Tabia ya kuibia majeruhi pale ajali inapotokea imekithiri Tanzania

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,740
2,243
Habari wanajukwaa! Naamini muko vema na kama umeamka hauko vizuri kwa namna yoyote pole sana!

Jamani binadamu wa kizazi hiki sijui tunaelekea wapi! Yaani watu sasa hivi wamekuwa na roho ngumu kuliko maelezo!.

Yaani siku hizi ikitokea ajali tu iwe kwa mtembea kwa mguu, boda boda, gari au mazingira yoyote bara barani, watu imekuwa ni haraka mno kufika eneo la tukio. Lakini cha ajabu jua kabisa utaibiwa kila kitu ulicho na cho wakati huo, yaani watu wanakimbilia eneo la tukio kuibia majeruhi na sio kuokoa yaani mpaka marehemu wanasachiwa masikini wa Mungu kama una hela zinaenda hizo aise.

Hakika hii ni tabia mbaya isiyo ya utamaduni wetu watanzania kwani tunapoteza hofu, upendo na utamaduni wetu kiasi hiki?!, inasikitisha na kushangaza sana.

Tabia hii imekithiri mno kwa sasa hasa katika maeneo ya mijini. Uwe umezimia au uko vizuri jua katika harakati kusadiwa utaibiwa simu, wallet na peza ulizo nazo zote.

Zamani ilikuwa ikitokea ajali mali zako kuna wasamalia wema wanazichukua na kukutunzia mpaka ndugu zako watakapofika na wanakabidhiwa bila shaka!

Leo ni mara chache sana na mara chache ubinadamu huo umebaki maeneo machache ya vijijini kabisa huko. Sijui ni njaa au kukosa ndio kukos ajira, tamaa au ni vitu gani mimi sielewi watu wa mjini.

Jamani tujifunzeni roho nzuri kesho kwa huyu kesho kwako ajali inaweza kukuta hata kama huna gari ndugu zangu utajisikiaje na wewe kuibiwa vitu vyako! Huu sio uingwana!
 
Jamii imebadilika sana
Heko kwa wanaharakati wa kipambana dhidi ya mila.na desturi bila.kuchuja zenye faida
 
Maadili yamebadilika mno vijana wamejawa na tamaa tu
Familia imekuwa mtego na siyo taasisi bora tena.

Serikali ipo bize kumsifia Rais badala ya kujibidiisha kwenye ustawi wa jamii ambayo tutapata viongozi wa baadaye
 
Sasa hata nisipokuibia mimi hivyo vitu watakuibia polisi tukikabidhi kwao, so ni bora mimi niliyewahi kwenye ajali nikakusitiri kwa kukufumba macho ukiwa umekufa kuliko polisi kuvichukua.
 
Habari wanajukwaa! Naamini muko vema na kama umeamka hauko vizuri kwa namna yoyote pole sana!

Jamani binadamu wa kizazi hiki sijui tunaelekea wapi! Yaani watu sasa hivi wamekuwa na roho ngumu kuliko maelezo!.

Yaani siku hizi ikitokea ajali tu iwe kwa mtembea kwa mguu, boda boda, gari au mazingira yoyote bara barani, watu imekuwa ni haraka mno kufika eneo la tukio. Lakini cha ajabu jua kabisa utaibiwa kila kitu ulicho na cho wakati huo, yaani watu wanakimbilia eneo la tukio kuibia majeruhi na sio kuokoa yaani mpaka marehemu wanasachiwa masikini wa Mungu kama una hela zinaenda hizo aise.

Hakika hii ni tabia mbaya isiyo ya utamaduni wetu watanzania kwani tunapoteza hofu, upendo na utamaduni wetu kiasi hiki?!, inasikitisha na kushangaza sana.

Tabia hii imekithiri mno kwa sasa hasa katika maeneo ya mijini. Uwe umezimia au uko vizuri jua katika harakati kusadiwa utaibiwa simu, wallet na peza ulizo nazo zote.

Zamani ilikuwa ikitokea ajali mali zako kuna wasamalia wema wanazichukua na kukutunzia mpaka ndugu zako watakapofika na wanakabidhiwa bila shaka!

Leo ni mara chache sana na mara chache ubinadamu huo umebaki maeneo machache ya vijijini kabisa huko. Sijui ni njaa au kukosa ndio kukos ajira, tamaa au ni vitu gani mimi sielewi watu wa mjini.

Jamani tujifunzeni roho nzuri kesho kwa huyu kesho kwako ajali inaweza kukuta hata kama huna gari ndugu zangu utajisikiaje na wewe kuibiwa vitu vyako! Huu sio uingwana!
Wadai marehemu haendi na kitu mbinguni."tuachie sisi" na ukibisha wanakumaliza.Naamini baada ya muda wanateseka sana kisaikolojia
 
Tena njia ya tanga ukiwa kwenye private umepata ajali,wanakuja watu
Na kuwamaliza kabisa

Ova
 
Back
Top Bottom