1963: Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Julius Nyerere akiweka pini katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. U Thant

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Pichani ni Julai 16, 1963, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Julius Nyerere akiweka katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant pini yenye alama ya mwenge wa taifa.

Kulia kabisa ni mwakilishi wa kudumu wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa wakati huo Chifu Erasto A.M Mang'enya na kushoto kabisa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika Oscar Kambona.

Mwenge wa taifa ulipandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro pindi Tanganyika ilipopata uhuru wake, mnamo tarehe 9, Desemba, mwaka 1961.

1639985943153.png

📸: UN Photo
 
Tuseme nchi ingeenda alivyotaka mwalimu Nyerere ni nini kingetokea ?

Hakuwa na tamaa ie mzee Kenyatta aliyejigawiya karibia ardhi ya nchi nzima.

Madini huku akijua kabisa chini kuna madini ila akasema ngojeni

Nidhamu ya kazi ilikuwepo.

All things changed sasa
 
Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa. Watu walihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.

Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera. Hata mwenyewe alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda.
 
Matatizo yalianza baada ya athari za sera ya Ujamaa. Watu wakihamishwa pasi kuwa na maandalizi ya kutosha. Vijiji vingi havikuwa na maji, umeme wala barabara za kueleweka. Pia dhana ya kufanya kazi kwa pamoja ilizalisha goigoi wengi.

Uchumi uliharibika sana baada ya vita ya Kagera. Hata mwenyewe alitangaza miezi 18 ya kufunga mikanda.
Sema sera ya vijiji vya ujamaa ingeundwa vizuri tungekuwa mbali.

Nahisi watu wa mikoa hii ya arusha Kilimanjaro hasa ndo waliingilia kupinga ujamaa.

Vile walijua vihamba vyao vitagawiwa.

Kufanya kazi pamoja kwa manufaa yenu wote ni nzuri.

Ni kama wasomi waliokuwepo hawakumsaidia mwalimu kuunda hivi vitu.

Mngezaliwa mjikute hivyo ni kuwa yangekuwa ndo maisha yetu.

Vita kweli vilipukuta uchumi wetu.

Akiba yote ikaishia vitani.

Ni kama tokea pale nchi haijakaa sawa tena.

Anyway nilimpenda sana Mwalimu Nyerere.
 
Collectiveness au Ujamaa unahitaji nidhamu ya hali ya juu. Kuwaamini wachache watunze pesa za wengi inahitaji kuweka kanuni madhubuti za adhabu itakayowapata wabadhirifu. Bila hivyo yanatokea yaliyotokea Urusi na hata hapa kwetu.
 
Tuseme nchi ingeenda alivyotaka mwalimu Nyerere ni nini kingetokea ?

Hakuwa na tamaa ie mzee Kenyatta aliyejigawiya karibia ardhi ya nchi nzima.

Madini huku akijua kabisa chini kuna madini ila akasema ngojeni

Nidhamu ya kazi ilikuwepo.

All things changed sasa

Kaondoka madarakani nchi imefilisika , Kauwa maelfu ya wazanzibari katika uvamizi wake na wengi wa viongozi wa Zanzibar alishiriki katika mauwaji .

Mzimu wake unaendelea kuitesa Tanganyika mpaka leo. Kila uchaguzi wanauliwa watu Zanzibar na majeshi yake yaliyopiga kambi kila mtaa pamoja na usalama wake
 
Chief Erasto Mang'enya ni Marehemu. Huyu alikuwa Mbunge wa Muheza kabla ya Luka Kitandula
Mang'enya aliwahi kuwa Spika wa Bunge la JMT

JokaKuu Mag3
Historia ya Mang'enya na Muheza inasisimua sana. Inataka nafasi kuilezea

Luka Kitandula alikuja kua Mbunge wa Muheza baadae. Naona na mwanae Dan Luka Kitandula anaendelea kua Mbunge wa Jimbo la Mkinga kwa kipindi cha tatu mfululizo sasa
 
Pichani ni Julai 16, 1963, Rais wa Jamhuri ya Tanganyika Julius Nyerere akiweka katika koti la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant pini yenye alama ya mwenge wa taifa.

Kulia kabisa ni mwakilishi wa kudumu wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa wakati huo Chifu Erasto A.M Mang'enya na kushoto kabisa ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Tanganyika Oscar Kambona.

Mwenge wa taifa ulipandishwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro pindi Tanganyika ilipopata uhuru wake, mnamo tarehe 9, Desemba, mwaka 1961.

View attachment 2050781

📸: UN Photo
Baba wa Taifa, Mzalendo wa kweli kabisa
 
U-Thant mwanadamu aliyezuia vita ya kinyuklia baina ya Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Dunia haimkumbuki sana bali wanaokumbukwa ni J.F Kennedy na N.S Khrushchev.
Wakati Mang’enya akiwa balozi wa kudumu wa Tanzania UN na JF Kennedy akiwa Rais, Mwalimu allionekana katika picha nyingi kipindi hiki. Kuna moja alikaribishwa na Kennedy kwenye presidential retreat.
 
Kwenye kupigania Uhuru hutosikia majina ya machifu...hawa walikuwa beneti na wakoloni
Ajabu Nyerere alivyopewa nchi Tu..
Akaleta hawa machifu kwenye serikali..

Mang'enya
Fundikira na wengineo

..nadhani kwa kiasi fulani Machifu walipewa jina baya ili kuhalalisha maamuzi ya serikali ya Tanu kufuta uchifu.

..mfano mzuri ni propaganda dhidi ya Mangi Marealle kwamba alikwenda UN na kupinga petition ya Tanganyika kupata uhuru.

..USHAHIDI wa maelezo na maoni ya Mangi Marealle UN upo na alieleza mambo tofauti kabisa na ambavyo Watanganyika tumedanganywa kwa muda mrefu.

..Mangi Marealle alitetea Watanganyika kupewa uhuru na alisisitiza suala la Watanganyika kupatiwa nafasi nyingi zaidi za masomo kama maandalizi ya kujitawala.

..Mangi Marealle pia aliulizwa kuhusu nafasi ya Machifu ktk Tanganyika huru na jibu lake lilikuwa anapendekeza tuige mfumo wa Machifu wa Ghana.

..Hata Nyerere alipokuwa UN ali acknowledge mchango wa Mangi Marealle kabla yake kuwa unashabihiana na msimamo wake na wa Tanu.

..Hili suala anayetaka kujiridhisha aende kwenye ARCHIVE za UN atakuta mahojiano ya Mangi Marealle, na ya Mwalimu Nyerere, mbele ya kamati ya udhamini ya UN.

..Ukiacha hilo, kuna ushahidi wa Machifu wa Usukumani kuunga mkono Tanu. Kazi ya kuwashawishi Machifu wa Kisukuma ilifanywa na Paul Bomani.

..Nyerere alimheshimu Paul Bomani kutokana na ushawishi wake na kazi kubwa alivyofanya kuipenyeza Tanu kanda ya Ziwa.

..Jambo lingine ni mchango wa FEDHA toka Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuendesha Tanu. Nimewahi kusoma kwamba kuna wakati kanda ya Ziwa ilikuwa inachangia 2/3 ya fedha za kuendesha chama. Kama sijakosea habari hii iko ktk kitabu cha John Illife kuhusu historia ya Tanganyika.

Cc Nguruvi3, Mamndenyi, Pascal Mayalla, Fundi Mchundo, MALCOM LUMUMBA
 
..nadhani kwa kiasi fulani Machifu walipewa jina baya ili kuhalalisha maamuzi ya serikali ya Tanu kufuta uchifu.

..mfano mzuri ni propaganda dhidi ya Mangi Marealle kwamba alikwenda UN na kupinga petition ya Tanganyika kupata uhuru.

..USHAHIDI wa maelezo na maoni ya Mangi Marealle UN upo na alieleza mambo tofauti kabisa na ambavyo Watanganyika tumedanganywa kwa muda mrefu.

..Mangi Marealle alitetea Watanganyika kupewa uhuru na alisisitiza suala la Watanganyika kupatiwa nafasi nyingi zaidi za masomo kama maandalizi ya kujitawala.

..Mangi Marealle pia aliulizwa kuhusu nafasi ya Machifu ktk Tanganyika huru na jibu lake lilikuwa anapendekeza tuige mfumo wa Machifu wa Ghana.

..Hata Nyerere alipokuwa UN ali acknowledge mchango wa Mangi Marealle kabla yake kuwa unashabihiana na msimamo wake na wa Tanu.

..Hili suala anayetaka kujiridhisha aende kwenye ARCHIVE za UN atakuta mahojiano ya Mangi Marealle, na Mwalimu Nyerere, mbele ya kamati ya udhamini ya UN.

..Ukiacha hilo, kuna ushahidi wa Machifu wa Usukumani kuunga mkono Tanu. Kazi ya kuwashawishi Machifu wa Kisukuma ilifanywa na Paul Bomani.

..Nyerere alimheshimu Paul Bomani kutokana na ushawishi wake na kazi kubwa alivyofanya kuipenyeza Tanu kanda ya Ziwa.

..Jambo lingine ni mchango wa FEDHA toka Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuendesha Tanu. Nimewahi kusoma kwamba kuna wakati kanda ya Ziwa ilikuwa inachangia 2/3 ya fedha za kuendesha chama. Kama sijakosea habari hii iko ktk kitabu cha John Illife kuhusu historia ya Tanganyika.

Cc Nguruvi3, Mamndenyi, Pascal Mayalla, Fundi Mchundo, MALCOM LUMUMBA
Ccm figisu walianza zamani sana
 
Back
Top Bottom