2/3 of Africans have no toilets! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2/3 of Africans have no toilets!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba la Nyoka, Mar 22, 2008.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa CNN
  two third of Africans have no toilets,

  sijui wametumia vigezo vipi kufikia conclusion hiyo, au wanafikiri waafrika wanajisaidia maporini?
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Definition yako na yao kuhusu toilet inaweza kuwa tofauti, wao wame idefine toilet vipi?

  Wanaweza kukwambia toilet lazima iwe na running water, au pit latrines are not toilets.If they are operating under such definitions then yes, two thirds of Africa do not have toilets. Mind you the population of Africa is mainly rural using pit latrines, even with rural urban migration most migratnts reside in slumlike places like Nairobi's Kibera or some of Dar-es-salaams Madongokuinamas where there is no running water (come to think of it even Sinza does not have running water and some first floor apartments in Upanga require a water pump to have running water!)

  From www.dictionary.com

  1. a bathroom fixture consisting of a bowl, usually with a detachable, hinged seat and lid, and a device for flushing with water, used for defecation and urination.
  2. a lavatory.
  3. a bathroom.
  4. toilet bowl.
  5. a dressing room, esp. one containing a bath.

  Lavatory

  1. a room fitted with equipment for washing the hands and face and usually with flush toilet facilities.
  2. a flush toilet; water closet.
  3. a bowl or basin with running water for washing or bathing purposes; washbowl.
  4. any place where washing is done.
   
 3. T

  Tom JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2008
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Afrika ina collectors/hunters and normadic 'tribes' nyingi tu, hata Tanzania zipo na watu wote wa hizo tribes hujisaidia porini. Kuna makabila mengine ni ya wakulima lakini pia wana hiyo taboo/culture. Hata Tanzania hatujapata mafanikio ya kufutilia mbali hiyo taboo.

  Miji yetu sehemu kubwa haina plan na kuna pit-latrines nyingi tu zisizojengewa/ezekwa ama ambazo unaona kinyesi moja kwa moja na mlango ama hamna ama ni wa gunia na inzi hutembelea kinyesi wapendavyo. Vingi hutegemea mvua inyeshe ili ku-flush (Mwananyamala nk)- hivi standard yake ni sawa na kujisaidia porini.

  Tuna safari ndefu Tanzania (Afrika?), lakini wananchi hawapo informed. Ama viongozi wetu wengi wametokea kwenye hizo taboo, hivyo hawaoni kama ni tatizo kubwa. Hata ofisi zao za serikali hazina maji ama toilets.

  Sello, mambo ni kwenye ndoo na watu wamejazana.
  Hizo theruthi mbili wametuonea aibu tu.
   
 4. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  duh! kama huo ndo ukweli basi ukweli unauma!.
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  WAHESHIMIWA .....!WE HAVE TO BE CAREFUL WITH THESE COLOURLESS PEOPLE..!(white?)ALL THEY HAVE NI NEGATIVE ABOUT AFRICA...darfur,refugees,rwanda,kenya election,bokassa,savimbi,CORRUPTION,BOT,EPA,drc.etc...!
  THEY DONT HAVE THE GOOD SIDE OF IT......peace,kilimanjaro,nyumbu automobile assembly plant,good political parties,nyumba za wilaya mbinga zinazoongoza kwa ubora(matofali ya kuchoma),etc.....!BECAUSE THEY DONT HAVE THE GOOD SIDE OF IT, WE HAVE TO GIVE THEM...!
   
 6. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  6 in 10 Africans remain without access to proper toilet: poor sanitation threatens public healthWEBWIRE – Friday, March 21, 2008


  Hili ndio linalosemwa, nafikiri mwanzishaji wa hii mada hakufafanua.
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  May be they don't need them. They hardly eat!
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Mar 24, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani ndio ukweli huo!...
  Toilet ni kama inavyojieleza hatuwezi ita choo cha shimo toilet.. wala mkokoteni kuitwa Truck (lorry) kwa sababu tu nalo huchukua mizigo.
   
 9. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Wakome kabisa kuzungumzia "vyoo vyetu". Kwanza imenikumbusha Wamasai wanayotucheka sisi wengine tunapojenga nyumba zenye "sehemu ya mavi ya ndani"!

  Swala la choo lina dimension ya utamaduni. Kwa Mmasai, ni "aibu" mtu kuacha wageni sitting room kisha unakwenda haja kubwa chumba kinachofuatia!

  Tuna wanyama pori wengi sana. Na kila mmoja wao choo chake ni kibaya kuliko cha binadamu. Hakuna tatizo la vyoo vyao. Sisi ni lazima tuwe na vyoo vya aina ya nyumba? Hivyo vyoo vyetu vya siku zote (ambavyo sii vya nyumba) kwanini tukubali kwamba sio vyoo?

  Inawezekana theluthi mbili ya Waafrika hawana vyoo vya aina ya nyumba, lakini wana vyoo. Haiwezekani kuishi bila vyoo.
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Moshi, toilet na "choo" vinaweza kuwa vitu viwili tofauti.They are talking about toilets, specifically in the western hygienical sense, bowl running water, flush and the whole nine yard.

  Mmasai kama ulivyosema anaweza kukuonyesha kichaka akakuambia hiki ndiyo choo.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Mar 24, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hii mbona rahisi sana....harufu ya kinyesi na mkojo inanuka kila kona ya Dar...na hiyo ni mjini. Kijiji kwa babu mtu ukibanwa haja kubwa au ndogo unatafuta kichaka tu halafu unajiachia.....you don't even need a study to figure this one out.
   
 12. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2008
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Gamba,
  Yep ukweli kuluma muno!

  Na wala tusiende mbali kwa kuzungumzia ukosefu wa vyoo vijijini ingali sehemu nyingi za Dar msalani ni zoezi. Mpaka leo hii sehemu congested kama Mwananyamala, Buguruni n.k. bado watu wanashare vyoo....tena vya shimo.

  kama unafikiri ile myth ya watu kusubiri mvua inyeshe ili wa-release ni ulongo, basi jaribu kutembelea maeneo maeneo. Kuna tofauti kubwa kati ya maji ya mvua na maji ya chooni..
   
 13. N

  Ngao Member

  #13
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukran sana kwa hoja za Pundit, Dua na Moshi! Ila Dua ametusaidia zaidi kutuletea hiyo habari yenyewe, kwani hata mie nilishaanza kufadhaishwa nayo.
  Uweli ni kwamba hili suala la 'toilet' na choo yapaswa tuyaangalie kwa umakini zaidi kwani yana kigezo kikubwa cha utamaduni wa watu. Kwani toilet ni choo?? Lakini kuna suala la kuwa na choo na utaratibu mzima wa kwenda chooni. Jaribu kulinganisha vile vyoo vya mijini vya umma (vya miaka ya sabini, na hata vingine vya sasa hivi) jinsi vilivyokithiri uchafu na hatari zake za kueneza maradhi ya mlipuko kwa upande mmoja na utaratibu wa wakazi wa shamba wa kutumia jembe kujichimbia mashimo ya dharura haja inapotokea wakamaliza haja zao na kufukia vizuri na kunawa mikono kwa upande mwingine.
  Kwa hiyo tunapolijadili hili suala tuyaweke maanani yote hayo. Jaribu kufikiria umejikuta uko huko bara vijijini, unafanya utafiti wako hata kama ni wa post graduate ya masuala ya afya, umejikuta uko pahala hakuna hiyo toilet wala lavatory, umebanwa na haja, una vichaka na labda kwa bahati tissue, huna hata hilo jembe jirani. Nambie, utaanza kutheorize mambo ya toilets na matumizi yake sahihi?
  Lakini suala lilikuwa kuikubali hiyo hoja ya wanahabari kama chanya na iliyostahili kuchapishwa, au ni kuwazushia waafrika kiuonevu, sio? Naona ni hoja ya msingi tu ambayo haihitaji kutuchanganya. Kwa sababu kwa minajili ya habari yenyewe, wala si Afrika pekee, bali hata sehemu zingine duniani ambazo huo utmaduni wa toilets haujaweza kuenea.
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hamna cha utamaduni hapa! Mbona tunapoambiwa ni asilimia kumi tu wenye access na umeme hatutafuti tofauti ya umeme wao na umeme wetu? Sanitation ni eneo ambalo tumelipuuzia kwa muda mrefu sana na haya ndiyo malipo yake. Mji wa Dar es Salaam, wenye wakazi zaidi ya milioni 3, hauna Waste Treatment Plant wala extensive sewer system tunategemea nini? Tunatumia septic tanks na soak pits ( ambazo zimebuniwa kwa matumizi ya mashambani) kwenye high density plots, sehemu za kariakoo, manzese n.k wanashirikiana vyoo ambavyo wala sio VIP bali ni basic mashimo (pit latrines) na wengine bila shaka wanajisaidia kwenye rambo!Tumefikia wakati ambapo badala ya kutafuta solution ya pesistent water shortages Chuo Kikuu tunawajengea pit latrines! Huko vijijini ni wangapi wenye vyoo (na wote humu tunajua choo ni nini)? Ukitilia maanani jinsi idadi ya watu inavyozidi kuongezeka na mabadiliko ya lishe hiyo solution ya kujisaidia maporini haiko sustainable. Hapana, ukweli ndio huu na ni aibu kubwa kwetu. Basi badala ya kulalama lalama kuwa hawatupendi tufanye juhudi za dhati kutuondoa kwenye hali hii. Majibu yapo, yanawezekana lakini hatuna political will! Aliyetoa hizi takwimu ametusaidia sana na sasa kazi kwetu!

  Amandla!
   
 15. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Tutaendelea "kuangalia hoja kwa makini" lakini ukweli upo pale pale. The truth is, sanitation achilia mbali Africa, kwa Tanzania ni tatizo kubwa unfortunately no body cares! nendeni hata maofisini hapa hapa Dar...hali inatisha! Kwanza naamini hizo data zimetupendelea lakini the situation is worse than that! Personally sijawahi kuona kuona kijijini kwetu kama kuna hizi modern toilets..kama zipo hazizidi 1%. na hiyo 1% ni chafu hakuna maelezo.... Thats reality. na mwingine aje hapa aseme kwao ni vipi....tuache utani we are in deep shit!
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Thats reality. na mwingine aje hapa aseme kwao ni vipi....tuache utani we are in deep shit!

  Kweli tupu, mkuu....kweli tupu! Truer words have never been said!
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Laiti kila mwana JF hapa, angehakikisha yeye na familia yake wana choo kwa maana ya choo, huenda hiyo takwimu ingelikuwa tofauti.

  Lakina ukipita Dar kwa wajanja wa mjini, unakuta maji ya choo yanatililika kwenye mifereji. Mimi huwa najiuliza hivi hizi shule tunazosoma zinatufundisha nini?

  Usipoweza kutatua mazingira yanayokuzunguka, huna haki ya kusema umesoma.

  Sio lazima vyoo kwa maana ya West, lakini lengo la choo ni kuhakikisha mtu anayekuja baada yako haoni tena kinyesi chako. Enzi za mtu ni afya, Nyerere alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha kila familia ina choo, bahati mbaya wamekuja wajanja wa mjini, tumerudi hatua kumi nyuma.

  Hili pamoja na kuilaumu serikali lakini sisi kama watu lazima tu take initiatives, hakuna sababu ya kuzungukwa na uchafu. Ukizungukwa na uchafu ni uzembe wako binafsi pamoja na akili yako (samahani kama nimetumia neno kali sana) lakini hili la uchafu Dar mimi linaniudhi sana.
   
 18. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  kuna rafiki yangu mmoja nilipomueleza kuhusu ishu hii akasema hizo statistics mbona siyo ajabu!, jamaa anadai anakumbuka enzi hizo anasoma skuli, vyoo vyao vilikuwa haviendeki, ukiingia chooni lazima uvue shati otherwise ukitoka tu shati lote linanuka kinyesi,jamaa akadai kulikuwa kuna kichaka near by huko ndo wanafunzi walipokuwa wanashusha haja zao, jamaa anadai tena sometimes mnakutana wengi na stori mnapiga kama kawaida huku mkishusha mambo
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kuwa katika density levels za sehemu nyingi za makazi yetu inabidi serikali ( ya mitaa au kuu) inabidi iwajibike katika suala la saniation. Bila kuwa na centalized system katika sehemu kama Mwananyamala, Buguruni na kwengine tatizo hili litabaki kuwepo. Pit latrines (VIP or otherwise) zinachangia ku'comtaminate' ground water na maji yanayopita kwenye mabomba mabovu ambayo ndiyo tunayotatumia majumbami mwetu. Nakubali kuwa kuna haja ya kubadilika kitamaduni katika jamii yetu na kuchukia hali hii kwa dahti. Pengine hapo ndipo tutaweza kushinikiza serikali zetu kutoa kipaumbele kwenye suala la sanitation kama vile wanavyofanya kwenye suala la maji safi!
   
 20. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2008
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  kumbe basi tungefanya juhudi katika suala hili la vyoo, tusingekuwa na milipuko ya mara kwa mara ya kipindu pindu, tatizo la typhoid lisingekuwa kubwa sana,
  kuna wakati Tanzania mtu ukiwa na malaria kuna hatari ya kuwa na typhoid at the same time, kumbe sababu inawezekana inachangiwa na haya mambo ya sanitation.na gharama ya kutibu ugonjwa kama wa typhoid ni kubwa sana, kuepuka gharama hii ni vyema tukatatua tatizo la vyoo
   
Loading...