2006 Coca-pepsi (cola) vicious trade war & corporate espionage: Secretary wa COCA-COLA alivyoiba "highly classified documents" kwenda kuwauzia PEPSI

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
PEPSI WALIGOMA KUNUNUA SIRI ZA KIBIASHARA ZA COCA COLA BADALA YAKE WAKAAMUA KUTOA TAARIFA POLICE/FBI

20200703_131217.jpg


Kama ingefanikiwa, basi ingekuwa ni usaliti mkubwa sana wa kibiashara katika historia ya dunia. Secretary mmoja aliyekuwa anafanya kazi katika ofisi ambazo ndio makao makuu ya kampuni ya utengenezaji wa vinywaji baridi vya Coca Cola alikamatwa kwa kosa la kuiba nyaraka muhimu sana za kampuni hiyo na kisha kuzificha katika begi lake na kutaka kwenda kuziuza kwa mpinzani wa Coca, ambaye ni Pepsi, kwa kiasi cha dollar za kimarekani 1,500,000 mnamo mwaka 2006.

Katika kampuni kama Coca Cola, secretary ni moja kati ya watu muhimu sana katika kuongoza kampuni. Wafanyakazi wote hufanyiwa "security check" ya mara kwa mara. Camera za usalama (Surveillance Cameras).

Silaha yao ya thamani sana, kanuni ya utengenezaji wa unga wa Coca cola (The Cola Powder Formula), inasemekana imefungiwa katika locker/shelf yenye thamani ya mamilioni ya dola za kimarekani, na ni watu wawili tu hapa duniani ndio wanaifahamu, na siku zote hawapandi ndege moja bali kila mtu anapanda ndege tofauti na mwenzake just in case kama ajali itatokea basi wasife pamoja hahahaaaaa this is funny kwakweli.

images-12.jpg


Katika mazingira kama haya yaliyojaa usiri wa hali ya juu, Joya Williams alikuwa ni mfano wa kuigwa.

Binti wa mchungaji wa Kanisa la kilokole, na msimamizi mkuu wa shughuli zote za Sunday School, alikuwa tayari amekwishafanya kazi kwa muda wa miaka 4 katika kiwanda kikubwa cha kutengeneza chupa cha hao hao Coca cola kabla ya kuhamishiwa headquarters mwaka 2005.

Kwa kuwa alikuwa ni msaidizi wa administrative assistant wa mkuu wa idara ya matangazo duniani kote, aliaminiwa na kukabidhiwa emails nyeti sana, nyaraka za ndani mno pamoja na mipango ya bidhaa ambazo Coca walikuwa wanajiandaa kuzalisha na hii ni kulingana na taarifa za baadhi ya wafuatiliaji wa masuala vita za kibiashara.

images-14.jpg


Lakini miezi 14 katika ajira yake hiyo ya malipo ya dollar za kimarekani 50,000 kwa mwaka, alianza kuhisi kuwa alikuwa ananyanyaswa na alianza kuandaa mipango ya kulipiza kisasi.

Katika kufanya tukio la hatari sana la kula njama ya kibiashara ambalo baadae lilikuja kuonekana kuwa ni la utoto mwingi na lililokosa utaalam, msaidizi wa mkurugenzi (Global Brand Director) alituhimiwa kwa kutaka kuanzisha tena vita kubwa (Cola War) baina ya kampuni hizi mbili zenye historia ya pinzani katika suala zima la ladha, udhamini, matangazo ya biashara, virutubisho katika vinywaji vyao pamoja na kanuni za utengenezaji.

Mwishoni mwa mwezi wa November mwaka 2005, Williams alitambulishwa kwa rafiki wa rafiki yake aliyejulikana kwa jina la Edmund Duhaney. Akiwa na umri wa miaka 40, na baba wa watoto 3, Duhaney ndio kwanza alikuwa ametoka jela kwa makosa ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na alikuwa akitafuta kibarua cha kufanya.

images-26.jpg


Williams akamwambia Duhaney ya kwamba alikuwa anayo mafaili ya siri sana (highly classified documents) ya kampuni ya Coca cola ambayo yangeweza kuwapatia fedha nyingi sana kutoka kwa wapinzani wa Coca ambao ni Pepsi. Lakini tayari alikuwa ana makubaliano maalum ya kutotoa siri (non-disclosure agreement) na asingeweza kupeleka hizi documents yeye binafsi.

Williams alihitaji mtu wa kumtumia katika kuuza hizi documents, na Duhaney alikuwa anamfahamu mtu mmoja aliyejulikana kama Ibrahim Dimson, jamaa mmoja fisadi, mtoto wa mjini, na ni mcheshi haaaswaaa aliyekutana naye alipokuwa jela.

Akitumia jina la uongo la "Dirk" Dimson alituma barua (kwa kutumia bahasha rasmi yenye nembo ya Coca cola) akiituma kwa moja kati ya wakurungenzi waandamizi wa Pepsi akidai kuwa yeye ni afisa muandamizi wa Coca anayetaka kuwapa siri za ndani sana za kibiashara.

image.png


Lakini secretary yule hakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya uhusiano uliokuwepo sasa baina ya wapinzani hao wawili (Vodacom Tanzania na Tigo).

Wiki mbili baadaye, wakati ambao Williams alikwishaanza kufurahi, Dimson akapigiwa simu kutoka kwa mtu aliyesemekana kuwa ni mfanyakazi wa Pepsi aliyejiita kuwa ni Jerry. Jerry alikubali kununua siri zile lakini alihitaji ushahidi kwanza juu ya uwepo wa siri hizo.

Dimson akamtumia Jerry kwa njia ya fax kurasa 14 za nyaraka za kampuni ya Coca cola zilizowekewa alama ya "confidential information" na kisha kumwambia Jerry ya kuwa anataka kutumiwa pesa katika bank account aliyomtajia ili kumuonesha ya kuwa yeye ni business partner mzuri na mwaminifu.

Punde tu hapo baadae akatumiwa pesa kiasi cha dollar 5,000, na baada ya hapo sasa balaa ndio likaanza.

Kama mwanamke aliyeaminika miongoni mwa viongozi waandamizi wa Coca cola, Joya Williams aliweza kuchukua sio tu idadi kibwa sana ya documents (presentations, emails za ndani za viongozi wa kampuni, mipango ya maendeleo ya kibiashara) bali pamoja na sampuli za bidhaa za Coca-Cola ambazo bado hazijaanza kuuzwa.

Siku moja mida ya jioni kuelekea usiku akiwa katika makao makuu ya Coca cola - jengo kubwa, lililoshiba na kujaa kati kati ya jiji la Atlanta Georgia - Williams alijaza begi lake kwa kubeba documents za siri pamoja na kichupa kidogo cha bidhaa ya siri ambacho Coca walikuwa wakiandaa kabla ya kupeleka sokoni.

Baada ya kuzipata nyaraka zile, Williams akazipeleka kwa Dimson, ambaye mara moja chaaaap akamshawishi Jerry kuzinunua kwa dollar 75,000 - dollar 30,000 papo kwa hapo na zilizobaki atalipa baada ya kufanya testing.

Kwenye tarehe 17 mwezi wa June, Dimson na Jerry walipanga kukutana huko uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hartsfield Jackson jijini Atlanta, ambapo mchana kweupeee peee Dimson alikabidhi begi lililokuwa na rangi ya brown lililojaa documents muhimu kisha yeye akapewa box dogo la rangi ya kaki lililojaa pesa nyingi.

Dimson akaondoka airport, akaingia katika gari akiwa na jamaa yake Duhaney kisha wakaelekea mpaka Decatur, huko Georgia, ambapo waligawanya mpunga, cash, mapene, mkwanja. Jamaa waliula aisee.

Dimson akaondoka airport, akaingia katika gari akiwa na jamaa yake Duhaney kisha wakaelekea mpaka Decatur, huko Georgia, ambapo waligawanya mpunga, cash, mapene, mkwanja. Jamaa waliula aisee.

Dollar 2,000 kwa Duhaney, dollar 6,000 kwa Williams na dollar 22,000 kwa Dimson mwenyewe.

Ila siku yenyewe ya malipo ilifuata siku 10 baadaye ambapo Jerry alimpigia simu Dimson na kuahidi kulipa dollar 1,500,000 kwa documents za siri zilizobaki.

Hawa jamaa kwa akili zao fupi wakaona kama vile wameokota dodo kwenye muarobaini. Wajinga kweli.

Ona sasa, huyu Jerry hakuwa manager mwandamizi wa Pepsi. Jerry alikuwa ni mpelelezi wa FBI jina lake halisi akiwa Gerald Reichard.

Viongozi wa Pepsi walilitolea taarifa suala lile kwa mabosi wa Coca ambao nao pia wakawataarifu Police.

Miezi kadhaa nyuma baada ya Pepsi kupokea barua kutoka kwa wahalifu hawa watatu, wao (Pepsi) wakaituma barua ile chaaaap kwa Coca-Cola na kisha kuwajulisha kuwa wana msaliti ndani ya kampuni yao. Matokeo yake Coca-Cola wakaomba msaada wa FBI kufanya upelelezi wa siri.

Maafisa wa FBI waliovalia kiraia wakajifanya kuwa ni mabosi waandamizi wa Pepsi kisha kujifanya kuwa wanataka kununua nyaraka zile na kumkamata dada yule papo kwa hapo (redhanded).

Mnamo tarehe 05, mwezi wa 6, mwaka 2006, Williams, Dimson pamoja na Duhaney, walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu pamoja na wizi wa nyaraka za siri za kibiashara.

Director of Public Prosecutions (DPP) kisha akatoa taarifa yake maalum ya kuwapongeza Pepsi kwa kufanya jambo lililo jema sana kwa sababu siri za kibiashara ni muhimu kwa wadau wote wa biashara husika. Walijua fika kama siri zao za biashara zitavuja basi wao wataathirika pa kubwa sana, soko pamoja na wadau wengine wote pia wataathiriwa vile vile.

ITAENDELEA NEXT TIME. JUST STAY TUNED.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Secretary wa Vodacom Tanzania anaenda kuuza siri za kampuni yake kwa Tigo Tanzania alafu Tigo wanakataa kununua kisha wanawajulisha police.

Don't you find this strange?

Bro ukiingia kwenye biashara kubwa kama hizi ndio utaelewa jamaa hawako serious kwenye competition kama tunavyoaminishwa nishawahi kufanya kazi kampuni moja kubwa sana ya vinywaji siku mtambo umeharibika kuna chip fulani hivi ilivunjika eti wakaenda kuomba kwa mpinzani la sivyo kiwanda kingesimama kama week mbili hivi no production halafu mpinzani wao akawapa kiroho safi na hadi fundi wa kuwafungia akawaletea
 
Secretary wa Vodacom Tanzania anaenda kuuza siri za kampuni yake kwa Tigo Tanzania alafu Tigo wanakataa kununua kisha wanawajulisha police.

Don't you find this strange?
Not strange at all..
Btw coca wanasema siri ya kutengeneza recipe ya kinywaji chao ni the most guided secret.. lakini hata pepsi wakiipata haitawasaidia kitu. Pepsi wanaendelea kuwa sokoni kwa sababu ya identity yao walioitengeneza.. the moment pepsi watakapoanza kuuza soda zenye ladha exactly kama coca ndio mwisho wao utakapokua umefika.

Kwahio pepsi hawana shida na kununua siri ambayo haiwasaidii kitu na inawezekana mpaka sasa wanaijua au wanaweza kutengeneza recipe ya coca sema wakisema watengenezee wanakua wamejiua kibiashara.

Same applies to voda ma tigo.. utofauti wao ndio strength yao.. ya nini kuchukua siri ya mtu mwingine ambazo ukizitumia utakua kama yeye tu. Labda zingekuwa ni siri za makosa waliofanya au loopholes kwenye mikataba yao.
 
Secretary wa Vodacom Tanzania anaenda kuuza siri za kampuni yake kwa Tigo Tanzania alafu Tigo wanakataa kununua kisha wanawajulisha police.

Don't you find this strange?
Strange ndiyo lakini kwa jicho jingine inabidi ikupe indication kwamba kunaweza kukawa na na maofisa wa Vodacom wameajiriwa na Kampuni ya Tigo, pasipo wao Tigo kujua kuwa ni maofisa wa Vodacom na kinyume chake pia kwa Kampuni ya Tigo
 
Strange ndiyo lakini kwa jicho jingine inabidi ikupe indication kwamba kunaweza kukawa na na maofisa wa Vodacom wameajiriwa na Kampuni ya Tigo, pasipo wao Tigo kujua kuwa ni maofisa wa Vodacom na kinyume chake pia kwa Kampuni ya Tigo
Double agents make the first line of defence. You're right. Coca probably had moles in the Pepsi's top brass hierarchy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom