SoC04 10% ya fedha inayotolewa na Halmashauri kwaajili yakuwainua vijana kiuchumi zitumike kujenga vyuo vya ufundi kuendana na kasi ya teknolojia ya dunia

Tanzania Tuitakayo competition threads

Joyce laurent shija

New Member
May 25, 2024
4
2
Ili Tanzania kuendana na kasi ta teknolojia duniani ni lazima tuwe na vyuo vingi vya ujuzi angalau kila wilaya, ilikusudi wale wanao onekana wameshindwa mitohani basi baraza liwachague kwenye hivyo vyuo vya ujuzi kuliko kuwaacha wakae mitaani tu.

Hali zikisha kuwa ngumu za maisha ndo wanageuka kuwa majambazi, walawiti, mashoga, nk kwa sababu ya ugumu wa maisha nakukosa fedha kwaajili ya kuendelea na masomo.

Kwa sababu siyo wote wanaofeli mitihani hawana akili hapana wengi wao wanavipaji na ujuzi mkubwa sema nhi yetu imeshindwa kutoa nafasi ya vipaji mbalimbali kutokea madarasa ya chini kumgundua mtoto anakipaji gani astiki mpaka chuo kikuu.

Mapendekezo yangu fedha zinazotolewa almashauri ili ziwainue vijana kiuchumi ni bora zijenge vyuo vya ufundi ili kupata wataalamu wengi wa teknolojia kuliko kuwapa vijana ambao hawana uwezo wakuendesha biashara eidha kuwepo na vigezo vyakutolewa fedha hizo ili kuepusha upotevu wa fedha.
 
Tujiulize pia kwanza kwamba je? Hao vijana wanaoijua teknolojia hata sasa je? Wanalo soko la kufaa bidhaa/huduma zao sasa hivi kabla hatujafikiria kuongeza wengine.

Ps Nyongeza: jazia nyama insha zako zote dada angu shindano linataka maneno kama mia850 hivi.
 
Back
Top Bottom