uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Tman900

    JamiiForums Tanzania Message za uchaguzi sasa zinakera

    Kila Dakika system ina unatuma Sms Ya Uchaguzi Imekua kero. Mbona kama Hamjiamini Mshasema Watu Wame elewa. Wanaotaka watakuja na wasiotaka mtaona kimya wanaendelea na shughuli zao. Note: "Hamjiamini na Mnachokifanya"
  2. Abdul Said Naumanga

    JamiiForums Tanzania Serikali ya Tanzania Yalaumiwa kwa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Human Rights Watch, limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuchukua hatua za haraka kurekebisha hali inayozidi kuzorota ya haki za binadamu nchini, kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. Kwa mujibu wa ripoti...
  3. BOB LUSE

    JamiiForums Tanzania Kujiandikisha Ili upige kura ni kurasimisha uharamia wa CCM katika uchaguzi

    CCM imejipanga kukalia viti Kwa hila, hata kumwaga damu na kupoteza watu kama tulivyo shuhudia Mwaka huu. Ni ujinga wa Hali ya juu kwenda kupanga foleni, ujiandikishe, upige kura wakati CCM wameshaandaa nani atashinda wakisaidiwa na vyombo vya Dola. Vizuri, tuwaachie wenyewe, ndani yao...
  4. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Askofu Dkt Shoo: Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi ni muhimu kwa Maendeleo ya Nchi

    Dkt. Fredrick Shoo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), amesisitiza umuhimu wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi kwa ajili ya chaguzi nchini Tanzania. Akizungumza katika mkutano wa kuwasilisha maoni ya CCT kuhusu miswada mbalimbali, Dk. Shoo alieleza kuwa mabadiliko haya ni muhimu...
  5. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Amos Makalla: Tulipokuwa tunajiandaa na Uchaguzi wenzetu walikuwa kwenye Maandamano!

    CPA Amos Makalla ametoa angalizo kwa vyama vya upinzani hususan CHADEMA kuwa kimeanza kutafuta visingizio vya kishindwa uchaguzi wakati ambapo hakijajiandaa kabisa na uchaguzi. “unachokipanda ndicho unachokivuna wenzetu wameanza kulalamika tulitegemea haya mana hawakujipanga Sisi Viongozi wote...
  6. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Amos Makalla ajiandikisha kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mikocheni

    Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Amos Makalla, leo Oktoba 16 ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi ya Serikali za Mitaa TPDC, Kata ya Mikocheni, Wilaya...
  7. Mwanongwa

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wananchi Mbeya Jiji ni kama wamekata tamaa ya uchaguzi

    Licha ya viongozi wa vyama na serikali kuhamasisha Wananchi kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura, hali ni tofauti na matarajio yao. Wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo sana katika zoezi hilo na hii ni kutokana na Wananchi kuona hakuna umuhimu wa kupiga kura. Nimepata bahati ya...
  8. G

    JamiiForums Tanzania Muda wa kujiandikisha uchaguzi wa serikali za mitaa kuongezwa?

    Zoezi linasuasua Hadi aibu! Licha ya viongozi wa kiserikali na wale wa kisiasa kuhamasisha watu wajitokeze lakini wamegonga mwamba. Watu ni kama wamepigwa ganzi hawana shauku Wala hamu na zoezi Hilo. Nikama wamesusa au wamekata tamaa. Uzuri ni kuwa wenye dhamana wamekiri zoezi kusuasua. Na...
  9. Lugano Edom

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Tujitokeze kujiandikisha uchaguzi Serikali za Mitaa

    Ndugu zangu, wanajamii Forum TUJITOKEZE kwenye kujiandikisha daftari la wapiga kura serikali za mitaa na vijiji. Kwani Halichukui muda mwingi .. Majina yako matatu, miaka yako... Sahihi yako tu. Dakika moja tu unakuwa umeondoka.
  10. S

    JamiiForums Tanzania LGE2024 CHADEMA yajipanga kuzuia watoto kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wabaini madudu haya

    Katika maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, chama cha CHADEMA kimebaini udanganyifu katika mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura. Mawakala wa chama hicho wamegundua kuwa kuna wanafunzi ambao wamejiandikisha ili kupiga kura, ingawa hawajafikisha umri wa miaka 18. Wanafunzi hawa...
  11. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania LGE2024 TAMISEMI kufanya mkutano na Waandishi wa Habari kujibu hoja kadhaa kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

    Wakuu, TAMISEMI wanatarajia kufanya mkutano saa tano hii Oktoba 15, 2024 kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
  12. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Rais Samia: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usichukuliwe poa, utatoa taswira ya Uchaguzi Mkuu

    Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Wiki ya Vijana katika Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza, leo 14 Oktoba, 2024. Amesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, utatoa taswira ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na Wananchi...
  13. Mganguzi

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi wa serikali za mitaa unapewa thamani kubwa namatumizi makubwa ya fedha lakini viongozi hao hawana posho Wala mishahara,

    Wasimamizi wa vituo vya kujiandikisha wapiga kura wanalipwa 350000, kwa mmoja ,kituo kimoja wakiwa wanne ni zaidi ya 1.2m ,kwa nchi nzima ni mabilion ya pesa !! Kwanini mnathamini mchakato na sio ajenda? Mkishawachagua hao viongozi wanaanza kujitolea hawana hata posho Wala mishahara ,ifike...
  14. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Ado Shaibu: ACT haturidhishwi na uandikishaji, Bila uandikishaji wa Haki, hakuna uchaguzi wa Haki

    Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema chama hicho haridhishwi na zoezi la uandikishaji wa Wapigakura linaloendelea hivi nchini. Ado Shaibu ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Dar es salaam. Amesema: "Bila...
  15. R

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kumbukizi ya homa za uchaguzi CCM 2020

  16. Amo1

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Kama uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 CCM ilipata ushindi 99.9%, Je tutegemee ushindi wa 100% 2024?

    Wakuu.. Najaribu kuwaza kwa sauti hapa. Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mafanikio Sana kwa chama Cha mapinduzi(CCM) katika chaguzi za serikali za mitaa. Walishinda kwa kishindo huku wakipita bila kupingwa kwa baadhi ya mikoa. Japokuwa wajuzi wa Mambo wanasema kuwa ule uchaguzi ulikuwa na dosari...
  17. Nyanda Banka

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu, tukajiandikishe

    Nichukue nafasi hii kuwakumbusha Watanzania wenzangu wote kuwa serikali za Mitaa ni muhimu na ndiyo sauti ya wananchi hivyo tujitokeze kujiandikisha katika daftari la mpiga kura. Bila kujali itikadi zetu hili ni jambo muhimu sana Kwa taifa letu kwa ujumla. Pia soma: Kuelekea 2025 - LGE2024 -...
  18. Nyendo

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Kilimanjaro: Kituo cha kujiandikisha kupiga kura kimewekwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa kitongoji ambaye naye ni mgombea wa CCM

    Kituo cha kujiandikisha kupiga kura kimewekwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa kitongoji ambaye naye ni mgombea wa CCM, je hii ni sahihi? Pia soma: LGE2024 - Uzi Maalum wa Kasoro na Rafu kwenye zoezi zima la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
  19. U

    JamiiForums Tanzania Donald Trump ahofia njama za Iran kumuua, aomba ulinzi wa ndege na magari ya kijeshi wiki za mwisho kampeni uchaguzi Mkuu Marekani

    Wadau hamjamboni nyote? Rais Biden asema ameshatoa kibali trump apewe ulinzi sawa na Rais aliyeko madarakani Soma Pia: Marekani yasema Iran ndo ilitaka kumuua Trump Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara Taarifa kamili hapo chini kwa kimombo: October 11...
  20. K

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Leo nimetumia haki yangu kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali Za Mitaa

    Leo ndiyo siku ya kwanza kwa wananchi kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Wananchi wanajitokeza kwa wingi lakini kwenye kituo nimewaona wakala wa vyama viwili tu yaani CCM na CHADEMA. Je Vyama vingine viko wapi?. Mfano ACT-Wazalendo, Chauma, TLP, NCCR sijawaona wakala...
Back
Top Bottom