exactly the same to me, mpaka sasa hua naota napaa angani mara kwa mara, i think utafiti wa kina ufanyike, mi hua naota matukio kisha nikiingia kwenye mitandao nakutana nayo. jana mchana wakati mke wangu ana andaa lunchi niliota nipo houston kwa mama mdogo eti mara nikasikia sauti ikinitakA niache dhambi na nimpokee yesu kama mwokozi wangu. nikawa nabisha huku nikitaka ushahidi kama kweli yesu ni muokozi matokeo yake kichwa changu kikabonyea kwa mbele na kutoa ishara ya msalaba eti nikawa nalia huku natubu mbele ya mzungu mmoja ambae alitajia jina lake,mara mke wangu akaniamsha na kuniambia kua nililala vibaya na nilikua naweweseka sana, nilivyostuka nikaamua ku google jina la yule mzungu mara akatokea kua ni admission officer wa houston bible school na nikakuta namba za simu. kwa kifupi nimechanganyikiwa sijui kwanini. mimi nimekua mpingaji mkubwa wa uwepo wa mungu na dini kama alivyo kiranga. anaeweza kunisaidia nitashkuru sana.