Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.
Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.
Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.
Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
Maafisa Usafirishaji (Madereva bodaboda) wametakiwa kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa kwa kutokuwa tayari kutumika kwa namna yoyote katika vitendo vya rushwa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi mkuu 2025.
Wito huo umetolewa leo Aprili 17, 2025 na Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma TAKUKURU...
Baada ya kimya kirefu tangu kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, leo ubalozi wa Marekani hapa nchini umetoa tamko kuhusu hali ya kisiasa na wasiwasi wake mkubwa kwa serikali ya Tanzania kuhusu matukio ya hivi karibuni ya kuminya demokrasia na ukandamizaji kwa vyama vya...
Hamfai na hamna sifa ya kurudi. Hilo mnalithibitisha wenyewe ndani ya bunge.
Kila anayezungumza anasifia kila jambo kuwa Rais Samia kafanya yeye sasa nyie mmefanya nini kutumiza wajibu wenu? Msije mkasema wajibu wenu ni kupiga makofi kwa kila kiletwacho na serikali.
Yale ya wajibu wenu...
Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zuber anatarajiwa kuongoza Dua ya Kuiombea nchi na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwaombea Dua masheikh walitangulia mbele ya haki.
Mufti Abubakar amesema katika Dua hiyo inatarajiwa kufanyika kwa siku 2 tarehe 8 - 10 jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi...
https://youtu.be/UrmiHUuMW8k?si=8Zq7aoVlL4uoABVb
Ameeleza kuengua wagombea wa chama fulani tu ni dhahiri ajenda ya siri. Amesema Jeshi la Wananchi peke yake kwa sasa ndio linafanya kazi kwa uzalendo. Mambo ya kula kwa urefu wa kamba yake hawana
https://youtu.be/cfHzDQSD8vs?si=8UR5XPRjzS4yzanv
Mwanasheria msomi na Wakili wa LHRC amempinga Mkurugenzi wa Tume isio Huru ya Uchaguzi Tanzania Bwana Ramadhani Kailima kuwa ati CHADEMA wameondolewa kwene Uchaguzi wa 2025 kwa kukataa kusaini Kanuni za maadili ya Uchaguzi.
Wakili msomi Maduhu...
"Mwaka 2024/25 Ofisi ya Rais TAMISEMI iliidhinishiwa shilingi bilioni 254.82 kwa ajili ya kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 247.03 ni fedha kutoka serikali kuu na shilingi bilioni 7.78 ni fedha za mapato ya ndani ya...
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Doroth Semu ameeleza kuwa Chama hicho kitashiriki kikamilifu uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu kwenye nafasi zote za Udiwani, Ubunge, Uwakilishi na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Zanzibar.
Akizungumza na wanahabari leo Aprili 16...
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema wanaingia kwenye uchaguzi mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu wakiamini wao ni washindi katika uchaguzi huo kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Othman ameyasema hayo leo Aprili 16, 2025 wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi...
Sasa hivi inaonekana kama vile chadema inatumia nguvu kubwa ya ziada kupambana na matokeo ya kugomea kusaini maadili ya uchaguzi mbali na nguvu inayotumika kwenye No reforms No election.
Kama chadema wangesaini maadili ya uchaguzi kisha wakaendelea na harakati yao ya No reforms No election...
Kipindi Cha uchaguzi wa mwaka 2020 zilitolewa ahadi kede kede ikiwemo ujenzi wa "flyovers" Kwa junctions kama magomeni, Morocco, na mwenge.
Hizi zingesaidia sana kupunguza foleni katika Jiji la Dar es salaam.
Hadi sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mwingine na ubao bado unasoma "bila bila"...
Mbunge wa Mbogwe Nicodemus Maganga amebainisha kuwa watumishi wa serikali wanatakiwa kufanya kazi kulingana na matakwa ya kazi zao ili kutowaingiza wabunge katika wakati mgumu .
Amesema kumekuwa na watumishi wasio tenda haki na wajibu wao kutokana na utekelezaji kufanyika kwa asilimia 50 huku...
WASIRA AYAMALIZA NA MBELWA PETRO WA CHADEMA ZIARA YAKE YA KWANZA MKOANI KAGERA
Na Grace Mpondwe.
Katika hali isiyotarajiwa leo Machi 25, 2025 aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Biharamulo mwaka 2020 kupitia CHADEMA amekihama chama hicho na kujiunga na CCM akipokelewa na kukabidhi...
Mwenyekiti wa Umoja wa vijana CCM taifa (UVCCM), CDE Mohamed Kawaida amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa vijana wa CHADEMA wakilalamikia kunyimwa haki ya kuchagua na chama chao kwa kitendo cha kugoma kutia saini kanuni za maadili ya uchaguzi.
"Chama chochote cha siasa ambacho hakifanyi...
Wanabodi leo nimekutana na hii taarifa kuwa imepostiwa na BBC kwamba CHADEMA wameomba maridhiano ya kisiasa ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu. Je, ni kweli?
1. Wanachama wenzangu. Hii game tushashinda mezani.
2. Lililobaki, tupange Safu ya vyeo kuanzia PM, Mawaziri na vyeo vingine (Wakurugenzi, Makatibu Wakuu, RC, RAS, Wakurugenzi Halmashauri, DC, DAS) kila mtu apate.
Habari wakuu nimesikia mjadara sehemu wa sheria ya maadiri inataja vitu vifuatavyo
1, chama cha siasa au mgombea anaweza kusain fom ya maadili muda wowote kabla ya kampeni kuanza
2, uchaguzi ni haki ya kikatiba kwa vyama vyote ,itahesabika chama kimekubaliana na masharti kikitoa kauri ya...
Uchambuzi wa Kikatiba chini ya Ibara ya 74(11) na (12) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
Utangulizi
Demokrasia ya kweli hujengwa juu ya misingi ya kuheshimu Katiba, taasisi, na sheria. Katika muktadha wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kuna umuhimu mkubwa wa kufanya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.