Kheri bangi kuliko unga
Kheri bangi kuliko unga
Kweli nimeamini ile nyimbo aliyoimba yeye mwenyewe 20% alikuwa akimaanisha kitu(bange bange imenisababisha ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)
huyu bana kashikwa na Bange lake la Gram kadhaaaaaaaaaa,
Hivi hawa wasanii wetu bila hayo mabange yao hawawezi kuishi wala kuimba?
haya sasa ngoja ukanyee ndoooooooooooooo
Hata Uswisi sio kosa tena wao wametenga maeneo mahsusi ya kuvutia bangi na mihadarati, kwa mji wa Bern, eneo huru la kuvutia ni mbele ya jengo la bunge la nchi hiyo, The Bundes House, hii inafanya kuingiza mihadaraji nchini humu sio dili.
20% kakutwa na 20 grams, hicho ni kiwango kidogo halali kwa matumizi yake.
Kosa la kukutwa na bangi, linatakiwa lifanywe kama kosa la kufanya mapenzi hadharani, ukifanya private sio kosa.
Kuna yule lecture wa UDSM, Mjamaica, alikutwa anavuta hadharani, akapelekwa mahakamani, akakiri kuwa anatumia hiyo kitu na bila kuitumia hawezi kufanya chochote, alilipishwa faini na kuachiwa, ila aliambiwa akiitumia, aitumie private sio public!.
Nakumbuka enzi za O-level Tambaza, hiyo kitu ilitumika sana kule juu summit, wengi wa watumiaji walitoka na Div I kali, hivyo nilipojoin form V Ilboru, niliijaribu ili nami nifumue one, unfortunately mimi ilinituma vibaya!.
Ndio maana hoja za kulegalize zina uhalali fulani, tufike mahali tukubali, wale zinaowatuma vizuri, waruhusiwe kuitumia hiyo kitu, kuna wengi zinawatuma vizuri na kuna justified medical use ya marijuana kusaidia magonjwa fulani na kupunguza acute pain, na wengine inawapa raha ya ajabu katika ile game.
Lakini iendelee kupigwa marufuku kwa wale inaowatuma vibaya. Angalizo, sigara ya kawaida ina sumu ya nicotine kuliko bangi. Na kikombe kimoja cha kahawa, kina cafeine nyingi zaidi ya kusabisha addiction kuliko msokoto mmoja wa Bangi!.
Polisi inabidi wawakamate wasanii wote wanao tumia vinginevyo twaweza sema polisi kuna mkono wa mtu umetumika kumhujumu 20%
yule si rasta??nazani kama ni mvutaji basi atakuwa ametendewa haki