2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

Ishu ya BEST LOSERS!!

Hao "best losers" (ambao rasmi wanaitwa timu bora za nafasi ya tatu) wanapatikana kwa kuwekwa kwenye msimamo mmoja wa pamoja (single table) unaojumuisha timu zote 12 zilizomaliza nafasi ya tatu kwenye makundi yao.Ili kupata timu 8 bora zitakazofuzu kwenda hatua ya mtoano (Raundi ya 32).

FIFA inatumia vigezo vifuatavyo kwa mfuatano ili kuzitofautisha:Idadi ya Alama (Points): Timu zenye alama nyingi zaidi kwenye mechi zao za makundi zinawekwa juu. (Kwa kawaida, timu ikifikisha alama 4 inakuwa imefuzu moja kwa moja).

Tofauti ya Magoli (Goal Difference): Kama zinalingana alama, inaangaliwa timu yenye tofauti nzuri ya magoli ya kufunga na kufungwa (GD) katika mechi zote za kundi.

Magoli ya Kufunga (Goals Scored): Kama bado zinalingana, timu iliyofunga magoli mengi zaidi kwenye hatua ya makundi inasogea mbele.

Nidhamu Uwanjani (Fair Play Score): Kama zinalingana kila kitu, zinaangaliwa kadi walizopata. Kila kadi ya njano au nyekundu inakatwa alama (kadi chache za njano/nyekundu ndio ushindi).

Nafasi ya FIFA (FIFA World Ranking): Kama vigezo vyote juu vimeshindwa kuzitenganisha, timu yenye nafasi ya juu zaidi kwenye Viwango vya Ubora vya FIFA ndio inayofuzu.
asante kwa ufafanuzi mkuu.
 
IMG_0631.jpeg
 
Back
Top Bottom