12 wafa, 22 majeruhi ajali ya moto shuleni Iringa

Nawapa pole wazazi wa watoto hawa ambao walitegema mengi toka kwa watoto wao. Inauma sana. Je Mamtum Mahiza unasemaje hapa??? Maana tumezoea comments zako za .....(ni kubwa mno kuliweka hapa). Hafai.
 
Ni ajali na wmarehemu walale mahali pema lakini Ngeleja ana kitu cha kutueleza kuhusu hili, akishindwa kutueleza...
 
Picha za tukio zima la moto. Mtaniwia radhi kwa wale watakao pata usumbufu kwa kuangalia picha hizi.
1251010732_the_main_entrance_to_the_center.jpg

Hili ndo bweni walilo kuwa wakilala wanafunzi inasemekana lilikuwa linabeba zaidi ya wanafunzi 400 kama mnavyo ona mlango ni mmoja tu wakuingia na kutokea.

Naibu waziri wa Elimu na ufundi Mwamtumu Mahiza na badhi ya viongozi wakiangalia maiti.

Maiti za wanafunzi 12 walio ungua moto.


Mabaki ya miili ya wanafunzi 12 ilivyo ungua.


Naibu waziri Mwamtumu akimwaga chozi.
 
Last edited:
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.Ameni. Suala la moto linataka kutuzidi nguvu sasa. Nilifikiria ingekuwa vema kama hizi sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kuwe na fire fighting systems. Baadae nimegundua kuna ugumu maana kama mshumaa ndio ulioleta moto hata kama utajenga tank, pumping system itataka umeme either wa nation grid au generator. hapo sasa ndopa kujipanga maana moto unakuwa tishio sasa kwa mali na usalama wa watu
 
MUNGU awaponye mapema waliojeruhiwa na pia azilaze roho za marehemu wanetu mahala pema peponi- AMEN
 
Hawa wanafunzi wamekufa kifo kibaya sana,
lakini pia nimesikia radio clouds asubuhi kwamba watoto wakati wanataka kutoka mlangoni kuna mtu alikuwa anazuia mlango kwa nje kwamba wasitoke , sasa sijui ni nini kinaendelea hapo.
 
CCM ndio chama tawala kwa maneno mengine chama chenye serikali ndio kinabeba lawama mambo yakienda vibaya au sifa mambo yakienda vizuri. Kumbuka wabunge wanatoa ahadi kibao wakati wa chaguzi moja wapo ni kupeleka umeme majimboni kwao. Pia ni bunge la chama tawala in this case CCM ndio linapitisha bajeti za serikali hivyo kama halioni mikakati ya maendeleo kwenye hizo bajeti ikiwa ni pamoja na kufikisha umeme sehemu zisizo na umeme lawama apewe nani?

Hivi milioni 200 zilizotengwa kwa ajiri ya chai na vitafunwa hazitoshi kuweka umeme ktk hilo eneo/jimbo au wilaya?? CCM Oyeeeeeee!!
 
Hawa wanafunzi wamekufa kifo kibaya sana,
lakini pia nimesikia radio clouds asubuhi kwamba watoto wakati wanataka kutoka mlangoni kuna mtu alikuwa anazuia mlango kwa nje kwamba wasitoke , sasa sijui ni nini kinaendelea hapo.

Kumbuka ya shauri tanga na kwingineko, sitaki kuamini kwamba dini zimehusishwa ktktukio hili lakini ni wazi kwamba shauri tanga ni dhehebu fulani la didi lilitekeleza mauaji yale.

Huwezi kuamini ni nia gani watu wanakuwa nayo hadi ufikie hatua ya kuchoma moto watoto wasio na hatia kisa tu eti imani yako. Sjui pia mmiliki wa ile shule ni nani na anafungamana na dini gani.
 
Fire in Tanzania Kills 12 Students

http://www.nytimes.com/2009/08/24/world/africa/24tanzania.html?_r=1&scp=2&sq=tanzania&st=cse

By AGENCE FRANCE-PRESSE
Published: August 23, 2009
DAR ES SALAAM, Tanzania (Agence France-Presse) - At least 12 children died and 20 others were severely burned when a fire razed a dormitory at a secondary school in central Tanzania, the police said Sunday.

"The fire is believed to have started after a net caught fire from a candle and spread throughout the dormitory," Evarist Mangala, the Iringa regional police commissioner, told Agence France-Presse.

He said the police were investigating the fire that struck Idodi Secondary School, about 285 miles southwest of Dar es Salaam, on Saturday evening.

The school has no electricity, Mr. Magala said, and students normally study by candlelight after dark.

The bodies were charred beyond recognition, so the dead will be buried Tuesday in a common grave in the Iringa district, said Mwantumu Mahiza, the deputy education minister.
 
Wastarehe kwa amani marehemu wote na mwanga wa milele uwaangazie..Poleni wafiwa mungu azidi kuwapa nguvu katika wakati huu mgumu na majeruhi wote mungu awape faraja na afya njema. Mshukuruni mungu kwa kila jambo... Waziri wa Wizara ya Elimu anapashwa kuwajibishwa. Hizi pesa wanazopewa kila wizara kazi yake ni nini naomba kuuliza? sasa nini faida ya kuwa na waziri wa Elimu kama hali za shule zipo namna hii kweli kwa karne ya 21, Tanzania bado watoto wetu wanasoma gizani? Nani anapitisha vibali vya shule kama hizi hata kuoperate shule ambayo haina hata umeme si ajabu hata vyoo tu.
 
Inashangaza na inatia uchungu jinsi shule zilizojengwa kwa mamilioni ya shilingi za walalahoi zinavyoungua na kupoteza maisha ya watoto wetu. Je nini kifanyike? Na je kuungua kwa mashule nchini Tanzania ni hujuma au nini?
 
..MUNGU awalaze pema peponi.

..Pole kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu hawa, na kuwapa nguvu wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu.
 
Asalam aleikum, ndugu zanguni? na wenye imani kama yangu pasi na kuwasahau wengine mlio na imani zingine bila kuwasahau wale wasio na imani kabisaaa.....!!!

Pole kwa wafiwa wote na pole pia kwa majeruhi wote, Mwenyezi Mungu pekee ndio mwenye uwezo wa kumfanya mzima kuwa mfu na mgonjwa kuwa mzima, tumtegemeeni yeye kwa kila na kile tukifanyacho AMIN.

Ni kweli ajali ni ajali, na ajali haina kinga. si dhani kama aliyewasha angejua hayo angelithubutu.

Onyo kwa ndugu yangu Indume Yene na Kigogo.
Will you guys lean how to differenciate between serious matters and nun serious matters?

Thanks

Nafikiri ingekuwa vyema ukaeleza serious na non serious matters ni zipi. Yaani watu kupoteza maisha kwa ulafi wa hao fisadiz leo imekuwa non-issues. Kama wangekuwa na umeme huo mshumaa ungewashwa????? Hicho ndicho nilizungumzia, serikali yetu imekalia kununua magari ya kifahari wakati wananchi wake wanataabika. Hii nayo unasema ni non-issue? Kama serikali yetu ingekuwa na priorities majanga kama haya yanaweza kuzuiwa au kuepushwa.

Kuna sehemu Mh. Zitto alikuwa anazungumzia jinsi pesa ya ujenzi wa barabara ya Manyovu ilivyopatikana. Hapa namnukuu Mh. Zitto "Mimi niliongoza timu ndogo ya Wabunge kufumua Bajeti ile na tukaja na wazo la kupunguza bajeti ya 'matumizi mengineyo' kwa asilimia 15 na fedha zote kwenda katika barabara. Katika mazungumzo haya ndipo nilipofanikiwa kupata fedha za Barabara ya Mwandiga Manyovu (kutoka 800m mpaka 7bn mwaka ule, na imekuwa hivyo kwa miaka iliyofuatia)".

Sasa ukiangalia hiyo pesa iliyopatikana kwa mradi huo toka milioni 800 hadi bilioni 7 (Go figure). Unafikiri kama viongozi wetu pamoja na wabunge wangeendelea kufanya hivyo kama alivyofanya Zitto tusingeweza kupata fedha kwa miradi mingine ya maendeleo kwa Taifa???? Hatuna PRIORITIES. Lakini siwezi kukulamumu maana nafikiri wewe miradi ya maendeleo kwa Taifa unaona ni kununua magari ya kifahari serikalini, kununua ndege mbovu kwa bei sawa na mpya, ununuzi wa Rada pamoja na ndege ya Rais kwa bei ya kifisadi, safari zisizoisha nje ya nchi kwa viongozi wa serikali. Kwa mtindo huu kweli tutafika tu.
Natanguliza shukrani Mzee Non-Issue.
 
Back
Top Bottom