2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency



Viunganishi

Ruka hadi maelezoAccessibility Help

Uongozaji BBC

Menyu

Tafuta katika BBC

Swahili navigation

Yaliyomo

Matokeo Marekani 2016: Trump amshinda clinton majimbo muhimu

Dakika 58 zilizopita

Mshirikishe mwenzako

Image copyrightAP

Wagombea urais wawili wakuu wa urais Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wanakaribiana sana katika matokeo ya uchaguzi wa urais katika majimbo muhimu yanayoshindaniwa.

Clinton ameshinda Virginia naye Trump akashinda Ohio, Florida, na North Carolina.

Kwa sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Lakini mgombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Chama cha Republican kinaonekana kuwa njiani kuhifadhi wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.

Image copyright@REALDONALDTRUMP / TWITTERImage captionDonald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.

Kama ilivyotarajiwa, Bw Trump ameshinda katika ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma na Texas, ABC News wanakadiria.

Trump v Clinton: Nani anaongoza?Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?Trump na Clinton sako kwa bako Marekani

Bw Trump pia anakadiriwa kushinda Arkansas, Kansas, North Dakota, South Dakota, Montana na Wyoming.

Shirika hilo linakadiria Bi Clinton atashinda ngome za Democratic majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia.

Mshindi anahitaji kupata kura 270 kati ya jumla ya kura 538 za wajumbe ndipo atangazwe mshindi.

Image copyrightREUTERS

Upigaji kura umemalizika katika majimbo 39 na matokeo kamili yalitarajiwa mwendo wa saa 23:00 EST (04:00 GMT Jumatano - Saa moja asubuhi Afrika Mashariki), upigaji kura utakaomalizika Pwani ya Magharibi.

Matukio mengine makuu:

Bodi ya Uchaguzi Carolina Kaskazini imekubali kuongeza muda wa kupiga kura maeneo manane wilaya ya Durham ambapo kuna milolongo mirefu ya wapiga kura.Mgombea wa Republican aliyeshindwa kwenye mchujo Marco Rubio amehifadhi kiti chake cha useneta FloridaThamani ya pesa za Mexico, peso, imeshuka sana baada ya Trump kuonekana akiongoza FloridaMtu mmoja alifariki kwenye ufyatulianaji wa risasi karibu na kituo cha kupigia kura jimbo la Azusa, California. Watu watatu walijeruhiwa.

Bw Trump, tajiri kutoka Manhattan, na Bi Clinton, anayetaka kuwa rais wa kwanza mwanamke Marekani, walipiga kura mapema Jumanne katika jiji la New York.

Mwongozo wa matukio makuu uchaguzi Marekani

Bw Trump alizomewa alipofika kupiga kura yake Manhattan, akiandamana na mkewe, Melania, na bintiye, Ivanka.

Wawili hao wamekuwa wakifuatilia matokeo kutoka jiji la New York.

Image copyright@HILLARYCLINTON / TWITTERImage captionClinton amepakia picha hii, pamoja na ujumbe wa shukrani kwa watu wote, licha ya matokeo ya usiku wa leo

Bi Clinton atahutubia wafuasi Javits Centre, Manhattan naye Bw Trump atahutubu katika hoteli ya Hilton Midtown.

Maafisa wa polisi zaidi ya 5,000 wametumwa jijini New York kuimarisha usalama.

Utafiti wa maoni wa baada ya upigaji kura, uliofanywa na ABC News, unaonyesha wapiga kura 61% hawampendi Bw Trump nao 54% ndio hawampendi Bi Clinton.

Mapema Jumanne, Bw Trump kwa mara nyingine alikataa kusema iwapo atakubali matokeo.

"Tutaangalia tuone vile mambo yatakuwa," aliambia Fox News, huku akidai kwamba kumekuwa na kasoro hapa na pale kwenye uchaguzi.

"Ninataka kila kitu kiwe wazi."

Katika baadhi ya vituo, mitambo ya kupigia kura ilifeli na kwingine kukawa na milolongo mirefu, lakini yalionekana kuwa matatizo ya kawaida.

Bw Trump, aliyezua utata kuhusu kuaminika kwa shughuli ya uchaguzi kwa kudai kura "zitaibwa" mapema, pia amewasilisha kesi ya dharura Nevada.

Maafisa wa Republican wamemshtaki msajili wa wapiga kura wilaya ya Clark, wakidai jimbo hilo lilifungua vituo vya kupigia kura muda mrefu kuliko inavyofaa.

Lakini jaji ameitupilia mbali kesi hiyo.

Kando na kura za urais, Wamarekani wamekuwa pia wakipiga kura za Maseneta, wabunge wa Bunge la Wawakilishi na Magavana.

Viti vyote 435 Bunge la Wawakilishi vilikuwa vinashindaniwa, na ABC News wanakadiria kwamba bunge hilo litabaki chini ya udhibiti wa Republican.

Lakini theluthi moja ya viti Seneti, ambao Republican wamekuwa wanaongoza, pia vinashindaniwa, na Democratic wanatumai wanaweza kudhibiti bunge hilo.

Jumla ya Wamarekani 45 milioni, idadi kubwa zaidi kuliko awali, walijitokeza kupiga kura mapema.

Bw Trump na Bi Clinton wanapigania kumrithi Barack Obama wa Democratic.

Rais Obama haruhusiwi kuwania kikatiba baada ya kuhudumu mihula miwili ya miaka minne.

Rais mpya ataapishwa tarehe 20 Januari 2017.

Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

EmailFacebookMessengerTwitterWhatsApp

Rejea mwanzo wa ukurasa

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Wanawake wanavyokaribia kutawala dunia

8 Novemba 2016

Bill Clinton ataitwa nani Hillary akishinda?

1 Novemba 2016

Mwongozo wa matukio makuu uchaguzi Marekani

8 Novemba 2016

Hillary Clinton atabahatika mara ya pili?

18 Oktoba 2016

Gumzo mitandaoni



Ashinda kesi ya kuitwa Zebra





Mwanamfalme Harry athibitisha mpenziwe



Shimo kubwa lameza barabara nchini Japan





Marekani yaamua: Trump, Clinton na Bangi



Wanawake wanavyokaribia kutawala dunia





Nguo ya ndani ya mke wa Hitler yapigwa mnada



Diamond Platinumz ashinda tuzo 3 za Afrimawards Nigeria





Wezi waiba mtambo wa ATM Nairobi



Canada yachunguza kelele za ajabu kutoka bahari ya Arctic

Habari zilizosomwa zaidi

1Trump mbele ya Clinton majimbo muhimu Marekani
 
Magufuli wa marekani anatoboa jamani hakika wamarekani hawata acha kuisoma number
 
Kwani kwa sasa tunajitawala mkuu?
Huoni tunavyotawaliwa!!!!
Bora mtawala awe sii miongoni mwetu itaturudishia umoja wetu.

ONA SAMWELI SITA ANAVYOVURUMISHIWA MANENO AKIWA KWENYE JENEZA.

TUNATAWALIWA MKUU.
Umeongea kitu cha maana sana...SAFI
 
Mkuu tutakuwa tumerudi kwenye ukoloni,Huyu jamaa anasema akiingia ikulu basi Africa ijiandae kutawaliwa tena
Safi tu, kwani haya meusi yanatufanyia nini? Wacha jamaa lichukue halafu lihamasishe Afrika tutawaliwe tena! Umesikia mibunge ya ccm imegawana 10m kila mmoja halafu jinga moja linasema kwani kuna ubaya gani ccm kugawana fedha yao? Shenzy type kabisa, wacha tutawaliwe tu hatuna maana sisi!! Halafu mwenyekiti naye amenyamaza tu huku anajidai kuchukia ufisadi na rushwa!!! Go go go Trump!!!
 
Namuona bush katika kivuli cha trump kwa mbali akiikaribia ikulu wacha tuone
 
You can't separate trump and Putin . Hivi umesahau cyber attack iliyofanywa Na Russians kwenye dhidi ya Hillary Clinton.
Unachojua wewe ni kipi ukilete hapa?
 
MATOKEO HADI KUFIKIA SAA 8:30 ASUBUHI E.A TIME

Electoral votes Clinton 215 while 50,942,017 (47.2%) popular votes

Electoral votes Trump 244 while 52,079,143 (48.2%) popular votes

In order to win election that candidate must acquire 270 electoral votes

Matokeo haya yanaendelea kushangaza kula za maoni, wengi walivyotegemea imekuwa sivyo.
Kwa vile ni kula za maoni wala hainishangazi. Lakini zingekuwa kura za maoni ningeshangaa kidoòoogo!!!!
 
Hauko sahihi. Trump alimshambulia Obama kwa kumsifu Putin kutokana na Obama kuruhusu Putin kufanya anavyotaka kule Cremea na Syria lkn km Trump ataingia atamfurusha Putin popote alipo kwa nguvu zote unaweza kukumbuka kituo kikubwa cha mabomu mazito cha Poland alichojenga Bush. Sasa Trump atavijenga vingi sn yote hiyo ni kuibana Urusi
Unamzungumzia Trump wa zamani huyo lakini sio wa sasa! Trump wa sasa role model wake ni Putin and the reason behind ni ISIS! Kwa Trump, Obama na timu yake wanawalea lea ISIS kwavile goal yao ni kumuondoa Assad madarakani wakati goal ya Trump inaendana na Putin... yaani kuwafyekelea mbali ISIS! Na ndio maana wiki chache zilizopita, "wahuni" walipoweka banner ya Putin kwenye daraja ya Manhattan, ikahisiwa waliofanya hivyo ni Trump Supporters!
Putin.png
 
Kwa mama hirari Kama Kuna msiba asee kumepoa Sana naona wengine wanatoa machozi
 
Trump akichukua tu Pennsylvania tayari ni rais wa Marekani japo mchuano ni mkali ila kinachoshangaza Pennsylvania huwa ni koloni la hawa Democrats ila uchaguzi huu Repulican wanaongoza

238+20 za Pennsylvania basi Hapo Potus ni Donald Trump na kama pia atatoboa Michigan basi tena Hilary
 
Mhhhhhhh itabidi uniambie jina lako faragha aiseee,same here (niko na jina la kiarab)

Nilimuambia mtu hivi asubuhi hii,ndoto kushney [emoji17]
[emoji3] [emoji23]

Ila mimi afadhali kidogo Surname iko neutral labda wanaweza kunihurumia ila first name wazee walikomesha utasema nimeshuta toka Oman [emoji23]
 
Safi tu, kwani haya meusi yanatufanyia nini? Wacha jamaa lichukue halafu lihamasishe Afrika tutawaliwe tena! Umesikia mibunge ya ccm imegawana 10m kila mmoja halafu jinga moja linasema kwani kuna ubaya gani ccm kugawana fedha yao? Shenzy type kabisa, wacha tutawaliwe tu hatuna maana sisi!! Halafu mwenyekiti naye amenyamaza tu huku anajidai kuchukia ufisadi na rushwa!!! Go go go Trump!!!
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom