FisadiKuu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 8,108
- 13,346
Habari wanabodi,
Kwa wasio na ufahamu AMCOS ni vyama vya ushirika ambavyo vinakusanya mazao kwenye vijiji mbalimbali kwa niaba ya chama kikuu cha ushirika. Mfano wa vyama vikuu vya ushirika ni Kilimanjaro Native Cooperative Union (KNCU), Kagera Cooperative Union (KCU), Mtwara Masasi Cooperative Union (MAMCU). Hivyo hivi vyama vikuu vinakuwa na AMCOS ambazo ndio wawakilishi wake kwa kila kijiji. AMCOS hizi zinakuwa na uongozi wake na nguvu ya kukopo na kukopesha kwa utaratibu maalum uliowekwa na Serikali. Pia AMCOS hizi zinakaguliwa mahesabu yake na zinafanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
AMCOS zinajiendesha kutokana na ushuru wanaoupata kwenye mauzo ya mazao yao. Mfano, wanamkata kila mwanachama wake shillingi 70 kwa kila kilo ya zao alilouza. Hivyo kama AMCOS imepeleka mnadani Tani 800 ya zao fulani ushuru wake unakuwa ni Tshs. 56,000,000. Na pesa hizi zinatumika kwa shughuli mbalimbali za uendeshaji wa chama kama kulipa wazabuni, kulipa mishahara wafanyakazi, kulipa walinzi na kulipa wachukuzi n.k
Kutokana na msimu wa Korosho 2018/19 kuwa na changamoto kadhaa. AMCOS zilipata ushuru wa shillingi 14 tu ambao kwa uhalisia haukuweza kulipa madeni yote waliyonayo pamoja na mishahara ya wafanyakazi wake. Hivyo iliwalazima Chama kikuu kuongea na Mabenki ili AMCOS ziweze kukopeshwa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa mwanzo wa vyama vyao kwa Msimu huu wa 2019/2020. Bank za CRDB na NMB ambao ni wadau pia wanufaika wakubwa sana kwa wakulima wa korosho walikibali kuwakopesha fedha AMCOS kwa ajili ya uendeshaji wa vyama mpaka hapo watakapoanza kupata ushuru wao.
Kwa faida tu ya wasiofahamu, kwa mkoa wa Mtwara pekee korosho inaingiza zaidi ya Billion 800 kwa wakulima. Na asilimia 99 ya hizo billion 800 huwa zinapita kwenye bank hizi kubwa mbili.
Cha kusikitisha mchakato mikopo ulishaisha mapema kabla hata ya kufungua maghala yao ili wapate mikopo hiyo kwa ajili ya marekebisho na maandalizi mbalimbali. Kwa takribani wiki 3 sasa AMCOS zimekuwa zikizungushwa na bank hizi pamoja na kwamba walikamilisha vigezo vyote vya kupata mkopo.
Cha kusikitisha zaidi AMCOS ziliamua kutugeukia wadau wa korosho angalau waweze kupata kiasi cha kuweza kuendesha vyama vyao na ingawa hali zetu pia ni mbaya ila wadau wengi tumefanya kazi bega kwa bega na AMCOS kwa kusaidiana vijisenti tangia wanafungua maghala mpaka sasa ambapo mnada wa kwanza ni Ijumaa ya tarehe 1 mwezi wa 11 na kwakuwa kuna dalili ya wanunuzi wengi kujitokeza ndio Bank zimetuma statement kwa AMCOS kwamba wataanza kuwaingizia fedha walizoomba jumatatu ya wiki ijayo.
Huu ni ubabaishaji mkubwa na Usanii mkubwa wa hizi bank zetu na tunaomba viongozi mnaosoma hapa hili lifike kwa Waziri Mkuu au hata Mheshimiwa Rais na bank zipigwe stop kwa ulaghai wanaotaka kuufanya. Kwanza, riba ambazo wameziweka ni kubwa sana lakini pia hakutakuwa na maana ya kuwapa mkopo wa kuendesha chama wakati tayari walishauza mazao yao kadhaa na vyama vitakuwa vimeshapata ushuru wao mpaka hiyo wiki ijayo.
Inasikitisha mteja wako anayekuingizia mabilioni ya fedha anakuomba million 4 ya kuweza kujiendesha unamfanyia usanii. CRDB na NMB acheni uzandiki, kungekuwa na bank ingine imara lazima tungeshawishi hivi vyama viwahame.