2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Mjadala wa nani GOAT utatamatika leo.

FB_IMG_1784113650844.jpg
FB_IMG_1784113652900.jpg
 
Mnaacha kushabikia morocco mnakimbilia kwa wanariadha kisa eti timu imejaza weusi 😄 aibu gani hii!!

Germany out
Brazil out
Portugal out
Senegal out
France out
Cape Verde out
Netherlands out
Uswis out
Bado england yenu yenye rashford😄 ndio tumaini lenu sio! Au tunaenda na Argentina Saint Anne
Morocco ni mdudu gani?
Heri nisishabikie kabisa mpira kuliko kushabikia Morocco.

England tuna jambo letu
Rashid mpemba unamjua lakini akiamua?
Saka unamjua lakini?
Bellingham
Ukija kati unamkuta Hendo
Amekosekana tu Babe wangu Trent Alexander Arnold 🔥
 
Kwa hiyo unavyodhani wewe unahisi habari iliyowekwa na CBC inapingana na hoja yangu?
Kuna sehemu CBC wameripoti hiki ulicho kiandika ww?

"Siku 9 kabla ya fainali FIFA na viongozi wa AFA walisaini mkataba wa mabilioni ya fedha yakitumwa kwenye account ambayo sio ya shirikisho la AFA (hii ni big point)"

Unaweza nioneshea kwenye,kama ww ulikiona.
 
Swali hujajibu, umejitengenezea swali ambalo umeona ni rahisi halafu ndio umelijibu.

Mimi sijahoji kama Argentina hajawahi cheza na Giant kwenye hiyo miaka 17.

Hoja yangu imelenga utetezi wako wa kwamba Argentina anakutana na timu dhaifu kwasababu inanufaika kupitia matunda ya kuongoza kundi.

Ndio maana nikahoji, katika historia ya miaka 17 ya kombe la dunia ni timu gani nyingine ambayo iliwahi kunufaika kwa kuongoza kundi na kufaidi matunda ya kucheza hadi robo fainali bila kukutana na timu ambazo zipo top ten ya ranking?
Kunafaika vipi, hamna kunufaika ni matokeo ya uwanjani,ndiyo yanayo determined utakutana nani. Argentina kama angekuwa na matokeo mabovu angekuta na Spain round ya pili? au may be angeshika nafasi ya pili kwako ndio ungeamini hapendelewi.

Hoja zako hazieleweki unazungumzia hisia unasahau kinacho tokea uwanjani.
 
Msimu huu England hajakutana na top ten
 
Kuna sehemu CBC wameripoti hiki ulicho kiandika ww?

"Siku 9 kabla ya fainali FIFA na viongozi wa AFA walisaini mkataba wa mabilioni ya fedha yakitumwa kwenye account ambayo sio ya shirikisho la AFA (hii ni big point)"

Unaweza nioneshea kwenye,kama ww ulikiona.
CBC hawajaripoti hiyo quote

Wakati CBC inaandika hiyo habari hakukuwa na nyaraka za siri zilizovuja.

Nyaraka za siri zilikuja kuwa leaked na Romain Molina huyu ndio ameongea mengi ikiwemo sakata la unyanyasaji wa kijinsia ambalo mimi nimeliainisha hapo juu ambalo pia huwezi kulikuta kwenye CBC wala Lanacion ambayo ndio primary source wa hii habari.

Kwa hiyo hoja yangu bado inakuwa ni ya kweli ila haipatikani katika chanzo chako hicho ambacho unakirejea.
 
Kunafaika vipi, hamna kunufaika ni matokeo ya uwanjani,ndiyo yanayo determined utakutana nani. Argentina kama angekuwa na matokeo mabovu angekuta na Spain round ya pili? au may be angeshika nafasi ya pili kwako ndio ungeamini hapendelewi.

Hoja zako hazieleweki unazungumzia hisia unasahau kinacho tokea uwanjani.
Kwa hiyo matokeo ya uwanjani ndio yameanza kwa mara ya kwanza kuonekana msimu huu?

Kivipi katika miaka 17 kusiwe na scenario kama hii ya timu moja kufika nusu fainali ikiwa haijacheza na timu kubwa kwenye top ten?
 
Mtani uran haya niambie leo tabiri zako zinasemaje.

Au tuweke dau basi. 😂😂😂
Mtani leo hali sio hali.
Timu ninayoipenda zaidi England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 inacheza na Timu nisiyoipenda kabisa.

Yaani leo kwangu Mpira kumoyo.

Nashangaa sina wasiwasi kabisa.
England anaenda kuifurahisha Dunia.
 
Back
Top Bottom