12 wafa, 22 majeruhi ajali ya moto shuleni Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

12 wafa, 22 majeruhi ajali ya moto shuleni Iringa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbalamwezi, Aug 23, 2009.

 1. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Taarifa za kusitikisha ni kwamba wanafunzi 12 wamefariki kwenye ajali ya moto uliounguza bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi, Iringa. Wengine 22 wamejeruhiwa, kati yao vibaya sana.

  Mazishi ya pamoja


  Serikali imeamua kuwazika wanafunzi hao kwenye kaburi moja kutokana na ugumu wa kuwatambua baada ya kuungua sana.

  Wanafunzi walionusurika wanasema moto ulianza baada ya
  mshumaa mkuunguza chandarua wakati mwenye nao alipopitiwa na usingizi, lakini wakati wakijaribu kujinusuru, kuna mtu alikuwa (kwa maelezo, ni mwanamume mwenye nguvu 'sana' ) akisimama mlangoni na kuwazuia wasitoke, akiwaambia wale lazima wafie mle ndani.


  Wakati huo huo, wanafunzi hao wanasema walisikia pia harufu ya mafuta ya petroli.


  Ni nani? na kwa sababu gani hasa afanye hivyo? Je ni kweli chanzo cha moto ni mshumaa, au huyo mtu aliwasha kwa petroli? Je kuna nia gani thabiti ya kutafuta ukweli, huku taarifa za awali zikiunga mkono hoja kuwa chanzo ni mshumaa?

  Je, tumejifunza nini na hatua gani tumechukua toka majanga ya moto mashuleni ya miaka ya nyuma? Kuna tahadhari gani dhidi ya ajali za moto mashuleni? tuna vifaa vya kuzimia moto mabwenini? wanafunzi wanajua kuvitumia? Tuna mafunzo ya kukimbia hatari mashuleni?

  Kuna maeneo ya dharura ya kutokea wakati wa hatari?

  Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo tunapaswa kujifunza kwa vitendo sasa na siku zijazo, ili tupunguze vifo vya watoto wetu kwa namna hii.  Poleni sana Watanzania.
   
  Last edited: Aug 24, 2009
 2. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri wa hiyo nishati analijua hilo kuwa sehemu za kusoma mashule hazina umeme? Au kwa sababu ni ya binafsi???

  Poleni jamani mjue hii ndo ccm mliyoiweka madarakani vitu kama umeme wao wajua ni anasa.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCM kazi mnayo..Mshumaa umeunguza bweni Idodi wananchi wanawavaa ninyi?teh teh
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  jimbo la bwana lukuvi hili
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Sijui hata kama ana taarifa au habari naona yuko busy na mambo ya mbagala
   
 6. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  CCM ndio chama tawala kwa maneno mengine chama chenye serikali ndio kinabeba lawama mambo yakienda vibaya au sifa mambo yakienda vizuri. Kumbuka wabunge wanatoa ahadi kibao wakati wa chaguzi moja wapo ni kupeleka umeme majimboni kwao. Pia ni bunge la chama tawala in this case CCM ndio linapitisha bajeti za serikali hivyo kama halioni mikakati ya maendeleo kwenye hizo bajeti ikiwa ni pamoja na kufikisha umeme sehemu zisizo na umeme lawama apewe nani?
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  CCM hawawezi kukwepa lawama hizi. wao si ndiyo serikali watetea mafisadi, na wakifanya ufisadi wao wanaita vigi-cent...
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ajali ni ajali haina Chama. Mungu awalaze pema maiti wote .
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mlio fiwa na watoto wenu, poleni sana, tena sana. Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu mlicho wapoteza wapedwa na watoto wenu. katika janga la moto. Mungu ametoa na yeye mwenyewe amechukua.

  Mungu awafariji,

  Kwa majeruhi, Mungu awaponye na kuwatia nguvu. Baraka zake zikae nanyi na mfarijike na yeye Muumba wenu.


  POLENI
   
 10. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  poleni sana wafiwa na namuomba mola awape nafuu majeruhi wote.
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  kwa nini wakwepe wakati wameishatangazia taifa kwamba wao ndio serikali
  na bunge ni lao kwa hiyo kumweka kitimoto spika ni sawa kabisa (rejea maelezo ya makamba kuhusu kikao cha nec)

  sasa mtu akiilaumu serikali si ndio kuilaumu ccm au?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Aug 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Mungu azilaze roho za Marehemu pema peponi Amina.
   
 13. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mungu ametoa,Mungu ametwaa.KAZI YA BWANA IHIMIDIWE.
  Poleni wafiwa,majeruhi mpate nafuu na kupona mapema.
   
 14. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  nachukua fursa hii kutuma salamu zangu za rambirambi kwa rais Kikwete, mkuu wa mkoa Iringa, mkuu wa shule ya sekondari Idodi, na wafiwa wote. mungu awajalie afya njema wa wapone haraka wote waliopata majeraha
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hii ni ajali ambayo naweza kusema ni uzembe wa serikali. Politiksi zimetawala watendaji wa serikali badala ya kusaidia wananchi wake. Umeme kupelekwa sehemu fulani mpaka afe mbunge wa eneo hilo. Tulisikia baada ya Nyaulawa kufariki Serikali ikaanza kulaghai wananchi oooh tutaleta umeme, kisa walikuwa wanahitaji KURA. Uchaguzi ukafanyika, kura zikaibwa na SISIEMU ikachukuwa jimbo hakuna anayezungumzia tena Umeme. Kama nimekurupuka naomba mtu anisaidie hapa kunielimisha kama huyo mbunge aliyechukuwa nafasi ya Nyaulawa ameshaongelea suala la umeme huko ambako serikali ilitoa ahadi.

  Anyway, napenda kuchukuwa nafasi nyingine kutoa pole kwa wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa. Najua hivi sasa si wakati wa kutoa lawama wakati wengine wanaomboleza lakini ukweli utabaki pale pale. Serikali inatakiwa kuwa na priorities especially kwenye education. Kama hawa vijana wangekuwa na umeme haya ya mshumaa yangekuja vipi.

  Ni aibu kwa nchi kama Tanzania yenye rasilimali nyingi, magari mengi ya kifahari serikalini, tripu kibao za watendaji wa serikali kama Prezidaa kusikia wanafunzi wamepoteza maisha kwa sababu mshumaa uliteketeza bweni. Hivi kama kiongozi wa serikali, HOW WOULD U FEEL?
   
 16. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Pamoja na kuwapa wazazi na ndgu za watoto waliokufa na wale walioumia POLE, ni muhimu tukajifunza toka kwenye kila ajali kama hii.

  Ajali ya moto wa mshumaa! Mimi nadhani shule yoyote ya sekondari inapashwa kuwa na umeme wa genereta (kama iko sehemu ambayo haijafikiwa na national grid).

  Better still, umeme wa taa za shule sehemu kama hizo ingefaa utokane na solar power. Gharama ya solar power kwa ajili ya umeme wa taa peke yake sio kubwa.

  Napendekeza kwamba shule yoyote kabla ya kupata registration na kuruhusiwa kuchukua wanafunzi lazima ipate clearance ya District Fire Department kwanza. Na hawa itabidi waonyeshwe taa ziko wapi kwanza.

  Watoto wameshakufa wengi kutokana na moto wa mabwenini. Sasa inabidi kuweka sheria. Zimamoto wa kila wilaya watembelee mashule kuhamasisha kuhusu namna ya kukwepa hatari hizi. Tusisubiri janga lingine tena.
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  kwa kauli hizi ajali hazitaisha.
  Hata hivyo poleni sana wafiwa. Mungu awatie nguvu kwa kupoteza wana wenu wazuri.
   
 18. K

  Kamjuge Member

  #18
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asalam aleikum, ndugu zanguni? na wenye imani kama yangu pasi na kuwasahau wengine mlio na imani zingine bila kuwasahau wale wasio na imani kabisaaa.....!!!

  Pole kwa wafiwa wote na pole pia kwa majeruhi wote, Mwenyezi Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kumfanya mzima kuwa mfu na mgonjwa kuwa mzima, tumtegemeeni yeye kwa kila na kile tukifanyacho AMIN.

  Ni kweli ajali ni ajali, na ajali haina kinga. si dhani kama aliyewasha angejua hayo angelithubutu.

  Onyo kwa ndugu yangu Indume Yene na Kigogo.
  Will you guys lean how to differenciate between serious matters and nun serious matters?

  Thanks
   
 19. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hii ni ajali kama zingine, haina uhusiano na itikadi. ya chama fulani. Tumombe Mungu alaze roho za marehemu mahali pema peponi.
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  hii shule si ya binafsi, ni hizi shule zetu za kata.
  kuna kijenerata kimoja kibovu hivi,
   
Loading...