Na
Yericko Nyerere.
Ukitazama mwenendo wa chaguzi nchini, Lyatonga ali drive uchaguzi 1995 hata kama alipoteza. Mwaka 2000 uchaguzi haukuwa na mvuto kwasababu Mkapa alionesha kutosha na upinzani haukuwa na nyota alyeibuka wala chama kilichokuwa na nguvu yakufanana na NCCR ya Mrema 1995 au kuzidi pamoja na mageuzi yote ya kidemokrasia.
Mwaka 2005 Jakaya Kikwete ali drive uchaguzi ule hasa kutokana na mwamko wa sera ya vijana na siasa za upinzani kuwa kwenye mageuzi ya ndani kimfumo, Utumizi mkubwa wa pesa na rushwa ya kisiasa kushamiri.
Mwaka 2010 Dr Slaa alifanikiwa ku drive uchaguzi katika mazingira magumu kwani alikuwa anashindana na rais anaetetea nafasi yake, tofauti na Lyatonga alivyoshindana 1995 ambapo Mkapa alikuwa mpya na hakujulikana, Slaa alivutia kwasababu alikuwa anatoka chama chenye agenda, cha vijana wengi waliopuuzwa na kudhalilishwa na ccm, Chama chake cha Chadema kilichonekana mbadala na yeye mwenyewe akitokea bungeni ambako alifanikiwa sana ktk agenda ya ufisadi hivyo alikuwa tishio kwa utawala wa kijana kikavu.
Mwaka 2015 naona mashaka ndani ya ccm. Huko ccm simwoni mgombea mwenye mvuto japo nusu ya ule wa JK wa 2005, wale wote wanaojipambanua kutaka kugombea ambao ni Membe, Migiro, Lowasa, Sitta, Makamba, Pinda nk ni wahanga wa uchafuzi ulioasisiwa 2005 wakati wa kumwingiza JK madarakani. Wamejeruhiana mno.
Ukija kwenye upinzani kati ya wagombea wote vinara wa UKAWA bado mgombea mwenye nafuu ni Dr Slaa tu, Pamoja na dola kutumika kwa nguvu zote kufifisha nguvu ya Slaa kutoka 2010 hadi 2014, bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbatia au Lipumba kwasababu mbalimbali ambapo nitazichambua nipatapo wasaa,
Kwa upande wa Chadema, ujio wa rika jipya lenye nguvu ya uvuli wa ukombozi ni tunu mpya ndani ya chama hicho, Nikiwaangalia Tundu Lissu, Godbless Lema, Mch Peter Msigwa, Halima Mdee, Joseph Mbilinyi, Wenje, John Mrema, John Mnyika na wengine wengi ambao sijawataja, ni watu wenye bidii na uwezo wa kusimamia itikadi na misingi ya chama ipasavyo, pia wana uwezo mkubwa wa kiutendaji na wameshakijua chama vizuri tofuti na lile joka la mdimu (Zitto).
Slaa hana compromise na govt. Dr Slaa ama Mbowe wakiwa juu serikali itakuwa na wakati mgumu sana zaidi ya ilivyo sasa, Dr slaa anapaswa sasa asiwe anafanya kazi operational za chama badala yake anahitaji team ya watalamu wa siasa na uchumi kutoka vyuo vikuu ama wale ma expat, media na research institution pamoja na watu wenye uzoefu wa nchi kama kina Butiku, Salim, Mtei, Warioba, Jenerali Ulimwengu, Mbowe nk.
Iwe timu ya kama watu 5-10 ambao wanakutana kila wiki kumshauri na kumpa updates za nchi, Wamtengenezee agenda. Ahutubie kila mwezi kutoa mwelekeo wa nchi. Kazi za utendaji wa chama amwachie Mnyika ama kijana imara yeyote kama katibu mkuu. Wanachama na viongozi wakate rufaa kwake
Dr Slaa kwenye chama ni zaidi ya kiongozi. Ndio moyo wa chama kwasasa. Hajatengenezwa mwingine bado wakufikia yeye japo jopo la vijana wa kariba yake linaiva wakiongozwa na niliowataja hapo juu. Chama kimewatengeneza watu kama Mnyika na wengine ili wawe viongozi thabiti wa kisiasa wanaoweza kusimama wenyewe katika uga wa siasa za nera!
Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umeonyesha mtazamo chanya wenye turufu ya ukombozi, UKAWA Ikiwa namna hivi ilivyo miezi hii na ikawa na dhamira ya ukombozi wa nchi na kuamua kusimamia MGOMBEA urais mmoja ni hakika na kweli isiyotiliwa shaka kuwa wataiondoa ccm madarakani na hili bila shaka alama za nyakati zimesimama huru.
Ninashawika kuweka aina fulani ya mtazamo wa mgawanyo wa majimbo ili kudhibiti bunge.
Kati ya majimbo 189 bara, waamue NCCR iachiwe majimbo 20, CUF 20, na CDM 149. Kule zanz yale 50 CUF iachiwe yote.
Nccr ikipewa majimbo 20 haitashinda zaidi ya 10. Na 10 itakuwa kujazia ruzuku. CUF bara hawezi kushinda zaidi ya 5 na 15 itakuwa ruzuku. CDM haiwezi kushinda zaidi ya 70. Mengine itakuwa ruzuku. Na Zanzibar kati ya 50, CUF inaweza kushinda 25. Hivyo jumla UKAWA itakuwa imeshinda( 25+5), 70, na 10. Jumla 110 Kati ya majimbo 239.
Halafu ACT kama ni (chama kweli) ikijipambanua na agenda na ikacha siasa za kutumika kuidhoofisha CDM inaweza kushinda hata majimbo 2 wakiwa sereous kwasababu wanayo nafasi ya kuvizidi nccr na cuf. Na hawa UDP na TLP wakapata jumla 15
Upinzani kwa ujumla itakuwa na viti 127 kati ya 139. Hii ni zaidi ya nusu, Na hivyo kama itatokea UKAWA hawakushinda Urais, serikali itabidi iwe ya mseto kati ya UKAWA na CCM. HUYU ACT ATAAMUA NANI WAUNDE SERIKALI KATI YA CCM AU UKAWA lakini kutokana na pressure ya Umma kutaka mabadiliko, ACT HAITAWEZA KUUNGANA NA CCM. ITAKUWA KAMA ILIVOTOKEA UK LAST ELECTION
Liberal democratic ilikuwa 3rd force lakini mwamuzi. Ingawa kiitikadi inafanana na labor lakini ililazimika kuungana na Conservative ambayo kinyume chake kabisa policy wise na Ndivyo Labor ilivotoka.
Hivyo hitimisho ni kwamba 2015 nchi haina mgombea kutoka chama Tawala, bali yupo kutoka Upinzani ambae ni Dr Slaa.