"Ukikimbia kuingia chumbani, wanakichoma moto," anasema Fatima, akielezea shambulio la hivi karibuni katika kijiji chake Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria. "Ukitoka nje na kuanza kukimbia, wanakupiga risasi."
Watu hao waliojihami kwa silaha, waliofanya shambulio hilo saa nane usiku (saa...