2015 nchi haina mgombea Urais, isipokuwa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,272
Ukitazama mwenendo wa chaguzi nchini, Lyatonga ali drive uchaguzi 1995 hata kama alipoteza. Mwaka 2000 uchaguzi haukuwa na mvuto kwasababu Mkapa alionesha kutosha na upinzani haukuwa na nyota alyeibuka wala chama kilichokuwa na nguvu yakufanana na NCCR ya Mrema 1995 au kuzidi pamoja na mageuzi yote ya kidemokrasia.

Mwaka 2005 Jakaya Kikwete ali drive uchaguzi ule hasa kutokana na mwamko wa sera ya vijana na siasa za upinzani kuwa kwenye mageuzi ya ndani kimfumo, Utumizi mkubwa wa pesa na rushwa ya kisiasa kushamiri.

Mwaka 2010 Dr Slaa alifanikiwa ku drive uchaguzi katika mazingira magumu kwani alikuwa anashindana na rais anaetetea nafasi yake, tofauti na Lyatonga alivyoshindana 1995 ambapo Mkapa alikuwa mpya na hakujulikana, Slaa alivutia kwasababu alikuwa anatoka chama chenye agenda, cha vijana wengi waliopuuzwa na kudhalilishwa na ccm, Chama chake cha Chadema kilichonekana mbadala na yeye mwenyewe akitokea bungeni ambako alifanikiwa sana ktk agenda ya ufisadi hivyo alikuwa tishio kwa utawala wa kijana kikavu.

Mwaka 2015 naona mashaka ndani ya ccm. Huko ccm simwoni mgombea mwenye mvuto japo nusu ya ule wa JK wa 2005, wale wote wanaojipambanua kutaka kugombea ambao ni Membe, Migiro, Lowasa, Sitta, Makamba, Pinda nk ni wahanga wa uchafuzi ulioasisiwa 2005 wakati wa kumwingiza JK madarakani. Wamejeruhiana mno.

Ukija kwenye upinzani kati ya wagombea wote vinara wa UKAWA bado mgombea mwenye nafuu ni Dr Slaa tu, Pamoja na dola kutumika kwa nguvu zote kufifisha nguvu ya Slaa kutoka 2010 hadi 2014, bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbatia au Lipumba kwasababu mbalimbali ambapo nitazichambua nipatapo wasaa,

Kwa upande wa Chadema, ujio wa rika jipya lenye nguvu ya uvuli wa ukombozi ni tunu mpya ndani ya chama hicho, Nikiwaangalia Tundu Lissu, Godbless Lema, Mch Peter Msigwa, Halima Mdee, Joseph Mbilinyi, Wenje, John Mrema, John Mnyika na wengine wengi ambao sijawataja, ni watu wenye bidii na uwezo wa kusimamia itikadi na misingi ya chama ipasavyo, pia wana uwezo mkubwa wa kiutendaji na wameshakijua chama vizuri tofuti na lile joka la mdimu (Zitto).

Slaa hana compromise na govt. Dr Slaa ama Mbowe wakiwa juu serikali itakuwa na wakati mgumu sana zaidi ya ilivyo sasa, Dr slaa anapaswa sasa asiwe anafanya kazi operational za chama badala yake anahitaji team ya watalamu wa siasa na uchumi kutoka vyuo vikuu ama wale ma expat, media na research institution pamoja na watu wenye uzoefu wa nchi kama kina Butiku, Salim, Mtei, Warioba, Jenerali Ulimwengu, Mbowe nk.

Iwe timu ya kama watu 5-10 ambao wanakutana kila wiki kumshauri na kumpa updates za nchi, Wamtengenezee agenda. Ahutubie kila mwezi kutoa mwelekeo wa nchi. Kazi za utendaji wa chama amwachie Mnyika ama kijana imara yeyote kama katibu mkuu. Wanachama na viongozi wakate rufaa kwake

Dr Slaa kwenye chama ni zaidi ya kiongozi. Ndio moyo wa chama kwasasa. Hajatengenezwa mwingine bado wakufikia yeye japo jopo la vijana wa kariba yake linaiva wakiongozwa na niliowataja hapo juu. Chama kimewatengeneza watu kama Mnyika na wengine ili wawe viongozi thabiti wa kisiasa wanaoweza kusimama wenyewe katika uga wa siasa za nera!

Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umeonyesha mtazamo chanya wenye turufu ya ukombozi, UKAWA Ikiwa namna hivi ilivyo miezi hii na ikawa na dhamira ya ukombozi wa nchi na kuamua kusimamia MGOMBEA urais mmoja ni hakika na kweli isiyotiliwa shaka kuwa wataiondoa ccm madarakani na hili bila shaka alama za nyakati zimesimama huru.

Ninashawika kuweka aina fulani ya mtazamo wa mgawanyo wa majimbo ili kudhibiti bunge.

Kati ya majimbo 189 bara, waamue NCCR iachiwe majimbo 20, CUF 20, na CDM 149. Kule zanz yale 50 CUF iachiwe yote.

Nccr ikipewa majimbo 20 haitashinda zaidi ya 10. Na 10 itakuwa kujazia ruzuku. CUF bara hawezi kushinda zaidi ya 5 na 15 itakuwa ruzuku. CDM haiwezi kushinda zaidi ya 70. Mengine itakuwa ruzuku. Na Zanzibar kati ya 50, CUF inaweza kushinda 25. Hivyo jumla UKAWA itakuwa imeshinda( 25+5), 70, na 10. Jumla 110 Kati ya majimbo 239.

Halafu ACT kama ni (chama kweli) ikijipambanua na agenda na ikacha siasa za kutumika kuidhoofisha CDM inaweza kushinda hata majimbo 2 wakiwa sereous kwasababu wanayo nafasi ya kuvizidi nccr na cuf. Na hawa UDP na TLP wakapata jumla 15

Upinzani kwa ujumla itakuwa na viti 127 kati ya 139. Hii ni zaidi ya nusu, Na hivyo kama itatokea UKAWA hawakushinda Urais, serikali itabidi iwe ya mseto kati ya UKAWA na CCM. HUYU ACT ATAAMUA NANI WAUNDE SERIKALI KATI YA CCM AU UKAWA lakini kutokana na pressure ya Umma kutaka mabadiliko, ACT HAITAWEZA KUUNGANA NA CCM. ITAKUWA KAMA ILIVOTOKEA UK LAST ELECTION

Liberal democratic ilikuwa 3rd force lakini mwamuzi. Ingawa kiitikadi inafanana na labor lakini ililazimika kuungana na Conservative ambayo kinyume chake kabisa policy wise na Ndivyo Labor ilivotoka.

Taifa linahitaji mtu wa aina ya Dr Slaa atakaeweza kubadili siasa ya nchi hii kutoka za ukombozi hadi hivi sasa siasa za tumbo na atupeleke kwenye siasa za uchumi na mapinduzi ya viwanda, hii ni safari ambayo wenzetu tuliopata pamoja uhuru walishaimaliza na sasa ni nchi za kiuchumi, sio nchi za siasa za tumbo!

Pamoja na mambo mengine, taifa linahitaji rais atakaeweza kusimamia imara mageuzi ya taasisi nyeti ya Usalama wa Taifa , yapo mambo ya msingi yanayo takiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo hasahasa kuelekea 2015, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote kuanzialeadership,watendaji,te knolojia na sheria.

Sheria iliyounda chombo hiki inamapungufu kwa sasa kulingana na mageuzi ya kifikra na kiteknolojia, Sheria hii inaififisha tasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu,

Mathalani sheria hiyo inasema, "taasisi hii itahusika/itajihusisha na kutambua/kubaini na kutoa ushauri tu"
Kwamaneno hayo tu, TISS imenyimwa nguvu ya mojakwamoja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu.

Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika chombo hiki,

Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hii ili taasisi ya Usalama wa Taifa iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo nafikiri ihuishwe sheria hii imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii hawajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa ya kivyama.

Kwa taifa ambalo ni imara na lenye kiongo thabiti tumtakaye kama Dr Slaa, Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kikakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi. TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Is rael,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa mikakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50+ ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima kwanza tuwe na rais bora, na kisha tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii nikwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa tajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI yakutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate phyisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi

Taifa linataka rais atakayeweka malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)

Malengo makuu ya Rais ajae yanatakiwa kujikita katika:

1. Kuoneza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

2. Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis

3. Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

4. Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

5. TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

6. Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,k iulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa ‘Corroboration codification’

7. Kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndicho kinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

8. Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa ‘pyramid execution’.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

9. Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

10. Mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Hivyo hitimisho ni kwamba 2015 nchi haina mgombea kutoka chama Tawala, bali yupo kutoka Upinzani ambae ni Dr Slaa

Naiona hatari iliyombele yetu, hasa ya kisiasa, kiuchumi na machafuko ya kiroho ikiwa hatutafanya chaguo sahihi la Rais wa Tanzania 2015

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki 2015
 
Ukitazama mwenendo wa chaguzi nchini, Lyatonga ali drive uchaguzi 1995 hata kama alipoteza. Mwaka 2000 uchaguzi haukuwa na mvuto kwasababu Mkapa alionesha kutosha na upinzani haukuwa na nyota alyeibuka wala chama kilichokuwa na nguvu yakufanana na NCCR ya Mrema 1995 au kuzidi pamoja na mageuzi yote ya kidemokrasia.

Mwaka 2005 Jakaya Kikwete ali drive uchaguzi ule hasa kutokana na mwamko wa sera ya vijana na siasa za upinzani kuwa kwenye mageuzi ya ndani kimfumo, Utumizi mkubwa wa pesa na rushwa ya kisiasa kushamiri.

Mwaka 2010 Dr Slaa alifanikiwa ku drive uchaguzi katika mazingira magumu kwani alikuwa anashindana na rais anaetetea nafasi yake, tofauti na Lyatonga alivyoshindana 1995 ambapo Mkapa alikuwa mpya na hakujulikana, Slaa alivutia kwasababu alikuwa anatoka chama chenye agenda, cha vijana wengi waliopuuzwa na kudhalilishwa na ccm, Chama chake cha Chadema kilichonekana mbadala na yeye mwenyewe akitokea bungeni ambako alifanikiwa sana ktk agenda ya ufisadi hivyo alikuwa tishio kwa utawala wa kijana kikavu.

Mwaka 2015 naona mashaka ndani na nje ya ccm. Ndani ya ccm simwoni mgombea mwenye mvuto japo nusu ya ule wa JK wa 2005, wale wote wanaojipambanua kutaka kugombea ni wahanga wa uchafuzi ulioasisiwa 2005 wakati wa kumwingiza JK madarakani. Wamejeruhiana mno.

Ukija kwenye upinzani kati ya wagombea wote vinara wa UKAWA bado mgombea mwenye nafuu ni Dr Slaa tu, Pamoja na kuporomoka kwa Slaa kutoka 2010 hadi 2015 bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbowe au Mbatia au Lipumba kwasababu mbalimbali ambapo nitazichambua nipatapo wasaa,

Kwa upande wa cdm, Slaa angegombea uenyekiti na John Mnyika akawa katibu mkuu, Mbowe awe mwenyekiti bodi ya wadhamini. Itamsaidia Slaa kupumzika.

Mnyika ana bidii na uwezo wa kusimamia utendaji na anakijua chama vizuri, Pia itaondoa dhana ya uchaga na uchu wa madaraka. Slaa hana compromise na govt. Pia itaondoa dhana ya katiba ilibadilishwa ili mbowe aendelee. Kikubwa Dr Slaa akiwa juu serikali itakuwa na wakati mgumu sana. Mnyika pia atamsaidia management, Mh Mbowe kuwa mwenyekiti wa baraza la wadhamini bado atakuwa ni super threat kwa govt tofauti na watu wanavyofikiri.

Dr slaa alipaswa asiwe anafanya kazi operational za chama. Dr slaa anahitaji team ya watalamu wa siasa na uchumi kutoka vyuo vikuu ama wale ma expart, media na research institution pamoja na watu wenye uzoefu wa nchi kama kina Butiku, Salim, Mtei, Jenerali Ulimwengu nk.

Iwe team ya kama watu 5 ambao wanakutana kila wiki kumshauri na kumpa updates za nchi. Wamtengenezee agenda. Ahutubie kila mwezi kutoa mwelekeo wa nchi. Kazi za utendaji wa chama amwachie mnyika kama katibu mkuu. Wanachama na viongozi wakate rufaa kwake sio yeye akafukuze sasa wakate rufaa kwa nani au wamlilie nan?
Dr Slaa kwenye chama ni zaidi ya kiongozi. Ndio moyo wa chama kwasasa. Hajatengenezwa mwingine bado wakufikia yeye japo jopo la vijana wa kariba yake linaiva wakiongozwa na Lisu, Lema, Mnyika nk.

Chama kimewatengeneza watu kama mnyika na wengine ili wawe viongozi dhabiti wa kisiasa wanaoweza kusimama wenyewe

Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umeonyesha mtazamo chanya wenye turufu ya ukombozi, UKAWA Ikiwa namna hivi ilivyo miezi hii na ikawa na dhamira ya ukombozi wa nchi na kuamua kusimamia MGOMBEA urais mmoja, basi wagawane majimbo ili kudhibiti bunge.

Kati ya majimbo 189 bara, waamue NCCR iachiwe majimbo 20, CUF 20, na CDM 149. Kule zanz yale 50 CUF iachiwe yote.

Nccr ikipewa majimbo 20 haitashinda zaidi ya 10. Na 10 itakuwa kujazia ruzuku. CUF bara hawezi kushinda zaidi ya 5 na 15 itakuwa ruzuku. CDM haiwezi kushinda zaidi ya 70. Mengine itakuwa ruzuku. Na zanz kati ya 50, CUF inaweza kushinda 25. Hivyo jumla UKAWA itakuwa imeshinda( 25+5), 70, na 10. Jumla 110 Kati ya majimbo 239.

Halafu ACT kama ni (chama kweli) ikijipambanua na agenda na ikacha siasa za kutumika kuidhoofisha CDM inaweza kushinda hata majimbo 15 wakiwa sereous kwasababu wanayo nafasi ya kuvizidi nccr na cuf. Na hawa UDP na TLP wakapata jumla 2.

Upinzani kwa ujumla itakuwa na viti 127 kati ya 139. Hii ni zaidi ya nusu, Na hivyo serikali itabidi iwe ya mseto UKAWA, CCM NA ACT.
HUYU ACT ATAAMUA NANI WAUNDE SERIKALI KATI YA CCM AU UKAWA lakini kutokana na pressure ya Umma kutaka mabadiliko, ACT HAITAWEZA KUUNGANA NA CCM. ITAKUWA KAMA ILIVOTOKEA UK LAST ELECTION

Liberaldemocratic ilikuwa 3rd force lakn mwamuzi. Ingawa kiitikadi inafanana na labor lakini ililazimika kuungana na Conservative ambayo kinyume chake kabisa policy wise na Ndivyo Labor ilivotoka.

Hivyo hitimisho ni kwamba 2015 nchi haina mgombea kutoka chama Tawala, Wote ni majeruhi ndani na nje ya upinzani wafanye haya.

Yericko wewe huna lolote tunakufahamu wewe ni mchumia tumbo huna jipya
 
Mungu inusuru chama, akina Mwigamba walianzaga hivi hivi kwa kuandika makala kama haya, unaweza kufafanua kwa vipi Dr. Slaa kaporomoka?, Ben Saanane tunaaomba uchambuzi wako yakinifu hapa.

Yote ni sahihi, ila bado napata shida kujua kwa mantiki ipi umetumia kuipa ACT majimbo 15 kwenye uchaguzi ujao wakati ni takribani miezi 13 tu imebakia kufikia uchaguzi mkuu.

Hiki chama bado hakijajulikana hata kwa 20% katika nchi, bado ni kichanga mno, chama hakijafanya walau uchaguzi mkuu wake ili kujua viongozi wake wa kudumu. Hiki chama bado kina kazi ya ziada kujipambanua kwa wananchi ili waondoe dhana iliyojengeka kwamba wao si wapinzani wa kweli bali wamekuja kupambana na CDM ili kuidhoofisha na hatimaye CCM ipate nafuu.

Bila kufanya hivyo ACT naweza kuipa Jimbo moja tu kule Kigoma, hata hilo sina uhakika kwa asilimia mia kama wanaweza kulinyakua mikononi mwa CDM, CCM ama NCCR Mageuzi.

Ni kweli kama CUF wataamua kwa dhati kabisa kushirikiana na CDM na kukubali dhana ya mgombea mmoja kwa tiketi ya UKAWA basi watanzania tuwe tayari kwa mageuzi ya kiuongozi katika nchi yetu kwa mara ya kwanza tangu Uhuru.
 
Pamoja na kuporomoka kwa Slaa kutoka 2010 hadi 2015 bado ndio mtu sahihi ukilinganisha na Mh Mbowe.

Kwa upande wa cdm, Slaa angegombea uenyekiti na Mbowe awe mwenyekiti bodi ya wadhamini. Itamsaidia Slaa kupumzika. Pia itaondoa dhana ya uchaga na uchu wa madaraka. Pia itaondoa dhana ya katiba ilibadilishwa ili mbowe aendelee.

Dr slaa alipaswa asiwe anafanya kazi operational za chama.. Kazi za utendaji wa chama amwachie mnyika kama katibu mkuu. Wanachama na viongozi wakate rufaa kwake sio yeye akafukuze.

Halafu ACT inaweza kushinda hata majimbo 15 wakiwa sereous kwasababu wanayo nafasi ya kuvizidi nccr na cuf. HUYU ACT ATAAMUA NANI WAUNDE SERIKALI KATI YA CCM AU UKAWA .
Japo sikubaliana na wewe kwa mengi ya uliyoyaandika, lakini nikiri kuwa nimeshangazwa na wewe kama mnazi wa Chadema kuyatamka haya, maana manazi wengi wa Chadema wanaamini chama hakijawahi kuporomoka toka kilipopanda 2007.
 
Yote ni sahihi, ila bado napata shida kujua kwa mantiki ipi umetumia kuipa ACT majimbo 15 kwenye uchaguzi ujao wakati ni takribani miezi 13 tu imebakia kufikia uchaguzi mkuu.

Hiki chama bado hakijajulikana hata kwa 80%, chama hakijafanya walau uchaguzi mku wake ili kujua viongozi wake wa kudumu. Hiki chama bado kina kazi ya ziada kujipambanua kwa wananchi, waondoe dhana iliyojengeka kwamba wao si wapinzani wa kweli bali wamekuja kupambana na CDM ili kuidhoofisha na hatimaye CCM ipate nafuu.

Bila kufanya hivyo ACT naweza kuipa Jimbo moja tu kule Kigoma, hata hilo sina uhakika kwa asilimia mia kama wanaweza kulinyakua mikononi mwa CDM, CCM ama NCCR Mageuzi.

Ni kweli kama kweli CUF wataamua kwa dhati kabisa kushirikiana na CDM basi watanzania tuwe tayari kwa mageuzi ya kiuongozi katika nchi yetu kwa mara ya kwanza tangu Uhuru.
Kumbuka maneno ya Samson Mwigamba kuwa wengi ndani ya chadema wanaisema vibaya ACT wakati wa mchana ila usiku wanalala nayo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom