2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

🏆 FIFA World Cup 2026 Finals Uzi Maalum.

2026 FIFA World Cup itakuwa toleo la kihistoria la Kombe la Dunia kutokana na mabadiliko makubwa katika mfumo wa mashindano.

🌍 Waandaaji

Mashindano yataandaliwa kwa pamoja na:

United States
Canada
Mexico


Hii ni mara ya kwanza World Cup kuandaliwa na nchi tatu kwa pamoja.

👥 Idadi ya Timu
Timu 48 zitashiriki (badala ya 32).
Jumla ya mechi zitakuwa 104.
Hii ndiyo World Cup kubwa zaidi kuwahi kufanyika.

⚽ Mechi ya Ufunguzi
View attachment 3586820

Mechi ya ufunguzi itachezwa katika Estadio Azteca, Mexico City.
Uwanja huu utaweka historia kwa kuwa wa kwanza kuandaa mechi za ufunguzi za World Cup mara tatu (1970, 1986 na 2026).

🏟️ Fainali

Fainali itachezwa tarehe 19 Julai 2026 katika Uwanja MetLife Stadium, New York City.

Thread Hii Itahusu

Ratiba na viwanja
●Timu zilizofuzu​
●Takwimu na historia​
●Habari muhimu za mashindano​
●Mjadala wa kila hatua hadi fainali​
Hii Hapa Ratiba ya Group Stage.​
Inaanza Tarehe 11.06.2026 hadi Tarehe 27.06.2026...​
Karibu kwenye special thread ya FIFA World Cup 2026 Finals! 🌍🏆
Hii ndio orodha ya waamuzi wote wa FIFA 2026. Yule refa wenu wa mchongo wa Fainali ya CAF kati ya Senegal na Morocco ametupwa nje. Na kati yao hakuna hata mtanzania mmoja, hata linesman hakuna:
 
1000788991.jpg
 
Back
Top Bottom