20% Apelekwa Mahakamani Kwa Kukutwa na Kilo 20 za BANGI

YEYE

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
437
72
Mwanamuziki Twenty Percent 20% amepelekwa mahakamani leo mkoani LINDI baada ya kukutwa na KILO 20 ZA BANGI katika gari lake siku nne zilizopita
 


chunga tamaaaaaaaaaaa mbayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..............LOL S
 
Last edited by a moderator:
pengine alibambikiwa wakuu. kuna mtu namjua amebambikiwa madawa na boss wake ofisini, kisa jamaa alikuwa anamsema huyo mnene
 
Sifa ya moyo tamaa, moyo sifa yake kutamani
Tamaa ya moyo, inaweza kukuweka matatani
Unatamani kuzaa, wakati bado uko shuleni
Tumia akili kukataza, kabla hujawa matatizoni
Ile ndoto ya kitandani, achana nayo
Kama uhanisi labda haiwezekani, kuendana nayo
Unaweza ukaota umejenga angani, angani
kuhifadhi ndoto ya shida gani, wewe.

Chorus --Tuliza moyo wako, kubali mapungufu yakoooo
--Rahisisha mahitaji yako, ongeza kipato chakooo
--Chunga tamaa mbaya, chunga tamaa mbaya x2


Sifa ya macho kuona, kutazama kinachoonekana
Ila sio kila unachokiona, utadhani kupata inawezekana
Nyumbani kuna msichana, njiani utaona wengi wasichana
Bora kuishia kutazama, kuliko kujifanya unaweza sana
Siri ya maisha yako iko kwa muumba, muumba
Alisema mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba, kuwa simba
Hawezi kuongea, eti anaforce kuimba
Bora kutulia ama kupiga marimba, utasikika pia

Chorus.......

Mwanzo wa safari nakufuata kijana, nakuja na swali unipe jibu la maana
Dunia bila wizi hivi itawezekana, kama haiwezekani siku tukijaonana,
Nitakiweka mbali kisimu changu cha mchina, vijana wote nitawaona hamna maana
Tunarudishana nyuma mambo ya kuibiana, mwenzenu naona noma polisi kupelekana, yeaah.

Chorus......
 
kama ni gram 20 basi sawa tu kwani ahwezi kuandika wala kuimba bila kunyonga na kupiga pafu japo tano
 
Hatukatai wanatumia lakini kilo 20 ni nyingi ndugu yangu hapa atakuwa muuzaji sio tena mtumiaji,Uholanzi ukikamatwa na misokoto 2-3 sio kesi lakini zikizidi 10 unalo.
Hata Uswisi sio kosa tena wao wametenga maeneo mahsusi ya kuvutia bangi na mihadarati, kwa mji wa Bern, eneo huru la kuvutia ni mbele ya jengo la bunge la nchi hiyo, The Bundes House, hii inafanya kuingiza mihadaraji nchini humu sio dili.

20% kakutwa na 20 grams, hicho ni kiwango kidogo halali kwa matumizi yake.

Kosa la kukutwa na bangi, linatakiwa lifanywe kama kosa la kufanya mapenzi hadharani, ukifanya private sio kosa.
Kuna yule lecture wa UDSM, Mjamaica, alikutwa anavuta hadharani, akapelekwa mahakamani, akakiri kuwa anatumia hiyo kitu na bila kuitumia hawezi kufanya chochote, alilipishwa faini na kuachiwa, ila aliambiwa akiitumia, aitumie private sio public!.

Nakumbuka enzi za O-level Tambaza, hiyo kitu ilitumika sana kule juu summit, wengi wa watumiaji walitoka na Div I kali, hivyo nilipojoin form V Ilboru, niliijaribu ili nami nifumue one, unfortunately mimi ilinituma vibaya!.

Ndio maana hoja za kulegalize zina uhalali fulani, tufike mahali tukubali, wale zinaowatuma vizuri, waruhusiwe kuitumia hiyo kitu, kuna wengi zinawatuma vizuri na kuna justified medical use ya marijuana kusaidia magonjwa fulani na kupunguza acute pain, na wengine inawapa raha ya ajabu katika ile game.

Lakini iendelee kupigwa marufuku kwa wale inaowatuma vibaya. Angalizo, sigara ya kawaida ina sumu ya nicotine kuliko bangi. Na kikombe kimoja cha kahawa, kina cafeine nyingi zaidi ya kusabisha addiction kuliko msokoto mmoja wa Bangi!.
 
Ni baada ya vuta nikuvute na polisi baada ya kukaidi kukaguliwa gari yake.
 
Kweli nimeamini ile nyimbo aliyoimba yeye mwenyewe 20% alikuwa akimaanisha kitu(bange bange imenisababisha ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)

huyu bana kashikwa na Bange lake la Gram kadhaaaaaaaaaa,
Hivi hawa wasanii wetu bila hayo mabange yao hawawezi kuishi wala kuimba?

haya sasa ngoja ukanyee ndoooooooooooooo
 
wanasema eti weed inawafanya wawe na sauti nzuri, halafu inawakinga kutokana na uchawi. Si unajua bongo fleva artist kwa kurogana?
T I D karudi rasmi kwenye matumizi ya unga, eti unamfanya awe na sauti nzuri
 
Back
Top Bottom