18% nini maana yake kwa watumishi wa umma wanaokopa kwenye bank za NMB na CRDB?

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
2,117
1,368
Nataka ufafanuzi kutoka kwa majuzi wa jambo hili kiundani, maana yupo ndugu yangu kaniambia kakopa 5.5M, kwa miaka minne , atarudisha 8.4M. Yaani riba ya 2.9M. Sasa najiuliza hii si kama 50%ya mkopo mzima? Hii 18% ni kokotolewaje? Mtaalamu aje atueleze mini maana ya kusema tofauti ,wakati uhalisia ni tofauti?
NB;
Wapo watakao nishauri niende moja kwa moja kuuliza ,lkn ukwel ukikutana na wale marketing managers wa lugha ambayo ipo promotional zaidi .Hivyo mliowahi kukopa hili likoje?
Asanteni.
 
20 parcent kwa mwaka mmoja...

ambayo kwa mwezi ni kama 1.7% ya principal amount uliyoikopa...

so miaka minne maana yake ni 20 *4 ambayo inaleta 80%

sema kwa sababu riba inapungua kwa jinsi principal amount inavyopungia ndio maana unaona gharama zinapungua..

ushauri mkuu kwa watu wote.. usipende kukopa bank huwa wanajali faida yao tu na riba kubwa sana bali nenda kakope saccoss
 
hapa nimekuelewa kumbe wanakokotoa kwa namna hiyo , je saccos zinaweza kumkopesha mtu hata kama si mwanachama wao?
 
USHAURI MZURI KULIKO YOTE...USIKOPE KAMA HUNA BIASHARA YA KWENDA KUFANYA. UKIDHANI UTAKOPA UKANUNUE TV, SMART FONI NA SABUFA UJUWE RIBA UTAIONA KUBWA NA KUZIDI KUCHANGANYIKIWA HATA UKINYWA SUPU.
hivi sasa umekuja vizuri,sio ile post ya nyuma. ushauri wako ni mzuri. Lazima mtu awe na business plan
 
Riba inalipwa kwa muda lets say hiyo 20% ni riba ya 20% kwa mwaka. Hesabu ziko hivi kama utakopa 10m kwa miaka miwili ila unalipa 300000 kila mwezi. Riba kwa mwezi itakuwa 20%/12 (kupata riba ya mwezi) halafu unazidisha na kiasi unachodaiwa kwenye pesa uliyokopa.

Kaa mfano huo riba itakuwa hivi:
Mwezi wa kwanza.
(20%/12) * 10m= 166,667

Mwezi wa pili.
(20%/12)* (10-makato ya mwezi wa kwanza)
0.1667 *( 10m - 133333)= 164,445

Kwa maana nyingine miezi ya kwanza utakuwa unalipa zaidi riba kuliko mkopo wenyewe. Na mikopo hii ina hssara moja ukikopa kwa muda mrefu na pesa za riba huongezeka zaidi.

Unaweza kutumia excel spread sheets kujua mkopo utakugharimu tsh ngapi jumla na kueavaluate options nafuu zaidi.
 
Ndio maana wana fomu za mkataba, kama umeridhia masharti yao kopa kama huwezi acha!
 
Mkuu naweza kukupatia ushauri wa bure kabisa. Ila uwe muwazi, au nifuate pm
 
Riba inalipwa kwa muda lets say hiyo 20% ni riba ya 20% kwa mwaka. Hesabu ziko hivi kama utakopa 10m kwa miaka miwili ila unalipa 300000 kila mwezi. Riba kwa mwezi itakuwa 20%/12 (kupata riba ya mwezi) halafu unazidisha na kiasi unachodaiwa kwenye pesa uliyokopa.

Kaa mfano huo riba itakuwa hivi:
Mwezi wa kwanza.
(20%/12) * 10m= 166,667

Mwezi wa pili.
(20%/12)* (10-makato ya mwezi wa kwanza)
0.1667 *( 10m - 133333)= 164,445

Kwa maana nyingine miezi ya kwanza utakuwa unalipa zaidi riba kuliko mkopo wenyewe. Na mikopo hii ina hssara moja ukikopa kwa muda mrefu na pesa za riba huongezeka zaidi.

Unaweza kutumia excel spread sheets kujua mkopo utakugharimu tsh ngapi jumla na kueavaluate options nafuu zaidi.
hii nimelewa kwa hiyo ataukataji wao wa fedha sio constant, yaani ukataji unaenda unapungua vile muda unavyosonga mbele.
 
Ndio inavyofanyika hivyo. Japo kwa wakopaji wakubwa kuna chance ya kunegotiate terms za kulipia mikopo
 
Mkuu naweza kukupatia ushauri wa bure kabisa. Ila uwe muwazi, au nifuate pm
Heshima yako mkuu.
Ni vyema ukatuelimisha wote hapa.
Maana ni wengi huwa tunafikiri kuhusiana na mikopo hii ya benki, kama njia ya kujikwamu.
 
Mkuu nimesema hivyo kwa sababu sera za mabenki kuhusiana na riba, loan to value ratio, masharti pia yanatofautiana. Kwa hiyo each case in utofauti.

Kwa mfano mikopo ya ujenzi wa nyumba huweza kuchukua hata miaka 20 au 15 na ina masharti tofauti. Maana yake ni kwamba ukikosea kuchagua una kazi nzito kwa miaka 15 mpaka 20 ijayo.

Hata hivyo kama ni Mfanyabiashara au unakopa lufanyia biashara ni vema kuhakikisha kwamba faida uipatayo kwenye biashara inaweza kulipia ile pesa unayolipa kila mwezi. Kinyume na hapo mkopo utaogharimu biashara yako.

Pia ni vema kutembelea bank zinazokuzunguka ili kujua riba wanazotoza. Usikimbilie NMB kwa kuwa wewe ni mteja huko nenda hata FNB. Hakikisha una taarifa za msingi za mabenki yote kuhusu riba na masharti ya kila bank ili mwishoni uangalie unafuu uko wapi (hili lina umuhimu usikope kwa mazoea unaweza kuta bank ambayo huijui riba ni 16%)

Cha mwisho kama una kipato interms of Dollars kakope kwa dollar bank kwa kuwa ni cheaper sana kuliko kukopa in Tshs.
 
vipi unaweza kujua Islamic banking inakopeshaje? Halafu umenishauri ni ku- pm, nmeona wengi wanahitaji maarifa haya. Mie nafikiri kukopa mwakani,nataka nijifunze kwa huyu jamaa yangu aliyekopa nione namna atakavyo invest, nataka nione knowledge gap
 
Back
Top Bottom