2025 na mbeleni

Reaction ya Watanzania baada ya uchaguzi ilitosha tu kukujuza kuwa CCM ni chama cha namna gani. Watanzania hawakuwa na si wajinga kama unavyoamini wewe....

Nenda kaangalie waliojitokeza kupiga kura ndio utafedheheka. Unawatumia wingi wa watanzania kama vile kutokuandamana ndio kuridhika na utawala wa hawa wezi wa kura na wamwaga damu. Kwa taarifa yako Iddy Amini aliuwa waganda hapo Uganda mpaka akachoka, na hakuna hata mmoja aliandamana.

Kwa huu mfano wako mfu kwakuwa waganda hawakuandamana kutokana na kuuliwa na Idd Amini, basi ni ishara kuwa waliridhika na utawala wake. Kama barabara ndio hitaji pekee la wananchi, Nyere na watanzania kwanini tulipoteza nguvu na mali zetu kiwapigania weusi wa Afrika kusini wakati wazungu walijenga miundombinu mara 1,000 ya hii ya kwetu ya mikopo?

Na napenda ufahamu kuwa ccm sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha dola kilichojivika koti la chama cha siasa. Naona unalazimisha kuwa ccm ni chama cha siasa wakati uhalisia hauonyeshi hivyo.
 
Hukuelewa kauli hiyo! Alimaanisha, baada ya kuwa katibu mkuu, hata taka uteuzi mwingine wa kuongezewa hapo (kwa kingereza - concurrently). Ukikumbuka, baada ya hapo watu wengi walinyanganywa vyeo vingine wakabaki na kimoja!

Kauli yake ilikuwa wazi, sidhani kama inahitaji huu ufafanuzi wako. Kama utaratibu huko CCM ni kuwa na cheo kimoja, kwanini Rais ni Mwenyekiti wa CCM?
 

Bado. Huwa nawaona makada ndani ya kijani wakiwa katika makundi maeneo ya ofisi za chama na maeneo ya shughuli maalum huku polisi wakiwa jirani.

Wakitawanyika baada ya shughuli, sare nazo kutoweka kinamna. Si rahisi kumuona mwanaCCM akizurura peke yake na hizo sare mbali na maeneo ya chama au hata ndani ya vyombo vya usafiri wa umma kama dala dala.

Nasema uongo mkuu?
 
Kubadili mawazo si sawa na kubadili katiba!

Get it nyumbu?
Marekani waliweka term limit zaidi ya miaka 150 baada ya kujitawala. Nini hasa ulikuwa msukumo kuweka huo ukomo wa mihula miwili?

Kwa mtazamo wangu, kuweka ukomo ni uminywaji demokrasia kwa kuwanyima haki wananchi kuchagua wampendaye.
 
Sijaelewa ni kwanini kuna watu wanauhusisha uteuzi wa Dkt. Bashiru kuwa katibu mkuu kiongozi na Rais Magufuli kuongeza muda kuiongoza Tanzania kwa zaidi ya mihula miwili...
Hujui kitu au ukabila umekupofusha
 
Mkuu, maneno ya Bashiru sio katiba isipokuwa la Rais kuongezea/kuongezewa muda ni la kikatiba
 
Mkuu, maneno ya Bashiru sio katiba ispokuwa la Raisi kuongezea/kuongezewa muda ni la kikatiba
Magufuli anajali katiba gani, kama angekuwa anaogopa katiba angeweza kupokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha? Ama hujui kuwa katiba imelitenga jeshi na siasa?
 
Magufuli anajali katiba gani, kama angekuwa anaogopa katiba angeweza kupokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha? Ama hujui kuwa katiba imelitenga jeshi na siasa?
Kwa hiyo haina haja ya kuendelea kupiga kelele za yeye kuongeza muda wa utawala Kwa kuwa katiba si kigezo cha yeye kuamua atakalo siyo?
 
May be hujawaelewa wanaolihusisha hilo swala la uteuzi wa Bashiru na Jiwe kutaka kuongeza muda.

The issue ni kuwa, Bashiru amenukuliwa mara kibao akikataa hilo suala kwamba rais hana nia hiyo na kwamba rais ataheshimu muda wa mihula miwili na Bashiru anaonekana hayuko enthusiastic na idea ya kuuongezea rais muda.

Sasa kwa rais ambaye akilini mwake ni kweli anataka kujiongezea muda ila anazuga tu kwa sasa kuendelea kuwa na katibu mkuu wa chama ambaye hataki kabisa idea hiyo atakuja kuwa kikwazo chamani huko mbeleni. Kwa hiyo unamfanyaje katibu mkuu wa aina hii?, Huyu unamuondoa kisailensa chamani unaweka mtu ambaye hatakuwa kikwazo ndani ya chama huko mbeleni pindi ukiamua kulianzisha hilo swala la kujiongezea muda!
 
Mkuu tatzo hata huyu Bashiru yeye mwenyewe haaminiki alisema hatakubali cheo kingine baada ya huo ukatibu mkuu wa CCM,Sasa Kama yeye mwenyewe ameshindwa kukiishi kiapo chake je huyo jiwe? So uhakika wa jiwe kuongeza miaka Ni 90%
 
Magufuli yeye hajanukuliwa akisema hataki mambo ya kumuongezea muda?
 
Magufuli yeye hajanukuliwa akisema hataki mambo ya kumuongezea muda?
Huyo haaminiki, siyo wa kumuamini maana ameshaahidi vitu kibao only kuja kuvikana baadae, mara kadhaa amekana hata kiapo akichokula cha kuilinda na kuihifadhi katiba na kutawala kwa mujibu wa sheria kwa kufanya kinyume cha vitu hivyo, sasa huyo wa kumuamini kwa kauli yake? - Kwa Magufuli nakushauri uangalie trend ya matendo yake na si kauli zake, he is ureliable, you cant take him for his word!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…