2pac alifanya harakati za kudai haki na kuelimisha jamii, Notorious Big aliedanganya maisha yake na kuimba uhuni pekee, anamsogelea kwa kipi?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
2 pac y.jpeg
2 pac.jpeg


Huyu alikulia hood mitaa iliyojaa msoto, uhalifu na umasikini, wazazi wake walikuwa kundi la black oanthers wanaharakati wa kupigania haki za wamarekani weusi, ni kundi lililokuwa likisakwa kila kukicha na serikali ,mama yake pekee alikuwa na kesi kama 50 zs uchochezi, kalelewa na ndugu tofauti tofauti ambao nao walikuwa black panthers maana baba yake hakuwepo na mama yake stress zilimsomba aingie kwenye madawa, hata ndugu alioishi nao wengi walipewa kesi za kufungwa jela, hali ya kukulia haya maisha nae alibeba vitu kwenye suala la kuwa mtetezi wa haki.

Tofauti na rappers wengi, 2 pac alipenda sana kujisomea vitabu kuongeza maarifa, kajisomea vitabu zaidi ya 70 !! Shuleni alipenda zaidi kujifunza masomo ya sanaa kwenye uandishi wa mashairi (poetry) na uigizaji,

2pac aliweza kufanya kazi kibao kudai haki, kuelimisha jamii, kutoa postive motivation, n.k. ilikuwa ni ndani ya damu yake kwa maisha aliyopitia na watu waliomkuza, waweza kumsikilizisha hata mtoto wako baadhi ya nyimbo zake apate cha kujifunza.

Changes ilikuwa kazi ya kiharakati kutetea haki za mtu mweusi, kukemea ubaguzi na kuhamasisha umoja wa watu weusi.

Dear mama ilitoa fundisho kuwa mama ni mama tu hata akiwa na mapungufu yake (mama yake alikuwa teja)

Only God can judge me alitoa ujumbe maridhawa kwamba ni Mungu pekee wa kumhukumu kikamilifu,

Brenda got a baby ilikemea mimba za utotoni.

A letter to my unborn child anatoa ramani kwa mtoto anaezaliwa kuwa mmarekani mweusi kwa magumu inayobidi ajiandae kuyapitia pamoja na kuwaasa waepukane na maisha ya usela ili kuepukana na hatari za kwenda jela ama kufa.

Keep ya head high ni bonge la postive inspiration kujua thamani yako.

Wonder why they call you bitch ilitoa darasa kwa dada zetu tabia za kujiepusha ili wasijishushe thamani.

2pac nae alikuwa muhuni japo ilikuwa ni mpaka umchokonoe, Biggie aliwahi kumtesti kilochotokea 2pac alimchapia dem wake na kumtolea diss track iliyovunja rekodi - hit em up.

hizo ni chache tu.........

RDT_20230926_1023153435585868002972009.png

1b4858fbd24046a81cace5ee18d19c868262b91f.jpeg


Ukija kwa Notorious Big, kwanza kabisa anadanganya kwamba aliishi maisha magumu wakati kiuhalisia hakulelewa maisha ya kitajiri ila sio haba aliishi maisha walau ya kati, mama yake alikuwa na kazi ya ualimu, Big alisomeshwa shule private, aliishi mitaa yenye hadhi ya wastan hakuishi hood kama 2pac, n.k. hali yake ilimpa wepesi kujuana na kina pdiddy, mama yake alikuwa anachukia sana kamlea vizuri ila yeye anadanganya kakulia kwenye shida

Big nyimbo kibao kajivika uhusika wa jina lake kuwa mkatoli asie na huruma (Notorious) pamoja na kujibrand zaidi zaidi kama muuza madawa ya kulevya.

anaimba kubrag (kujisifia) ana mkwanja, kuua, kupora, kupiga, n.k. sambamba na kudanganya kwamba aliishi magumu sana, aliacha shule akiwa na miaka kumi, n.k.

Big ufalme wake upo kwenye ku flow kama maji, kwakweli flow zake zina ladha tamu masikioni hata kama hujui lugha una enjoy kusikiliza, kumbuka shuleni alifanya vizuri zaidi somo la kiingereza huenda hii ilisaidia kujua kupanga maneno kwenye flow zake, kazi zake kama ten crack commandments anafundisha namna ya kuuza madawa lakini anavyo flow kama maji waweza kuweka kando ujumbe wake ujikite na flow yake, kazi nyingine kama big poppa kaimba pombe na milupo lakini huchoki kumsikiliza anavyo flow kama maji, aliwahi pia kufanya kazi na eminem - dead wrong kwa hakika aliflow kama maji japo ujumbe wake ni kubaka, kuwapora wanawake, kupiga wanamke na kuua kikatili.

Wayakuja watu kusema kazi zake za juicy na sky is the limit zina ujumbe, huo ujumbe ni upi ?

Juicy kaweka wazi mafanikio aliyopata kwenye mziki yamempa mkwanja wa kufanya umalaya na kupiga pamba kali, sioni cha kuelimisha hapo.

Sky is the limit humo kaendeleza uongo wake kwamba alikulia maisha ya kimasikini, kasifia kwamba kuuza madawa ya kulevya kuna mkwanja, hakuishia hapo alidanganya kwamba aliacha shule akiwa na miaka 10 ili auze madawa, n.k.
 
Now I'm lost and I'm weary, so many tears
I'm suicidal, so don't stand near me
My every move is a calculated step to bring me closer
To embrace an early death, now there's nothin' left

There was no mercy on the streets, I couldn't rest
I'm barely standin', bout to go to pieces, screamin', "peace"
And though my soul was deleted, I couldn't see it
I had my mind full of demons tryin' to break free

They planted seeds and they hatched, sparkin' the flame
Inside my brain like a match, such a dirty game
No memories, just a misery
Paintin' a picture of my enemies killin' me in my sleep

Will I survive til the mornin' to see the sun?
Please Lord, forgive me for my sins, 'cause here I come
 
Asili ya hip hop ni braggin, ila vijana wa NY ni next level, mistari yao ni bata, madem, vileo, hustlin. fatilia kuanzia Notorious, diddy, rakim, shawn cartel, Nas.

The bronx, brokylin, queens, manhattan. Utaimba nini hapo mzee?

By the way si kila muda mtu utataka kusikiliza revolutions.

#eastside4life
 
Asili ya hip hop ni braggin, ila vijana wa NY ni next level, mistari yao ni bata, madem, vileo, hustlin. fatilia kuanzia Notorious, diddy, rakim, shawn cartel, Nas.

By the way si kila muda mtu utataka kusikiliza revolutions.

#westside4life
Mzizi mkuu wa hiphop ni kuelimisha jamii....

Braggin (kujisifu) ni vitu extra tu kama ilivyo kucheza
 
Big was a typical street boy...

Big was doing it for money..

Big was a hustler and a true inspirational story for anyone who wants to change their story...

Pac was a Legend from politics to motivation and to a game changer .
Umemaliza kila kitu mkuu.

Nadhan mkuu sky soldier anatakiwa ajue pac na biggie ni watu wawili tofauti.

Wakati 2pac amelelewa na watu wa revolutions na political movement hata mziki wake ulibase huko unlikely notorious jamaa by nature ni street hustler, ambaye yupo tayari kuhustle kwa namna yoyote ili apate anachotaka hii ndo kitu inatuinspire wengi na hii ni nature ya vijana wengi wa new york, angalia rappers wengi waliokulia mitaa ya brooklyn, bronx, queens wanafanana hizo characters.

Refer kwanini carter na diddy wanaexist mpaka saizi ni watu wa deals nyingi na kuna mambo mengi wanayafanya nyuma ya pazia.
 
Umemaliza kila kitu mkuu.

Nadhan mkuu sky soldier anatakiwa ajue pac na biggie ni watu wawili tofauti.

Wakati 2pac amelelewa na watu wa revolutions na political movement hata mziki wake ulibase huko unlikely notorious jamaa by nature ni street hustler, ambaye yupo tayari kuhustle kwa namna yoyote ili apate anachotaka hii ndo kitu inatuinspire wengi na hii ni nature ya vijana wengi wa new york, angalia rappers wengi waliokulia mitaa ya brooklyn, bronx, queens wanafanana hizo characters.

Refer kwanini carter na diddy wanaexist mpaka saizi ni watu wa deals nyingi na kuna mambo mengi wanayafanya nyuma ya pazia.
2pac wazazi wake walikuwa wanaharakati lakini alilelewa na mama yake pekee ambae nae alianza kutumia madawa ikamlazimu 2pac kukuzwa na bdugu zake ambao nao walikuwa wanaharakati, hata huko kwa ndugu zake alihama hama maana walikuwa wanafungwa na serikali kwa kupigania haki.

Biggie huyo huwezi kumuita hata street boy, alilelewa vizuri tu ila ni yeye mwenyewe alitaka kuuza madawa si kwasababu hakukuwa na hela ila kwasababu ni yeye alitaka.

Pia big kasoma mpaka high school msije mkadhani aliacha kusoma akiwa na mjaka 10 kama alivyodanganya kwenye sky is the limit, kasomeshwa private ila ni yeye mwenyewe alipofika high school alimuomba mama yake asome shule public, huko ndiko alihamasika zaidi kuuza madawa.

Kuhaso kwa kuuza madawa kumewaweka wamarekani weusi kibao nyuma ya nondo, Big kusifia kuhaso kwa kuuza madawa haikuwa sawa.
 
Big was a typical street boy...

Big was doing it for money..

Big was a hustler and a true inspirational story for anyone who wants to change their story...

Pac was a Legend from politics to motivation and to a game changer .
Biggie hakuwa street boy, alidanganya kaishi maisha ya mtaani, pia alidanganya kwenye sky is the limit aliacha shule akiwa na miaka kumi aende kuuza madawa, big sio wa kumuamini kila kitu.

Big kuwa hustler nayo kadanganya kwamba alikuwa anakula dagaa (sardines)

Hii itakuws ilimuumiza sana mama yake aliejitoa sana kumpa big maisha mazuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom