Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 25,012
- 56,294
Habari wakuu…
Michuano ya Kombe la Vilabu la Dunia imewadia, ambapo vilabu 32 kutoka mabara tofauti vitapambana kumsaka bingwa kuanzia Juni 14 mpaka Julai 13 nchini Marekani.
Hii ni format mpya ambapo itaanza kutumika mwaka huu na michuano hii itakuwa inafanyika kila baada ya miaka minne.
Afrika tutakuwa na timu 4 ambazo ni Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Wydad pamoja na Esperance.
Bara la Ulaya timu 12 ambazo ni PSG, Real Madrid, Man City, Atletico Madrid, Bayern Munich, FC Porto, Chelsea, Benfica, Borussia Dortmund, Inter Milan na Juventus.
Hakuna nafasi kwa timu kama Barcelona, Liverpool, Arsenal na nyinginezo kwakuwa vigezo vimewabana. Kwa ulaya hakuna nchi inayotoa zaidi ya vilabu viwili.
Bara la Asia nao watakuwa na timu 4, Amerika ya Kaskazini timu 4 na kule Amerika ya Kusini timu 6, huku Oceania ikitoa timu 1 na wenyeji wakiwa na ofa ya timu 1 ya ziada ambayo ni Inter Miami ya Lionel Messi.
Timu hizo 32 zimepangwa kwenye makundi manane yenye timu nne kwa kila kundi. Hivyo timu zitaanza kucheza mechi za makundi, kisha mbili za juu kila kundi zitaenda 16 bora, robo fainal, nusu kisha Fainal.
Jumla ya viwanja 12 vitatumika huku mchezo wa ufunguzi ukipigwa katika dimba la Hard Rock Stadium ambapo Al Ahly wataikaribisha Inter Miami ya Messi kule Miami.
Mchezo wa Fainali utapigwa kule Metlife Stadium mjini New Jersey na utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 82,500.
Bingwa wa michuano hii atabeba Kombe pamoja na kitita cha Euro Million 140 sawa na Shilingi Bilioni 13 na Milioni 476. Kwa maana nyingine Kombe hili lina hela nyingi kuliko Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Changamoto ni masaa ya Marekani kupishana sana na masaa ya huku kwetu, kuna mechi zitapigwa saa 9 usiku, Saa 11 alfajiri lakini pia kuna mechi zitapigwa Saa 1 usiku na Saa 4 usiku walau hizi zitakuwa na nafuu.
Live updates zitakujia hapa kuanzia ratiba za mechi, muda, viwanja nk. Michezo hii itakuwa mubashara kupitia AzamTv, DStv, Canal Sports nk