Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu, Julai 7, ameahidi kutoza ushuru wa forodha wa angalau asilimia 25 kwa nchi kadhaa, zikiwemo Japani na Korea Kusini, washirika wawili wakuu wa Asia. Kwa Washington, hii inakusudiwa kuhimiza washirika wake wengine kutia saini mikataba ya biashara...