2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Kwanza Argentina hakupangwa kundi dhaifu bali juhudi zake za kushika nafasi ya kwanza zimemfanya awakwepe vigogo. Hiyo timu unayo ishabikia wewe Ureno, ilipangwa na timu zipi tuanze kwenye Rank za FIFA, tusiongee kwa hisia? Maana hata Ureno angeshika nafasi ya kwanza,basi robo ndio angekutana na timu ngumu ambayo ni Argentina, sasa yeye mwenye kashika nafasi ya pili sasa tutamsaidiaje wakati kazembea mwenyewe.Halafu kwenye michuano hii, timu gani ilipagwa kwenye kundi gumu? Utasema trend najua nyie timu CR7,okay Colombia kashika nafasi ya kwanza, kakutana na Ghana, then akatolewa na Uswizi, Uswizi akakutana na Argentina akapigwa.Okay kwa Trend hii Ureno kama angeshika nafasi ya kwanza si alikuwa anajipigia, ila yy mwenyewe kazingua.
Wapinzani wa Argentina
HatuaMpinzani FIFA Ranking
Kundi JAlgeria28
Kundi JAustria24
Kundi JJordan63
Hatua ya 32Cape Verde67
Hatua ya 16Misri29
Robo FainaliUswisi19


Niambie ni mwaka upi ambao kombe la dunia lilifanyika na ikatokea timu moja inafika robo fainali bila kukutana na timu yeyote kutoka kumi bora ya FIFA ranking?
 
Back
Top Bottom