECTION ya "A WAY FORWARD" yote, kasoro kipengele cha kukataa ushoga ndio naunga mkono, tukatae ushoga kwa nguvu zote, sababu moja kuu ambayo itatusaidia "Mahakama Ya Dunia Ya Haki Za Binaadamu" mwezi September, 2017 ilitoa hukumu kua "USHOGA/NDOA ZA JINSIA MOJA" SIO HAKI ZA BINAADAMU.

No Right to Homosexual Marriage says World Court of Human Rights

Mapingamizi Yangu juu ya Section tajwa hapo;

1) Kusimama sisi kama sisi bila support ya US na EU, haiwezekani, na tukilazimisha hilo basi tutaua raia kwa shida/dhiki na pengine hata machafuko/vita. Hasa ukizingatia sisi ni nchi ya hali ya chini (3rd World Country). Rejea alichoongea Mh Waziri Wa Fedha Dr Mpango hapo jana, kuhusiana na hali mbaya ya kifedha tuliokua nayo Tanzania hivi sasa, kutokana na kusitishwa kwa misaada na wafadhili halafu tafakari hapo WAMESITISHA TU misaada, Je wakituwekea VIKWAZO (Kama vya Uturuki na Urusi), si watatuua.

2) US na EU hawashindwi FITINA na hawajawahi kushindwa kuchochea vita, tumeshuhudia walivyochochea vita IRAQ, LIBYA, SYRIA. Tumeshuhudia walivyo chochea URUSI na UTURUKI kuwekewa vikwazo vya kibiashara (tena walikaziwa bolt mpaka tredi ya mwisho) n.k.

Fitina hizi zime waathiri sana hizo nchi husika, kufikia mpaka leo NCHI HAZITAWALIKI.

Russia taifa lenye nguvu kubwa, Rais Putin ilibidi akiri wazi kua vikwazo vile vimemtikisa kweli kweli (Hii ni nchi yenye uchumi mkubwa sana) na wana kila kitu;

i) Nuclear

ii) Viwanda vya silaha/ndege/submarines za kisasa (Gen 4 Arms & Jets Factory).

iii) Wana satelite zao.

iv) Gas & Dhahabu. Na kadhalika.

3) Tumeshuhudia kwa Zimbabwe alichofanywa kwa kuwekewa VIKWAZO na KUZUIWA MISAADA (Kwa bahati nzuri hatuja hadithiwa kuhusu Zimbabwe ya Robert Mugabe, Generation yetu imeshuhudia kwa macho na masikio yetu yaliyotokea huko).

Uchumi wa zimbambwe haukuyumba, ULIKUFA NA KUZIKWA kabisa. Ilifikia hatua mtu anakwenda sokoni na Billion 3 kununua mkate, au mtu akienda na Billioni 1 kuendea box za sigara.

***Kipi tulichojifunza kutokana na mifano hai tajwa hapo juu???

*** Jeuri inafaida gani na ya nini kwa wanaotuzidi nguvu, uwezo na maarifa??? Ukizingati sisi bado ni taifa lenye raia wengi wa hali ya chini/masikini. (Leo hii jeuri ya Robert Mugabe imemfikisha wapi kwa sasa alipo)

4) TUTAMBUE: USA na EU, wanategemea sana VITA duniani; ili,

a) Viwanda vyao vya silaha viuze silaha. Wapate pesa na mzunguko wa biashara.

b) "Practical Training" kwa wanajeshi wao, wanafundisha wanajeshi kisha wanahitaji kuwapeleka VITANI WAPATE PRACTICAL EXPERIENCE, sio mwanajeshi anapita depo kisha anakaa miaka 30 bila kujaribiwa vitani.

c) Majaribio ya UBORA wa silaha zao za kivita walizotengeneza MPYA (Geni 4 Firearms). Na kujifunza/kuzitumia mbinu MPYA za kivita wanazobuni.

NB Hayo nlioyapinga, yanaweza yakasababisha uchochezi wa machafuko/vita katika nchi yetu (wao wakiwa kama wafadhili wa machafuko/vita, kwa kutoa misaada kwa kundi linaloipinga serikali kwa msharti baada ya vita wachukue rasilimali zetu kama vile DHAHABU, ALMASI, GAS, TANZANITE, RUBY n.k) kama walivyochukua MAFUTA kule IRAQ na LIBYA.

5) Tusijipe moyo kwa kujidanganya, hatuwawezi USA na EU kwa lolote hata tufanye nini. Hawa watu wanaiendesha UNITED NATIONS na body zote za UMOJA WA KIDUNIA (Including African Union).

●Labda niulize swali, ili tuweke mambo sawa; Ukipitia kwa umakini hio MAKALA YA European Union na USA, bila kua BIASED/KUTETEA/KUVUTIA PANDE YOYOTE ILE;

□□1) Ni kitu gani walichosema ni cha uongo ambacho hakipo kabisa/hakijawahi fanyika nchini??? (Ambacho si kweli na wametusingizia tu Tanzania, pengine kwa wivu wao kama viongozi wetu wanavyosema).

□□2) Ni pendekezo gani ambalo wametoa EU na USA halina maslahi/nia njema kwa Tanzania???? (Kuachilia swala la kuhalalisha USHOGA, ambalo mimi binafsi napinga vikali kulinda MILA, DESTURI NA DINI ZETU, kama nilivyoeleza juu na kutoa sababu za kupinga).

□□3) Mapendekezo EU na USA waliotoa dhidi ya serikali ya Tanzania, kuna pendekezo gani litakalo leta madhara na hasara kubwa kwa taifa kama yakiitikiwa??? (Ukiacha la ushoga).

KWA ELIMU YANGU NDOGO;

Ukiacha hilo swala la ushoga ambalo napinga vikali. Yaliobakia mapendekezo hakuna hata moja baya wala la uongo walioandika Eu na USA.

Kila walichoandika ni UKWELI uliowazi kabisa na WENYE FAIDA KUBWA kwa taifa letu, kurudisha amani na mshikamano kama ulivyokua huko nyuma!!!

Wito wangu,

●Tusijaribu kushindana UBAVU na EU na USA, ni sawa na sisimizi kumchimba biti tembo, hatuwawezi kwa lolote na tusijidanganye kuthubutu, tutajuta sisi na vizazi vyetu vijavyo (Kama wanavyojuta Somalia, Iraq, Syria, Libya, Zimbabwe).

●Atakae thubutu kutaka kushindana na Eu na USA, basi historia haitakuja KUMSAMEHE na KUMSTIRI AIBU yeye na wenzake, pamoja na vizazi vyake. Mawili;

a) Watahakikisha wanamuua atakaepinga WITO wao waliotoa. Kama walivyomfanya Saddam Hussein au Muamar Gaddafi.

b) Watatolewa ARREST WARRANT na kushitakiwa ICJ (turejee kwenye historia ya baadhi ya viongozi wa Africa walikutana na meno/kucha za ICJ; Charles Taylor na Colonel Theoneste Bagosora).

● Tusijidanganye kua hao wa CHINA ni rafiki wa kweli (hao ni nyoka wenye sumu kali sana) na wanadhuru kuliko hata Eu na USA, Zambia misaada/mikopo imesababisha wametaifishwa na wa china;

1) Kenneth Kaunda International Airport.

2) ZESCO, shirika lao la umeme.

3) Channel ya television ya taifa.

4) Wanakaribia kuchukua migodi ya COPPER.

TUTAFAKARI!!!!; Tupokee wito wa hayo mapendekezo ya EU na USA (mapendekezo yenye tija na faida kubwa kwa taifa, isipokua la ushoga) au tufanye jeuri watuadhibu ili tuwaingize wachina waje watumalize kabisa??????

● Maamuzi binafsi ya wachache yasituletee ATHARI taifa zima na vizazi vyetu. Kuna msemo unasema "Ni heri wachache watolewe KAFARA ili wengi WAPONE".

● Mh Mahiga (Waziri wa Mambo Ya Nje) ndio alioshika mpini mpaka sasa, majibu atakayotoa juu ya matamko ya EU na USA, ndio yatakaotoa hukumu ya mwisho dhidi ya nchi yetu. Ningeomba asikurupuke kuwajibu kabla ya kukaa chini na kutafakari/kupata ushauri kwa kina na kufukia maamuzi sahihi/busara.

Pia asitokee kiongozi yoyote kutoa JIBU kwa NIABA ya NCHI (Tumeshuhudia viongozi wakikurupuka kutoa matamko hata yasiowahusu. Waziri wa Maliasili alitoa muongozo juu ya USHOGA akatoa kuhusu MAKATO YA WASTAAFU:- Sio kazi yake. Mkuu wa mkoa aliunda KIKOSI KAZI cha kukamata wakati serikali ikimtazama tu, kilivyonuka ndio wakajifanya kumkana. Haya ya kukurupuka ndio yametuchochea kwenye MOTO).

● Taifa tuungane tuwe kitu kimoja, vyama vya siasa tuweke pembeni na tuungane, hili janga ni la KITAIFA, na sisi wote tutaathirika (Hakuna atakae salimika).

● Kama kuna viongozi (bila kuangalia cheo) waliochochea KUHARIBU MAHUSIANO YETU NA NCHI NYINGINE, kama ni kuwajibishwa mbele ya sheria kwaajili ya kuweka taifa letu salama, basi waswekwe jela hata miaka 100 kwaajili ya taifa. Wachache wasituvunjie amani na misingi iliyojengwa kwa tabu toka uhuru miaka 58 iliopita.

Tusikubali hao jamaa watugeuze shamba la kujaribiwa na SILAHA ZAO wanazotengeneza (Kama Syria) watapiga mabomu mpaka INZI na MBU.

HAKIKA HATUJUI TUNALO LITAFUTA, ILA TUTAJUTA TUSIPOANGALIA.

Nawasilisha,
Zitto 2020, njoo utukosoe humu.
Asante kwa very objective analysis iliyoshiba hoja.
Mwenye masikio na asikie
P.
 
Watakuwa wamefanya jambo ambalo Mungu mwenyewe ndio ataamua uhalali wake na hatima yake maana yanayoendelea nchini kwa sasa ni kama yanafanywa na watu wasio na imani za kidini na wala wasiomjua Mungu!

Ukatili,ukandamizaji,dhuluma na uonevu; vinataka kugeuzwa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku!

Nakumbuka hata viongozi wetu wa dini walionya na kushauri ila waliishia kukejeliwa na kubezwa.Kwahiyo,kwa viburi hivi,wacheni Mungu atende limependazalo ikiwezekana kama alivyowatendea wana wa Israeli.

Tumefika pabaya maana hata kina MO leo hii wanalalamika ingawa wameamua kusamehe.
 
Watakuwa wametusaidi sana.
75C8776F-C8A0-4A50-82F3-C576C3EF793B.jpeg
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, kama ni kweli US/EU walimtoa Saadam Hussein kwa uongo wa kusaka WMD, kisha wakamtoa Ghadafi madarakani kufuatia kuwaunganisha Waafrika, na Mugabe wakamtoa kwa ku over stay?, Jee wakiamua kutoa rais Magufuli madarakani, jee wataweza?. Jee sisi Watanzania wazalendo wa Taifa hili tutakubali?.

Jana nimesoma nyaraka mbili za EU na US, ambazo kiukweli zimezungumza mambo makubwa, ikiwemo nia ovu ya kumuondoa rais Magufuli madarakani kwa kisingizio cha kujenga demokrasia. Wengi wemejikita katika hoja ndogo ya ushoga, lakini ni wachache sana wenye uwezo wa to read in between the lines, na kubaini the real motive behind, huo ushoga ni sugar cotting tuu ya shubiri iliyomo ndani ya mabandiko haya, ni kumgoa rais Magufuli madarakani! kwa kisingizio cha kukuza demokrasia.
Tamko la EU
European Parliament resolution on Tanzania - JamiiForums
Hapo number 8,hawa EU ni bure kabisa!, Rais Magufuli ndiye aliyesema hasomeshi wenye mimba, sasa una call authority gani iingilie?.

Number 9 wanampangia kazi Rais Magufuli?!.

Number 10 kuna watu wameshitakiwa for political crimes or ni criminal issues.

Hawajui kuwa Magufuli hapangiwi?. Kama katiba alioapa kuilinda ameweka pembeni, who is EU?.

Naona hawa wazungu wanajifurahisha tuu, kama vipi wazuie tuu misaada yao na watunyime visas za Shengen, tutakwenda UK na China.

Tanzania ni sovereign state, tuna uhuru wa kujipangia mambo yetu kama hatutaki ushoga wasitupangie na kutulazimisha bali tufundishwe tuu managing diversity ya kuwakubali mashoga kama walemavu wengine wote, tusiwabague wala kuwanyanyapaa lakini kubadili sheria zetu bado sana.

Wamarekani nao wakafuatia Baada ya EU, Serikali ya Marekani nayo yaugeukia utawala wa Rais Magufuli - JamiiForums

Huu ni mpango wa kumpindua rais Magufuli kwa kutumia kisingizio cha kukuza demokrasia, jee Watanzania Wazalendo tukubali?.

Sisi Tanzania tumeishazoea kutishwa nyau, sasa hatuogopi tena, kwani Marekani ndio nani? si ni nchi tuu kama Tanzania?, kwa nini watuingilie, watupangie?. Hili barua inampango wa kumuondoa rais Magufuli madarakani kwa mlango wa nyuma. kama walivyofanya kwa Ghadafi na Saadam, kwa kutumia vibaraka kwa mgongo wa human rights defenders.
Tanzania ni nchi huru, a sovereign state. tusikubali, wasitupangie, na wasituingilie, tunachofanya
ndio African democracy, kama vipi, tuwatimue tuu waende tuu na ubalozi wao wafunge, rafiki yetu wa kweli na wa dhati, China si yupo?.
Kwani walipotususa kuhusu ile demokrasia yetu ya uchaguzi huru na wa haki wa Zanzibar na pesa za MCC wakatugomea, tulikosa nini?, si tunadunda tuu, tena ndio kwanza tunajenga my flyover, tunajenga SGR, Stiggler Gorje na kununua midege ya kufa mtu, tena tunafanya yote haya kwa kutumia fedha zetu wenyewe za ndani, hivyo wasitutishe na vimisaada vyao njaa, Tanzania ni nchi tajiri japo wananchi wake ni masikini, ila ni masikini jeuri, waacheni tuu hao wamarekani waseme mchana, usiku watalala, huku Tanzania tukiendelea kudunda kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati tukielekea kuwa a donor country, ile nchi ya ahadi, mabomba nchi nzima, yatatoa maziwa na asali.

My Take.
1. Marekani na EU wataingilia mambo yetu ya ndani kwa ku fund vibaraka watakaokuwa dissidents na kuleta chokochoko.
2. Wataingilia uchaguzi wetu kwa kutupangia kibaraka wa kuchaguliwa.
3. Watakata misaada yao ili kutushinikiza kufuata mambo yao ikiwemo kuruhusu ushoga.

A way Forward.
1. Tanzania kama nchi huru ili kulinda uhuru wetu, kwanza tukatae misaada yoyote ya US na EU ili kuonyesha hawatuwategemei kwa lolote na badala yake tumtegemee China ambaye ndiye rafiki wa kweli na wa dhati na hata ikibidi kumkabidhi nchi yetu, tumkabidhi Mchina.

2. Tuwafukuze nchini mwetu, wafunge balozi zao na kufungasha virago vyao warudi kwao.

3. Tuandae the charter of Tanzania demokracy ikieleza shughuli za siasa kwa mwaka mzima ni right kwa chama tawala tuu, vyama vya upinzani ni mpaka wakati wa uchaguzi.

4. Tuirudishe Tanzania kuwa nchi ya chama komoja, mbona China na Korea Kaskazini wameweza na wana maendeleo makubwa, ili kuzuia US na EU wasitupenyezee vibaraka wao kwenye vyama vya upinzani na kuingilia uchaguzi wetu.

5. Japo Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru, tuifanye more inclusive ili kupunguza kelele za rafiki zetu wazuri wengine ambao wangependa kuona haki ikitendeka kupitia uchaguzi huru na haki.

6. Tusibadili sheria zetu kuhusu ushoga, bali tutoe elimu ya managing diversity kwa kuelimisha watu wetu kuwa ushoga ni ulemavu tuu kama ulemavu mwingine, watu wanazaliwa nao, hivyo tusiupromote bali tuukubali upo, tuuvumilie na kuwavumilia bila kuwabagua au kuwa nyanyapaa.

7. Tuvimonite very closely vikundi vyote vya utetezi wa haki za binaadamu, NGO's na political activists, wafanye utetezi wao kwa viwango vya Kitanzania with Tanzania democracy na sio vigezo vya kizungu. Mfano mzuri uchaguzi wa rais wa Tanzania, kunakuwa na mgombea mmoja mwenye vingora, state media, state logistic support, state machinery, na watu, fedha, magari ya state yanayobadilishwa number na gharama za state, kushindana na wagombea wengine kwenye uchaguzi huru na wa haki, na mshindi hupatikana kihalali.

8. Kwa vile US wataongeza funds kupitia US AID, tuwamonite funds hizo ziwe kufund shughuli za kijamii tuu na sio political ili wasituingilie mambo yetu ya ndani.

Kinga ni bora kuliko Tiba
Dalili ya mvua ni mawingu.
Mchelea mwiba mguu huo tende.
Chururu si ndo ndo ndo.
Haba na haba hujaza kibaba.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye.

Nyaraka hizi ni mawingu, ni mwiba, ndo ndo ndo, ni haba na haba, ni kilio tuu cha mwana, jee Watanzania wazalendo wa kweli wa Taifa hili, tusubiri mvua inyeshe, tusibiri mguu uote tende, tusubiri chururu, au tusubiri kibaba kijae, na kusubiri kuja kulia?.

Jumamisi Njema.

Paskali
@pascal mayalla yaani unajua kweli kumchanganya JIWE. akipitia hapa harakaharaka + kukurupuka kama kawaida yake.. anaweza kusema unamsaidia yeye kumbe maskini ni kama kukugeuzia kisogo afu unamzomea
mpaka aje kugundua ohooo kwishnehi 2020 inahusu.
 
visasi vya wazungu vinakaa hata karne,tangu lockerbie bombing iliyofanywa na ghadafi mpaka wanamtoa ni miaka,sadam,bush baba na mwana walipokezana

hawa watu wanayakumbuka matusi kuhusu migodi,mmewafanya wameingia gharama ktk gesi leo mnakimbia mradi mnaenda stiglers,hawa watu trilioni zao zinaoza! Je watakubali?
 
Back
Top Bottom