2016 US Election Results: Donald Trump has won the presidency

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,009








Nevada judge denies Trump request to separate early voting ballots

Washington (CNN)A Nevada court judge denied a request Tuesday from Donald Trump campaign lawyers to issue an order directing a county registrar of voters to preserve and separate ballots from voting machines in four early voting sites in Clark County, Nevada.

In legal briefs filed Monday night, Trump lawyers had asked for an order to have the pertinent early vote ballots not to be "co-mingled or interspersed" with other ballots after the campaign alleged the county registrar kept polling locations open beyond their designated hours.

Judge Gloria Sturman, of the District Court for Clark County Nevada, ruled from the bench, saying County Registrar of Voters Joe P. Gloria was already obligated by state law to maintain the records that the Trump campaign is seeking.
The judge at times expressed frustration with Brian Hardy, a lawyer for the Trump campaign.

"I am not ordering him (Gloria) to preserve anything," she said, adding, "This is Election Day. He has other things to be doing."

The Trump campaign had said Gloria kept polling locations open "two hours beyond the designated closing time." The lawsuit targeted polling places in the greater Las Vegas area that have larger minority voting precincts.


=========

UPDATE

Clinton ameshinda Virginia naye Trump akashinda Ohio, Florida, na North Carolina.

Kwa sasa Trump ana kura 244 za wajumbe na Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.

Lakini mgombea wa Republican Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.

Chama cha Republican kinaonekana kuwa njiani kushinda wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.

UPDATE 2

Donald Trump ameshinda nafasi ya Urais kwa kuvuka idadi ya kura za wajumbe apata kura za wajumbe 289. Clinton 218.

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.


Mfahamu Rais mteule wa Marekani, Donald Trump

Donald John Trump alizaliwa Juni 14, 1946 Jamaica Estates, Queens karibu na New York. Ni mtoto wa pili kati ya watoto watano wa Fred Trump na Mary. Ndugu zake watatu; Maryanne, Elizabeth na Robert wako hai wakati kaka yake mkubwa, Fred Junior alifariki mwaka 1981 kutokana na unywaji pombe wa kupitiliza. Donald anasema jambo hilo ndilo lililomfanya yeye kujiepusha na pombe na uvutaji sigara.

Baba yake Trump kwa asili ni Mjerumani wakati mama yake asili yake ni Scotland. Bibi na babu zake Trump wote ni watu waliozaliwa Ulaya. Jina lao la asili la Kijerumani ni Drumpf baadaye katika karne ya 17 ndiyo likawa Trump. Trump anasema anajivunia asili yake.

Trump alizaliwa na kukulia mjini New York, alipata shahada yake ya kwanza ya uchumi katika shule ya uchumi ya Wharton ya Chuo Kikuu cha Pennyslvania mwaka 1968.

Mwaka 1971 alikabidhiwa udhibiti wa kampuni ya ujenzi ya baba yake Fred Trump ambayo baadaye aliibadilisha jina na kuiita The Trump Organization. Trump ni mwenyekiti na Rais wa Jumuiya ya Trump ambayo ni kampuni tanzu ya ujenzi, wadhifa ambao alisema atauacha mara atakapochaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

Katika sekta ya ujenzi Trump amejenga ofisi, hoteli, casino na viwanja vya golf katika sehemu mbalimbali.

Mwaka 1996 hadi 2015, Trump alikuwa muandaaji wa mashindano ya urembo ya Miss USA na hapo pia akawa anaonekana katika filamu na vipindi mbalimbali vya runinga.

Mwaka 2016 aliorodheshwa katika jarida la Forbes kuwa mtu wa 324 kwa tajiri duniani, lakini anashika nafasi ya 156 ya utajiri nchini Marekani.

Ujana wake

Familia ya Trump ilikuwa na nyumba ya ghorofa mbili huko Wareham Jamaica Estates ambako Trump alikuwa akiishi wakati anasoma shule ya The Kew-Forest. Kutokana na tatizo la kimaadili, Trump aliacha shule akiwa na miaka 13 na kupelekwa chuo cha kijeshi cha New york (New York Military Academy - NYMA) ambako alimaliza sekondari mwaka 1983.

Baba yake (Fred Trump) wakati alipohojiwa kuhusu tabia za mwanawe alisema: “Donald alikuwa mkorofi alipokuwa mdogo.”

Mwaka 2015 Trump alimwambia mwandishi mmoja kuwa NYMA imempa mafunzo mengi ya kijeshi kuliko mtu yeyote aliyeingia jeshini.

Trump alisoma Chuo Kikuu cha Fordhan kwa miaka miwili kuanzia Agosti 1964 na kuhamia shule ya biashara katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambacho hutoa mafunzo kuhusu usimamizi wa ujenzi. Wakati akiwa chuoni hapo alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya familia iliyojulikana kama Elizabeth Trump & Son, jina la bibi yake mzaa baba.

Mwekezaji majengo

Trump hakuandikishwa kupigana vita ya Vietnam, lakini kati ya 1964 hadi 1968 akiwa chuoni alisimamishwa masomo mara nne.

Kuanza kazi

Trump alianza kazi katika kampuni ya baba yake mara tu baada ya kumaliza chuo. Kampuni hiyo ilikuwa ikijenga nyumba za makazi na kuzikodisha huko Brooklyn, Queens na Staten Island. Mradi wake wa kwanza aliousimamia ulikuwa ni kuboresha makazi ya Swifton Village apartment huko Cincinnati, Ohio sehemu ambayo ilinunuliwa na baba yake kwa dola 5.7 milioni mwaka 1962.

Donald na baba yake walisimamia mradi huo uliokuwa na uwekezaji wa dola 500,000 na kuweza kujenga nyumba 1,200. Trump anasema wakati anahitimu chuo mwaka 1968 alikuwa na utajiri wa kiasi cha dola 200,000 (sawa na dola 1,020,000 kwa mwaka 2015).

Mradi wa kwanza mkubwa wa Trump ulikuwa ni ujenzi wa Grand Hyatt Hotel mwaka 1978.

Mwaka 1981, Trump alinunua na kukarabati jengo huko Third Avenue mjini New York ambalo kwa sasa linajulikana kama Trump Plaza.

Mwaka 1983, Trump alikamilisha ujenzi wa Trump Tower yenye ghorofa 58 iliyopo Midtown Manhattan. Mwaka 1978 wakati Trump ananunua eneo hilo na kuweka mipango yake ya ujenzi kulikuwa na sintofahamu na majirani zake, ikabidi majadiliano yawe makali kwanini anataka kujenga jengo refu na kuwanyima haki ya eneo la anga jirani zake. Majadiliano yalipomalizika mwandishi mmoja wa The New York Times aliandika: “Trump alifanikiwa kulipata eneo… huo ni ushuhuda wa jinsi alivyo king’ang’anizi na uwezo wake wa kujadili na kufikia mwafaka.

Ndoa za Trump

Trump ameoa mara tatu na ana watoto watano na wajukuu wanane.

Mke wa kwanza wa Trump alikuwa ni Ivana. Huyu alikuwa ni mwanamitindo kutoka Jamhuri ya Czech, alimuoa mwaka 1977 na kuzaa naye watoto watatu: Donald Trump Jr, Ivanka na Eric. Ndoa hii ilivunjika rasmi 1992.

Ivana alizungumza na New York Post na kusema kwa sasa yeye na Trump ni marafiki na mara nyingi amekuwa akimshauri kuhusu hotuba zake. “Tulikuwa tunazungumza kabla na baada ya mikutano yake na alikuwa akiniuliza nafikiri nini? Nami humuambia kuwa atakuwa rais mzuri kwa sababu anasema kila kitu kama kilivyo.”

Aliyekuwa mke wa pili wa Trump ni Marla Maples, alimuoa 1993 na mwaka huohuo walipata mtoto wa kike waliyempa jina la Tiffany. Marla na Trump waliachana mwaka 1999.

Mwaka 2005 Trump alimuoa mwana mitindo mwingine Melania Knauss, huyu ni mzaliwa wa Slovenia. Mwaka 2006 akawa raia wa Marekani. Wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Barron.

Melania alipoulizwa katika mahojiano na CNN alisema: “hakuna nafasi ya kufikiri mambo madogo, hakuna nafasi ya matokeo madogo. Donald hufanya vitu vifanyike.

Hata hivyo, katika hali tofauti Melania aliwahi kumfananisha Trump na mtoto mdogo kwa kusema: “Mara nyingine husema nina wavulana wawili nyumbani. Ninaye mtoto wangu mdogo na ninaye mume wangu.”

Chanzo: Mwananchi
 
(CNN)Eric Trump may have broken the law Tuesday after he tweeted a picture of what appears to be his own ballot with a vote for his father. Then he broke social media code by deleting his tweet of the ballot picture.
"It is an incredible honor to vote for my father! He will do such a great job for the U.S.A! [HASHTAG]#MakeAmericaGreatAgain[/HASHTAG]," Eric Trump wrote Tuesday morning in the tweet, with an apparent image of his ballot, which was later taken down.

Eric Trump may have broken law with ballot tweet - CNNPolitics.com
 
Masaa machache kabla ya kuanza kuiona picha ya mueleko wa uchaguzi huu. GA wanasema pia turnout ya latino ilikuwa kubwa sana siuui kama wataweza kuibadili na kwenda kwa Hillary ngoja tusubiri. Nevada, Arizona, Colorado na Florida turnout ya latino ilikuwa kubwa sana kama hii ni kweli basi njia ya Hillary kutinga tena WH safari hii si kama FLOTUS bali POTUS inazidi kuwa nyeupe.

Tayari fununu za exit polls zishaanza kuingia na Hillary yuko juu PA.
Trump yuko juu GA [so much for GA being in play], AZ, IA, NC, na OH.

Colorado, Florida, Michigan, na Nevada ni mchuano mkali...too close to call thus far.
 
Masaa machache kabla ya kuanza kuiona picha ya mueleko wa uchaguzi huu. GA wanasema pia turnout ya latino ilikuwa kubwa sana siuui kama wataweza kuibadili na kwenda kwa Hillary ngoja tusubiri. Nevada, Arizona, Colorado na Florida turnout ya latino ilikuwa kubwa sana kama hii ni kweli basi njia ya Hillary kutinga tena WH safari hii si kama FLOTUS bali POTUS inazidi kuwa nyeupe.

GA sidhani kama itaenda Dems.

Latinons sio majority ya population huko.

Ni Bubba tu [Southern boy] tu ndo aliyeweza kuibeba 1992.
 
Ni kweli latino si majority lakini participation yao kwa wingi inaweza kabisa kubadili matokeo na GA kuangukia kwa Hillary wakati hii ni Red State.

GA sidhani kama itaenda Dems.

Latinons sio majority ya population huko.

Ni Bubba tu [Southern boy] tu ndo aliyeweza kuibeba 1992.
 
Tayari fununu za exit polls zishaanza kuingia na Hillary yuko juu PA.
Trump yuko juu GA [so much for GA being in play], AZ, IA, NC, na OH.

Colorado, Florida, Michigan, na Nevada ni mchuano mkali...too close to call thus far.
Forget mchuano Nevada, Colorado, Pennsylvania,Michigan ,Florida huko Trump kushinda anahitaji miracles,even North Carolina and Ohio itakuwa ngumu sana kwa Trump kushinda, Trump anaelekea kushindwa huu uchaguzi by landslide
 
Forget mchuano Nevada, Colorado, Pennsylvania,Michigan ,Florida huko Trump kushinda anahitaji miracles,even North Carolina and Ohio itakuwa ngumu sana kwa Trump kushinda, Trump anaelekea kushindwa huu uchaguzi by landslide

Hahahaaa daaah we jamaa bana.

Hizo ni fununu za exit polls.

Siyo maneno yangu.

Sawa?
 
Back
Top Bottom